Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Akiwa Amevalia Vazi la Fedheha na Aibu, kwa Amri Kutoka Amerika, Al-Burhan Anatafuta Kusawazisha Mambo na Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Kupitia maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa Waziri wa Kigeni wa Amerika (Mike Pompeo), katika maongezi ya simu mnamo 02/02/2020, kiongozi wa Baraza la Mpito la Ubwana, Luteni Jenerali Abdul Fattah Al-Burhan, alisafiri akiwa dhalili, akivalia vazi la fedheha hadi mji wa Uganda wa Entebbe ili kukutana na Waziri Mkuu Netanyahu wa umbile la Kiyahudi mnamo Jumatatu 03/02/2020, ambaye mikono yake inatona damu za watoto wachanga, wajane na wazee!! Afisi ya Waziri Mkuu huyo wa umbile la Kiyahudi ilithibitisha katika ujumbe mfupi, kuwa Netanyahu na Al-Burhan walijadiliana njia za ushirikiano wa pamoja ambao utapelekea usawazishaji mahusiano kati ya pande hizo mbili!! Taarifa iliyotolewa na afisi ya Netanyahu pia ilitaja kuwa Waziri wa Kigeni wa Amerika aliandaa mkutano na Al-Burhan (Gazeti la Kiarabu la The Independent). Kwa mujibu wa gazeti la Al-Saiha lililochapishwa mnamo 04/02/2020, chanzo kimoja cha serikali kilizingatia kuwa maandalizi ya mkutano ni mojawapo ya ajenda muhimu zilizokuwa zikizungumziwa kupitia maongezi ya simu kati ya Al-Burhan na Waziri wa Kigeni wa Amerika Mike Pompeo jana!!

Sisi katika Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Sudan, tunawafafanulia Ummah wetu yafuatayo:

Dola za kitaifa za Sykes-Picot, zilizoundwa na makafiri wakoloni katika nchi za Waislamu; ni vidola vidogo vinavyofanya kazi kutumikia miradi ya makafiri Wamagharibi; kuuweka mbali Ummah na Aqeedah (itikadi) yao, kuwagawanya, kufuja utajiri wake, kuweka amani na maadui zake (umbile la Kiyahudi) na kuwaua watu wake, kama katika tukio la utawanyaji maandamano, na hata kuyaua mapinduzi ya Kiarabu, yaliyoanzia Tunisia, kupitia Misri, Syria, Libya, na kwingineko.

Watawala katika nchi za Waislamu; walinzi wa gereza kubwa, ni vibaraka wa Magharibi na ni vyombo vyake, wanatii amri zake, na kutekeleza ajenda zake, kamwe hawajali jamii zao, ahadi yoyote ya jamaa zao au makubaliano ya ulinzi, wanashindana kuwaridhisha mabwana zao Magharibi. Hivyo basi, katika wakati ambapo serikali ya majeshi huru ya mpito na mabadiliko iko imeshughulika kuzikandamiza sheria kutoka kwa baadhi ya hukmu za shariah ambazo zimeingizwa kinafiki ndani ya nidhamu ya sheria za Kimagharibi, ambayo imerithi udhaifu na fedheha tangu ule unaodaiwa kuwa uhuru, wakati huu Al-Burhan anakimbilia kukutana na muuaji Netanyahu, huku akizipiga na ukuta hukmu za Uislamu, na hisia za Waislamu, na ule unaoitwa mkusanyiko wa wataalamu ukiubariki uovu na uhalifu huu mbaya. (kituo cha Al-Horra)!!

Palestina ni ardhi ya Kiislamu, iliyofunguliwa na Khilafah Rashidah na kuvamiwa na Mayahudi, baada ya kuvunjwa Khilafah, ambapo waliasisi umbile lao juu ya mafuvu na damu za Waislamu, kwa ulegevu wa watawala wa Waislamu; vibaraka wa Wamagharibi makafiri wanatekeleza maagizo ya Trump na kutaka kuhama kutoka kuwa ni walinzi tu wa umbile la Kiyahudi, hadi kusawazisha mahusiano nalo, chini ya alama (Usaliti ya Zama Hizi), baadhi yao hufanya haya chini ya meza, na wapayukaji kama Al-Burhan, hufanya waziwazi, ni uovu ulioje huu wanaoufanya!

Watawala hawa hufanya bidii kuiridhisha Amerika, kuamsha hamu ya watu wa kawaida kuwa kuondolewa kwa Sudan katika orodha ya ugaidi kutatatua matatizo ya nchi hii, ni upotoshaji tu na ujinga pekee, kwani riziki hutafutwa kupitia kumridhisha Mwenye Kuruzuku, mmiliki imara wa nguvu. Na kupata nguvu na fahari ni kutoka kwa Mwenye uwezo kuliko wote, Mwingi wa nguvu, na Al-Haqq Mtukufu amesema Kweli:

 [يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُوراً]

“Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet'ani hawaahidi ila udanganyifu.” [An-Nisa: 120]

Enyi Watu wa Sudan: Al-Burhan na serikali yake anaendelea kuvunja vunja hukmu za Uislamu, matukufu ya Waislamu, na hisia zao, akitoka katika usaliti mmoja na kwenda katika usaliti mwingine akiigiza uhalifu wa serikali iliyong'olewa, ambayo iliitenga Sudan Kusini, ili kuwaridhisha Waamerika, na kunyamaza kwenu kimya juu ya usaliti wa watawala hawa na uhalifu wao, ndio kuliko mkaribisha adui yenu kwenu, kiasi ya kuwa asubuhi hutuingilia kwa usaliti mmoja, na jioni hutuingilia kwa usaliti mwingine mbaya zaidi! Hivyo basi, ishikeni mikono ya watawala hawa makhaini ili muwazuie kutokana na kuifilisi kadhia ya Waislamu nchini Palestina, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema: 

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.” [Al-ِAnfal: 27].

Enyi Watu wa Sudan:

Enyi Waislamu munaomuabudu Mwenyezi Mungu, wale munaomtii Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), wale mulio na udhu mikononi mwenu, munaosujudu mabapa ya nyuso zenu, na wale munaotamani Mabustani ya Pepo za Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakati sasa umewadia wa kuwa na ikhlasi, hivyo dhihirisheni kutoka kwenu matendo mema na mufanye kazi pamoja na wafanyakazi ili kurudisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, inayo tekeleza Uislamu, na kuwang'oa wakoloni makafiri kutoka kwa nchi za Waislamu na nidhamu zao zote, na kupeleka majeshi ili kuikomboa Palestina, na ardhi nyingine za Waislamu zilizovamiwa, ili muregee kuwa taifa bora kuwahi kutolewa kwa wanadamu, linalobeba kheri kwa walimwengu, na kutoa watu kutoka katika giza na kuwaleta katika nuru, ili jua la siku mpya lisichomoze isipokuwa ukweli wake uwe hii ndiyo njia pekee. Kwa hili, wafanyakazi wafanye kazi. 

 [إنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ]

“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbiya: 106]

H. 11 Jumada II 1441
M. : Jumapili, 09 Februari 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu