Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

[شَهْرُ ‌رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ]

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.” [Surah Al-Baqarah 2:185]
(Imetafsiriwa)

Mwezi wa Ramadhan uko juu yenu. Inakuleteeni baraka za Rehema za Mwenyezi Mungu (swt). Basi jiwasilisheni kwenye rehema za Mwenyezi Mungu (swt), kupitia matendo yenu mema. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «تَعَرَّضُوا لِنَفَحَاتِ رَحْمَةِ اللهِ، فَإِنَّ لِلهِ ‌نَفَحَاتٍ مِنْ رَحْمَتِهِ، يُصِيبُ بِهَا مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ» “Jiwasilisheni kwenye Rehema za Mwenyezi Mungu (swt), ambazo Yeye (swt) humpa yeyote Yeye (swt) amtakaye katika waja wake.” (Imepokewa na Al-Tabarani)

Mwezi wa Furqan (Upambanuzi), Ramadhan, umekujieni. Inakuleteeni ukumbusho wa Siku ya Badr, Siku ya Furqan, pamoja na ukumbusho wa kufunguliwa kwa Makka, kufunguliwa kwa Al-Quds na Vita vya Ain Jalut. Huu ni ukumbusho wa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Waumini wachamungu. Basi jiwasilisheni kwenye ukumbusho wa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt), kwa kuinusuru Dini yake. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ‌إِنْ ‌تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad 47:7].

Mwezi wa Furqan umekujieni. Unawajibisha kutofautisha baina ya haki na batili. Basi kuweni watiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw), na jiepushe na ukafiri, makafiri, unafiki na wanafiki. Hakuna hukmu inayostahili kutawala isipokuwa ya Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[‌إِنِ ‌الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf 12:40]. Hakuna hofu kwa kitu chochote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[أَتَخْشَوْنَهُمْ فَاللَّهُ أَحَقُّ أَنْ تَخْشَوْهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ]

“Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [At-Tawbah 9:13]

Mwezi wa Ramadhan umekujieni. Inawatazamia Maanswari (Wenye kunusuru) wa leo, ambao ni kama Maanswari wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), wanaomnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Mwezi wa saumu umekujieni, ili kutia ndani yenu adhama ya Uislamu, nguvu ya waumini, na uimara wa wachamungu. Mwezi wa Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) umekujieni, ili kuimarisha azma ya majeshi ya Waislamu, ili wapate kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ‌قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُمْ مِنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ]

“Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mungu.” [At-Tawbah 9:123].

Enyi Wapendwa Waumini! Mwezi wa Ramadhan umekuwa juu yetu kwa takriban miaka mia moja, ambayo inashuhudia mgawanyiko wetu, mizozo, kukitupilia mbali Kitabu cha Mola wetu Mlezi (swt), na kupotea njia yetu. Hakika Waislamu wanazozana hata juu ya siku ya kuanza kufunga, na siku ya Idd. Mwaka huu, Ramadhan inashuhudia mauaji katika Ardhi Iliyobarikiwa, yanayofanywa na wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia. Ramadhan inashuhudia makumi ya maelfu ya mashahidi na waliojeruhiwa. Ramadhan inafikisha kwa Mwenyezi Mungu (swt) maombi ya msaada kutoka kwa watoto, wanawake na waliofiwa. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) anatutosha na Yeye ndiye Mlinzi Bora wa mambo.

Enyi Umma wa Muhammad (saw)! Je, hivi ndivyo mnavyoukaribisha mwezi wa Mwenyezi Mungu (swt)?! Je, mnaipokea Ramadhan kwa mgawanyiko wenu, utawala wa madhalimu, na kuitelekeza kwenu Al-Masjid Al-Aqsa, Kibla cha kwanza cha Waislamu na eneo la Miraj ya Mtume (saw) kwenda mbingu za juu kabisa?!

Enyi Umma wa Muhammad (saw)! Vipi mnaipokea Ramadhan katika hali kama hii, na wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliamini Dua ya Jibril (as), «رَغِمَ أَنْفُ رَجُلٍ دَخَلَ عَلَيْهِ شَهْرُ رَمَضَانَ، ثُمَّ انْسَلَخَ قَبْلَ أَنْ يُغْفَرَ لَهُ  “Jihadharini na msiba wa mtu ambaye ameingiliwa na mwezi wa Ramadhan, kisha ukatoka kabla ya kusamehewa,” (imepokewa na Ibn Hibban)?! Vipi wale wanaokataa kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) watapata Rehema na Msamaha wa Mwenyezi Mungu (swt)? Je, hamjui kile kinachochuma Rehema na Msamaha wa Mwenyezi Mungu (swt)? Ni ibada ya kweli kwa Mwenyezi Mungu (swt). Ni kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Ni kuhukumu kwa mujibu wa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Ni Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Dola ya Khilafah ndiyo inayosimamisha Dini na kutoa ushahidi juu ya wanadamu wote, ili Waislamu waondolewe faradhi yao mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Enyi Umma Shahidi, Umma Bora Uliowahi Kuletwa Kwa Wanadamu!

Jukumu lenu kwa Uislamu ni jukumu kubwa. Linawajibisha kujitolea nafsi zenu na mali zenu kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Linawajibisha watoto wa Waislamu katika majeshi na vikosi jeshi kuwapindua watawala vibaraka na tawala za wasaliti. Linawajibisha kufuta mipaka inayosambaratisha nchi za Kiislamu. Linawajibisha kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida. Linawajibisha kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wake (saw).

Jukumu lenu kwa Al-Masjid Al-Aqsa linawajibisha kufanya kazi kwa nguvu zenu zote kuukusanya Umma wa Kiislamu, na majeshi yake, kupigana Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Hii ni kwa ajili ya kuikomboa Al-Aqsa, kuziondoa tawala za vibaraka zinazolipatia umbile la Kiyahudi njia ya maisha na kuendelea kuwa hai, na kuweka mipaka ya miradi ya Magharibi na Marekani inayoegemea kwenye "suluhisho la dola mbili" kwenye kaburi la sahau.

Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa hawaombi makombo ya misaada, huku wakikumbwa na milipuko ya mabomu na mauaji ya halaiki. Badala yake, wanatamani kupata heshima ya kuyakumbatia majeshi ya Waislamu wanapoingia kwenye Ardhi Iliyobarikiwa, kwa kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa Wana wa Israili. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[فَإِذَا جَاءَ ‌وَعْدُ ‌الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا]

“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Israa 17:7].

Enyi Watu katika Ardhi Iliyobarikiwa! Kuweni na subira, uvumilivu, na muwe thabiti. Subira, uvumilivu na uthabiti wenu hautakuwa na malipo isipokuwa Pepo. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَا تَيْأَسُوا مِنْ ‌رَوْحِ ‌اللَّهِ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ ‌رَوْحِ ‌اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ]

“Wala msikate tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” [Yusuf 12:87]. Hata kama watu duniani watakutelekezeni, Mola wenu Mlezi (swt) wa mbingu na ardhi anakutoshelezeni katika jambo hili. Yeye (saw) amesema, «لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ‌ظَاهِرِينَ ‌عَلَى ‌الْحَقِّ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ، حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ كَذَلِكَ» “Kikundi katika Ummah wangu hakitaacha kudhihirisha haki. Hawatowadhuru watu wanaowatelekeza, mpaka amri ya Mwenyezi Mungu iwajie na ilhali wako katika hali hiyo.” (Imesimuliwa na Muslim). Na kwa mujibu wa Imam Ahmad na Al-Tabarani, kutoka kwa Abu Umamah (ra) aliyesema, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِن أُمَّتِي ‌ظَاهِرِينَ ‌عَلَى ‌الحَقِّ، لِعَدُوِّهِم قَاهِرِينَ، لا يَضُرُّهُم مَن خَالَفَهُم، حَتَّى يَأتِيَهُم أَمرُ الله عز وجل وَهُم كَذَلِكَ» “Kikundi katika Ummah wangu hakitaacha kudhihirisha haki.  Maadui zao watawatenza nguvu. Hawatowadhuru watu wanaowatelekeza, mpaka amri ya Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla iwajie na ilhali wako katika hali hiyo.” Wakasema, يَا رَسُولَ الله! وَأَينَ هُم؟ “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)! Na ni kina nani hao? Yeye (saw) akasema, «بِبَيتِ المَقدِسِ وَأَكنَافِ بَيتِ المَقدِسِ» “Wako Baytul Maqdis na viungani mwa Baytul Maqdis.”

Ardhi Iliyobarikiwa iko kwenye ukingo wa ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Basi tafuteni ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya nafsi zenu, kwa dhati yenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na amri ya Mtume wake (saw). Achaneni na watawala madhalimu na washirika wa Shetani. Zingatieni Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt) aliyosema:

[الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ ‌فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا]

“Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu.” [An-Nisaa 4:76].

Kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa ni kadhia ya Ummah na Aqidah (itikadi). Ardhi Iliyobarikiwa itabaki kuwa moto mkali unaowakisha Uislamu katika nafsi za Waislamu, hadi Umma wa Kiislamu utakapoamka kutoka katika usingizi wake. Ama makundi ya wasaliti dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake, washirika wa Mayahudi na vibaraka wa Marekani, laana ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake, na waumini imewekwa juu yao. Sunnah ya Mwenyezi Mungu (swt) itatekelezeka juu yao kama inavyotekelezeka kwa wote wanaotakabari. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[مَلْعُونِينَ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا (٦١) ‌‌سُنَّةَ ‌اللَّهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلُ وَلَنْ تَجِدَ ‌لِسُنَّةِ ‌اللَّهِ تَبْدِيلًا]

Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa. (61) Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu. (62)” [Al-Ahzab 33: 61-2].

Tunamalizia kwa wito wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa waumini. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ (٧) وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ (٨) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ (٩) أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ دَمَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا (١٠) ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ ‌مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا ‌مَوْلَى لَهُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. (7) Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.  (8) Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao. (9) Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo. (10) Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na makafiri hawana mlinzi.” [Muhammad 47:7-11]. Kwa yakini, ni kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema,

[ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ ‌مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا ‌مَوْلَى لَهُمْ]

“Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na makafiri hawana mlinzi.” [Muhammad 47:11] Basi zingatieni, enyi watu wenye kuelewa.

H. 1 Ramadan 1445
M. : Jumatatu, 11 Machi 2024

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu