Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ]
Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. [Al-Ma’idah: 51]
(Imetafsiriwa)

Katika wiki za hivi karibuni, Tunisia imeshuhudia mmiminiko wa maafisa wa Ulaya. Mnamo Jumapili, Juni 11, 2023, Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni (ambaye ziara yake ni ya pili ndani ya wiki moja), akifuatana na Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte. Hili lilisadifiana na mkazo wa taarifa zinazoonya kwamba kuanguka kwa Tunisia kungeathiri Ulaya yote. Hii ni pamoja na taarifa za maafisa wa Marekani wanaotumia Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kulazimisha masharti na ushawishi wao, hadi Tunisia imekuwa kitovu cha kuingiliwa kati na mataifa ya kigeni na uwanja wa ushindani wa kimataifa. Mambo muhimu zaidi yaliyotangazwa baada ya ziara hizi za Ulaya ni:

- Kutoa msaada kwa Tunisia ili kupunguza uhamiaji kwenda Ulaya.

- Kuanza kuiunganisha Tunisia na Ulaya katika uwanja wa nishati mbadala.

- Kwa ahadi za kuunga mkono Tunisia katika mazungumzo yake na IMF.

Makubaliano haya yanawakilisha hatari iliyokaribia na hata uchokozi dhidi ya Tunisia, na ili kufafanua hilo, tunajikumbusha yafuatayo:

1. Ulaya inajumuisha nchi kubwa zaidi zilizo zikoloni nchi za bara la Afrika ikiwemo Tunisia, hivyo mtazamo wake kwa Tunisia ulikuwa na bado ungali ni mtazamo wa nchi ambayo lazima ikoloniwe, na hata kujitoa kwa wakoloni (askari wao) kutoka Tunisia haikuwa chochote bali ni mabadiliko ya mbinu za ukoloni, kwani Tunisia imebaki tiifu chini ya mkoloni. Jambo hili limejikita sio tu katika fikra za Kimagharibi, bali pia katika fikra za wanasiasa wa Tunisia wanaoiona Tunisia kuwa ni nchi ndogo ambayo haiwezi kuishi bila ya msaada, na kwamba msaada huu lazima kimsingi uwe wa Ulaya. Kwa msingi huu, uhusiano kati ya Ulaya na Tunisia ulianzishwa kwa misingi ya kikoloni.

2. Ulaya ya kikoloni iliyanyonya makoloni kwa njia mbaya zaidi, kwani iliwafanya vijana wa Tunisia kuwa ngao ya kibinadamu katika vita vyake, kisha, vita hivyo vilipokwisha, Ulaya ilifungua milango yake kwa wafanyikazi wahamiaji kutoka nchi za Maghreb, Afrika na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kujenga upya kile kilichoharibiwa na vita, kisha pindi dori yao ilipokwisha, ilitaka kuwaondoa na kufunga milango mbele yao. Na kuta za Ulaya zilianza kuinuka kila siku, na kuwatangazia mamilioni ya watu katika nchi za Maghreb na kusini mwa Sahara kwamba hawatakiwi. Hili ndilo lililofanya uhamiaji usio wa kawaida unaoendelea, pamoja na mikasa yake yote, kuongezeka hadi bahari ya nchi yetu kunuka maiti.

Kwa hivyo, suala la uhamiaji ni suala la kuzikoloni na kuzipora nchi na kuwafanya watu wake kuwa masikini, hadi nchi hizo zikashindwa kuwadhibiti watu wao, ambapo ziliamua kuwaacha wakitafuta maisha ambayo huenda yakawa na staha. Wakati huo huo, ni suala la watawala ambao wanaona siasa si chochote bali utiifu kwa Ulaya. Kutokana na hayo, "misaada" wanayodai kutoa kwa Tunisia kwa kweli si chochote ila ufadhili wa usalama wa "vita", ambayo kwayo Tunisia imejitolea "kupambana" na uhamiaji usio wa kawaida na kubeba mizigo ya Wazungu katika kuwafukuza wahamiaji, ambayo ina maana kwamba Tunisia itageuka kuwa kituo cha usalama kulinda kusini mwa bara hilo.

Ama kuiunganisha Tunisia na Ulaya katika uwanja wa nishati, ni uovu uliokithiri. Inamaanisha tu uporaji zaidi na udhibiti, utegemezi zaidi na udhalilishaji. Mpango wa nishati mbadala ni mpango muovu, wa kishetani ambao kwao makampuni zaidi ya kimataifa yatapenya ili kudhibiti vyanzo vya nishati mbadala na vyanzo vyake na yataidhibiti baada ya kudhibiti na uporaji wake wa nishati ya mafuta ya kisukuku, ambayo tafiti zote zinathibitisha kuwa itamalizika kabla ya mwisho wa karne hii, na kwamba Afrika Kaskazini itakuwa chanzo bora cha nishati mbadala kwa Ulaya, Watunisia watabeba gharama yake kwa kasi kupitia mikopo ya muda mfupi ambayo inazidisha nakisi, umaskini na utegemezi.

Tumeona na kusikia taarifa zote za Ulaya zikitaka kukamilika kwa makubaliano na IMF, na katika muktadha huu inakuzwa kuwa rais wa Tunisia ndiye anayekataa maagizo ya IMF na kwamba anataka makubaliano bila ya masharti. Na taswira ilionekana kana kwamba kila mtu kutoka ndani na nje alikuwa akitaka rais akubali huku akisitasita na kusitasita, na ukweli ni kwamba rais hajali; kwa sababu kwanza pingamizi haiko na IMF, ambapo inamaanisha kukubaliana nayo aghlabu inamaanisha kukubali masharti yake, na hili linajulikana na Rais Kais Saeed. Hata hivyo, aliifanya serikali yake na mawaziri kukutana na wataalamu wa IMF, hadi mpango ulipoandaliwa kwa ajili ya Tunisia na makubaliano katika ngazi ya wataalamu katikati mwa Oktoba 2022, lakini ukweli sio kukataa kwa rais, bali kukataa kwa IMF kukamilisha makubaliano; Kwa sababu

anataka kuziuza taasisi za umma na kuondoa kabisa ruzuku ya nyenzo msingi na mafuta kulingana na ratiba iliyolazimishwa na IMF, hatua ambayo rais "aliikataa" kwa sababu kwa sasa haiwezekani kuitekeleza, na mawaziri wa rais waliwasilisha pendekezo kwa Baraza la Wawakilishi. IMF ikiahidi kuinua hatua kwa hatua ruzuku ya mafuta kuanzia 2024 hadi kukombolewa kwake kikamilifu mnamo 2026. Hii inaashiria kuwa mazungumzo bado yanaendelea kushawishi usimamizi wa IMF kuyaakhirisha. Katika muktadha huu, Ulaya inataka "kuiunga mkono" Tunisia katika mazungumzo yake na usimamizi wa IMF, ambayo ina maana kwamba Ulaya inataka idhini na kujitolea kwa Tunisia na inataka mnyumbuko kiasi kutoka kwa IMF ili makubaliano yaweze kutekelezwa.

Je, maslahi ya Tunisia yako wapi katika hili? Na kusitasita na kugombana kuko wapi? Tunaona tu kuuzwa kwa nchi kwa namna ya kujinyima na kukataa, baada ya yule aliyemrithi kuiuza kwa namna ya mwanademokrasia aliyehusika katika ulimwengu huru.

Enyi Watu wa Tunisia, Enyi Waislamu: Kila siku mnashuhudia jinsi nchi yenu inavyogeuzwa kutoka dola ndogo hadi kuwa “kituo” tu cha mpaka kwa ukoloni mpya, na wa zamani wa Ulaya, na suala la hatari ni kwamba haya yanatokea huku kukiwa na domo tupu ambayo kamwe hayaishi kuhusu ukombozi, ubwana na uhuru. Mabadiliko ya kweli sio maneno bila vitendo, na tunachosikia kutoka kwa rais ni maneno ambayo yanagongana na vitendo na "makubaliano." Katika wakati ambapo rais anazungumzia uhuru na ubwana, anapokea viongozi wa Ulaya, wanazungumza naye kuhusu mambo ya ndani ya Tunisia, na anawahusisha katika suala hilo. Badala yake, tuliyoyaona katika wiki za hivi karibuni yanaashiria kuwa suala la Tunisia limegeuka kuwa suala la Ulaya kwa ushiriki wa Tunisia. Je, Italia ina uhusiano gani na mgogoro wa kifedha wa Tunisia? Je, hili sio suala la ndani? Na ni nani aliyehalalisha Kamishna wa Uchumi wa Muungano wa Ulaya, Paolo Gentiloni (katika taarifa za televisheni zilizoripotiwa na Shirika la Habari la Nova mnamo Alhamisi, Juni 8, 2023) kuzungumzia kuhusu uthabiti wa Tunisia na kuepuka ulipaji?!

Basi uko wapi uhuru wakati Gentilotti anasema hivi "tume ina mpango tayari ambao utaongezwa kwenye mpango wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa" na kusema: "Tunafanya kazi kuwezesha mpango mpya wa IMF"? Afisa huyo wa Ulaya anazungumza kuhusu programu za kiuchumi ambazo zimewekwa kwa ajili ya Tunisia, ikiwemo zile zilizoundwa na Mfuko huo na nyenginezo na Muungano wa Ulaya. Basi, huu hapa ni Muungano wa Ulaya ukimteua afisa mwengine wa kudumu nchini Tunisia ambaye kazi yake ni masuala ya kiuchumi (kusimamia, kufuatilia, au kudhibiti?) Hakuna tofauti. Hivyo basi ubwana uko wapi? Kwa nini Wazungu wanaamua hatma ya Tunisia? Je, huu si uchokozi wa wazi dhidi ya Tunisia?

Enyi watu wa Tunisia, enyi Waislamu: Ulaya ni mkoloni mkongwe, mpya, na ujio wa viongozi wao si chochote ila ni uchokozi unaoendelea dhidi ya nchi yetu, kuwakaribisha na kuwaingiza katika nchi yetu ni kumleta adui anayetaka uchokozi, je mutakaa kimya? Je, mapinduzi yenu hayakuwa ya ukombozi? Kwa nini tunakaa kimya wakati nchi yetu inakua kila siku kwa utegemezi na udhalilifu? Kwa nini tuko kimya juu ya mamlaka duni ambayo yameifanya Tunisia kuwa kimbilio la kila adui?

Sisi ni Waislamu, na hatutakuwa na izza isipokuwa kwa Uislamu, na tukitafuta izza kwengine kando na Uislamu, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha, na kumbukeni, mkipenda, kauli yake Aliyetukuka:

[وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.” [Al-Munafiqun 63:8].

H. 26 Dhu al-Qi'dah 1444
M. : Alhamisi, 15 Juni 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu