Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Kuchoma Msahafu ni Uadui Dhidi ya Kila Muislamu
(Imetafsiriwa)

Baadhi ya watu wenye chuki walipanga kuzichoka nakala za Quran Tukufu kwa njia ya kuchukiza, mbaya nje ya msikiti mmoja mjini Malmö Ijumaa iliyopita. Polisi waliwaruhusu kufanya hivyo mwanzo, lakini sio mbele ya msikiti huo. Mnamo Jumatano, tovuti kadhaa za vyombo vya habari ziliripoti kuwa polisi walivipokonya leseni za kazi hiyo kwa sababu za kiusalama. Lakini licha ya hayo, mnamo Ijumaa, picha na video nyingi zilijitokeza, zikionyesha paredi ambayo nakala za Quran zilikanyagwa na kutupwa uwanjani, katika uwanja ambao polisi walikuwa wameufunga kwa umma ili watu hao wenye chuki watekeleze kazi yao bila ya kukabiliwa na mtu yeyote. Swali linaloibuka hapa ni je, polisi waliwahadaa Waislamu kwa kueneza habari za kupokonya leseni, au waliruhusu Qur'an kukosewa heshima bila ya leseni?! Katika hali zote hizi, jambo hilo ni kubwa la kutosha kuzua wasiwasi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Uislamu kushambuliwa. Tunakumbuka vyema kutukanwa kwa Mtume wetu mtukufu (saw) mnamo 2007 kupitia vikaragosi viovu chini ya kisingizio cha uhuru wa kujieleza. Na mnamo 2017 mwanasiasa mmoja alitangaza kuwa Waislamu, kihakika, sio binadamu. Katika mwaka huo huo, Waziri wa Haki na Usalama wa Ndani wa Sweden Morgan Johansson aliwamithilisha Waislamu na watu wa Nazi na watu wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia, akiwalaumu kwa kueneza hisia dhidi ya Mayahudi.

Kwa muda mrefu, matukufu ya Kiislamu yamechafuliwa na ibada za Kiislamu kugeuza uhalifu ili kuwalazimisha Waislamu kujioanisha ndani ya thaqafa ya Magharibi, kutabanni fikra za kisekula, na kuachana na maadili yao ya Kiislamu. Maandamano ya usiku wa Ijumaa iliyopita yanaonyesha kuwa Uislamu unaenziwa nyoyoni mwa Waislamu, kwamba kamwe hawatakubali matukufu yao kutukanwa, na kwamba hawataachana na kitambulisho chao cha Kiislamu. Hivyo basi, Magharibi haitafaulu katika kuwayeyusha Waislamu ndani ya jamii yake iliyo haribika.

Hii ndio sababu Magharibi, ikiwemo Sweden, imeamua kutumia mbinu ya vitisho na ulazimishaji ili kuwashinikiza Waislamu kuachana na dini yao. Katika ripoti moja ya Chuo cha Kijeshi mnamo 2009, ripoti hiyo ilikadiria kuwa ufugaji ndevu na kwenda msikitini mara kwa mara ni dhihirisho la misimamo mikali. Tangu 2019, kila anayetaka kufanya kazi katika manispaa ya Trelleborg amehitajika kuwapa mikono jinsia ya pili, na katika mwaka huo huo uvaaji Khimar (mtandio) uliharamishwa shuleni, katika manispaa mbili za Sweden. Mnamo 2018, kiongozi wa wanademokrasia wa kikristo Ebba Busch Thor alitoa wito wa kupigwa marufuku Adhan (wito wa swala), na mnamo 2017 manispaa ya Ronneby ilijaribu kupiga marufuku kufunga saum katika shule. Manispaa ya Bromölla pia imejaribu kupiga marufuku swala makazini. Yote hii ni mifano ya kuonyesha waziwazi jukumu la wanasiasa katika kukariri uchochezi dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Upande wa kulia haukuibuka kutokana na ombwe. Bali, ni matokeo ya kimaumbile ya sera zinazotawala katika Magharibi kwa jumla, ikiwemo Sweden. Kampeni za vyombo vya habari dhidi ya Uislamu na Waislamu katika ulimwengu wa Kimagharibi zimeujaza upande wa kulia, ambapo zimekuwa ni vyombo vya kuwahangaisha Waislamu na kuwasukuma katika uwiano mkamilifu wa lazima kutokana na hofu juu ya upande wa kulia na nguvu yake inayokua. Unawaambia Waislamu kwamba mnakabiliwa na machaguo mawili, ima kuachana na dini yenu, kitambulisho chenu na utiifu wenu kwa itikadi yenu, mutabanni usekula na kuyayuka ndani ya jamii, na muonyeshe utiifu wenu kwa serikali, ili iwakumbatie na kuwalinda, au msiwe na chengine ila upande katili wa kulia utakao watafuna.

Enyi Waislamu:

Hairuhusiwi kwa vyovyote vile kunyamaza kimya wakati dini yetu, Mtume wetu (saw), na Ktabu chetu vinatukanwa. Ni wajibu wetu kupinga kila jaribio la kuhujumu matukufu yetu, na endapo hatutafanya hivyo, basi hili litachukuliwa kuwa ni khiyana kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), na msimamo wa udhaifu na uoga hata kama baadhi watajaribu kuuvisha barakoa ya hekima na utulivu. Hatupaswi kuziua hisia zetu dhidi ya jambo tukufu zaidi katika yale tunayoyapenda. Ni lazima tupambane vilivyo na makabiliano haya, kukaa mbali na ubadilishaji, athari na vitendo vya vurugu ambayo hayaruhusiwi na Uislamu. Bali, Magharibi hunufaika kutokana nayo katika kuchafua sura ya dini yetu na katika kuhalalisha vita vyake dhidi yetu. Makabiliano sahihi ni kuubeba Uislamu kama mfumo, kama ujumbe sahihi kutoka kwa Muumba, ili kupambana kwao Magharibi na kuuwasilisha kwa njia ya ushawishi wa kisiasa na kifikra.

Usekula unaporomoka na hakuna badali yake ila ujumbe wa Uislamu. Basi tuweni na imani nzito katika dini yetu na tuiwasilishe kama suluhisho la matatizo ya ulimwengu. Hapa Magharibi, sisi sio wachache wanaong'ang'ana kwa ajili ya kuishi au kupata mapato.

Bali, sisi ni mpanuko wa taifa la kale lililotawala ulimwengu kwa uadilifu kwa zaidi ya miaka elfu moja, na ni utekelezaji wa Uislamu pekee ndio utakaounganisha tena taifa hili na kuregesha utukufu wake. Sisi tuko imara katika dini yetu na twaweza kufanikisha na kutimiza mengi endapo tutajitambua na kufuata njia sahihi bila ya kukimbilia kwa yale yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu.

 (وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِين)

“Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini (wa kweli).” [Al-i-Imran: 139]

H. 10 Muharram 1442
M. : Jumamosi, 29 Agosti 2020

Hizb-ut-Tahrir
Sweden

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu