Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali ya Mpito katika Toleo lake la Pili ni Serikali ya Utendaji ya Kutekeleza Ajenda ya Magharibi Kafiri Mkoloni, Hakuna Kheri Yoyote Inayotarajiwa Kutoka Kwake
(Imetafsiriwa)

Leo, Jumatatu tarehe 5/12/2022, katika Ikulu ya Jamhuri jijini Khartoum, muafaka wa makubaliano ya kisiasa ulitiwa saini kati ya wanajeshi na Baraza Kuu la Vikosi vya Kutangaza Uhuru na Mabadiliko. Jenerali Al-Burhan, ambaye ana uhusiano na Amerika, alilazimisha vikosi vya kisiasa vinavyohusishwa na Uingereza kufanya makubaliano ya kudhalilisha ili kurejea kwa mara nyengine tena kwenye viti vya utawala, ambavyo ni tupu kabisa na mamlaka halisi.

Makubaliano haya yalijengwa juu ya katiba ambayo ilizalishwa kwa haraka na Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wanasheria mnamo tarehe 30/8/2022, ambayo vikosi vya kimataifa vilimiminika, na kuisifu kuwa ni waraka unaofaa kwa kuleta pamoja vyama. Katika taarifa ya pamoja, balozi za nchi tisa za Magharibi ziliipongeza; ikiwemo Marekani na Uingereza zilizoidhinisha rasimu hiyo ya katiba, na kusema: "Kanuni msingi zilizomo katika waraka wa wanasheria zitakuwa muhimu katika kufikia mfumo wa kutegemewa na imara wa serikali ya mpito yenye uongozi wa kiraia" (Sudan Tribune, 11/9/2022)

Mchuzi wa sumu umeivishwa kwa mikono ya wenyeji, baada ya nguzo mbili za kikoloni (Marekani na Uingereza) kukubaliana kuunda serikali ya mpito kulingana na rasimu ya katiba ya Jumuiya ya Kisekula ya Mawakili, ambayo inaasisi maisha kwa msingi wa hadhara ya Magharibi Kafiri, kuangamiza umoja wa nchi, na kuifungua Sudan kwa upana ili utajiri wake ufujwe na makampuni ya kibepari katika mabara yote, baada ya mikono ya watu wa nchi hii kufungwa pingu na kuzuiwa kutokana na mali yao.

Enyi Watu wetu wa Sudan:

Serikali ya mpito itakayoundwa kwa mujibu wa makubaliano haya ya kisiasa na katiba ya Chama cha Wanasheria, watu wa Sudan hawatanufaika nayo, kwa sababu ni serikali inayofanya kazi sawa na mtangulizi wake, iliyokuja kutekeleza ajenda ya mkoloni iliyotungwa katika tamko la kisiasa na katiba, kama ifuatavyo:

Kwanza: Kujitolea maisha kwa ajili ya hadhara ya Magharibi kafiri kwa kuondoa sheria na mifumo ya maisha kutoka kwa utawala wowote wa Shariah. Kinyume na mfumo wa Uislamu (Khilafah), makubaliano haya ya kisiasa yanabainisha katika Ibara ya (3) kwamba: [Sudan ni serikali ya kiraia, ya kidemokrasia, ya kifederali, ya kibunge ambayo ubwana wake uko kwa watu...], na inaeleza katika Ibara ya (6) kwamba: [Kudhamini uhuru na kushikamana na mikataba ya haki za binadamu, hasa mikataba ya haki za wanawake]

Hizi ni maana zile zile zilizoainishwa ndani ya katiba, ambayo inautabanni mfumo wa kidemokrasia wa Kikafiri katika Ibara ya (1/3), na badala ya ubwana kuwa kwa Sharia ya haki, katiba inaeleza kwamba ubwana uko kwa watu (Ibara ya 5), na. badala ya kushikamana na hukmu za Shariah, makubaliano hayo yanatoa hati ya haki za kimsingi na uhuru, katika Sehemu ya II kwa ukamilifu wake kuanzia Kifungu cha 7 hadi Kifungu cha 33, haitegemewi kufutwa au kuathiri maandishi ya Ibara ya (77/2). . Hati hii imekusudiwa kufisidi yale ambayo hayakuathiriwa na ufisadi wa zamani kuhusu wanawake, watoto na wanaume, kwa maagano na makubaliano ya kimataifa ambayo yanagongana na itikadi tukufu ya Kiislamu, kama vile CEDAW, Mikataba ya Haki za Mtoto, na mengineyo.

Pili: Kuangamiza umoja wa dola, kwa kupitisha mfumo wa shirikisho katika makubaliano ya kisiasa na katika kifungu cha 35 cha katiba. Mfumo wa Shirikisho hugawanya mamlaka na kuanzisha vyombo (maeneo) ambayo yanafanana zaidi na majimbo. Katiba inakwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa kila kanda itakuwa na katiba yake (Ibara ya 36/1), ambayo inalisha maeneo na makabila katika kupigania madaraka katika kanda hizo. Kinacho angamiza umoja wa dola ni kuufanya Mkataba wa Juba kuwa sehemu ya katiba (Ibara ya 4/2), ambayo ni makubaliano ambayo yalijikita katika kugawanya nchi katika maeneo matano ya kikanda au kikabila, na kuvunja umoja wa dola kwa kuweka mfumo wa Hawakeer (Kifungu cha 38/8); sababu kuu ya migogoro na mizozo ya kikabila na kikanda katika maeneo mbalimbali ya Sudan!

Tatu: Kuondoka kwa dola kutoka kwa wajibu wake wa kimsingi, kwa mujibu wa Shariah. Ambayo ni kushughulikia mambo ya watu kwa kuhakikisha utoshelevu wa mahitaji yao yote ya msingi, kama vile chakula, mavazi, nyumba, kutoa usalama, elimu, na huduma ya Afya kwao.

Kwa hiyo, masuala haya hayajajadiliwa kwenye makubaliano ya kisiasa na rasimu ya katiba ya mpito, hivyo unakuta ibara moja tu ya uchumi, na ibara moja ya huduma ya Afya, na ibara moja ya elimu, na ibara hizo hizo hazilazimishi wajibu wowote kwenye shingo ya dola! Kwa sababu katiba inatunga sheria kwa ajili ya ukusanyaji ushuru wa dola, sio hali ya ustawi wa dola.

Nne: Kuhusu uchumi, baada ya bingwa wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia (Hamdok) kutekeleza maagizo mengi ya mfuko huo; kuanzia kwa kuondoa ruzuku kwa bidhaa na huduma zote, kupunguza matumizi ya huduma za afya na elimu, kuwafanya watu kurithi bei za juu, umaskini, na ugumu wa maisha, Serikali ya Mpito inakuja na kutishia watu kuongeza kodi, na kupanua mwavuli wa kodi kulingana na maagizo ya bajeti ya mwaka wa 2023, ili kuwatoa wananchi kutoka katika mzunguko wa uzalishaji, ili mikono yao izuiliwe kutokana na utajiri wa nchi yao, iwasilishwe na wakubwa wa ukoloni katika Serikali ya Mpito kwenye sahani ya dhahabu hadi kwa mabepari walafi. Shirika la Viwanda lilitangaza kufungwa viwanda 5940 kati ya jumla ya 7350 kutokana na gharama kubwa za uzalishaji, pamoja na ongezeko la ada na forodha, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika hilo (AFP). Hivyo basi, serikali ya mpito itazidisha umaskini, bei za juu, na ugumu wa maisha.

Kwa watu wetu wa Sudan:

Sunnah ya Mwenyezi Mungu imetaka mabadiliko yasitokee yenyewe, bali lazima yatanguliwe na fikra kuhusu maumbile ya mfumo unaobadilisha maisha yetu na kuyageuza juu chini, ili tunaongozwe kwenye mfumo mtukufu wa Uislamu na Khilafah yake kwa njia ya Utume. Kisha tufuate fikra na vitendo, ili Uislamu ufikie katika mamlaka safi na takatifu mikononi mwa watu wanyoofu wenye madaraka na ulinzi, tukimtegemea Mwenyezi Mungu, na kutafuta msaada kutoka Kwake, na kukata kamba za makafiri wakoloni, kuunganisha ardhi na mbingu, ili ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt) utushukie:

(إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ)

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Ghafir: 51].

H. 11 Jumada I 1444
M. : Jumatatu, 05 Disemba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu