Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

HTI Inautaka Utawala wa Kidhalimu wa Uzbekistan Kusitisha Kuwatesa Wanaharakati wa Da'wah

 

Waandamanaji wapatao 500 wa Hizb ut Tahrir Indonesia waliandamana mjini Jakarta wakiitaka serikali ya Uzbekistan isitishe kuwakamata, kuwatesa na kuwaua wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Uzbekistan, Alhamisi (mnamo 7/7) mbele ya ubalozi wa Uzbekistan, huko Jakarta. Katibu wa msemaji wa HTI, Ruslan Roni alisisitiza kuwa wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Uzbekistan na wanaharakati wengine wa da’wah wanafanya kazi ya kueneza haki na kuwaita watu katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). “Hivyo basi hawastahili kufanyiwa ukatili kama kwamba ni wahalifu wakubwa!” alitetea. Alikumbusha pia vitendo vya kinyama havitasimamisha shughuli za da’wah ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan, isipokua kwamba karibuni hatua kama hizo zitaiangusha serikali ya Karimov. Wakati wa mazungumzo hayo, wazungumzaji walitaja majina kadhaa ya wanaharakati wa da’wah wasio na vurugu walioteswa magerezani, na kuwa waathiriwa wa serikali ya Karimov, ambao baadhi yao ni Rosebayev Hakeem Jan, Ooulmasaw Mrzaiev Bahadiri na Abdul Aziz." Serikali ya Karimov ili uregesha mwili wa Mrzaiev Abdul Aziz kwa familia yake kichwa chake kikiwa kimevunjika vibaya, macho yametoka, shingo yake imeshonwa nyuma ya kichwa chake na kifua chake kikiwa kimepigwa mafundo kutoka kitovu hadi kwa kidevu,” alisisitiza Irwan Saifullah wa Kamati ya HTI. Utawala wa Karimov sio tu uliwatesa wanaharakati wa Kiislamu wa Da’wah wanaolingania Sheria ya Kiislamu na Khilafah, bali pia walitishia familia zao. “Mamlaka za Uzbek ziliwakamata jamaa zao, kuwahoji na kuwashawishi wawe wapelelezi wa serikali,” alisema Irwan. Ilhali wakipiga Takbir, waandamanaji walikuwa wameshikilia mabango kadhaa ya maandamano kwa lugha ya Kiindonesia, Kiarabu na Kiingereza.

Miongoni mwa mabango yanasema, ‘Utawala wa kidhalimu wa Karimov uanguke! Simamisha Khilafah!’; ‘Sitisha kuwakamata na kuwatesa wanaharakati wa Kiislamu'; 'Ni wapiganaji wa Kiislamu sio magaidi 'na' Kuwa na subira Ewe Ndugu! Akipenda Mwenyezi Mungu, Khilafah itasimamishwa hivi karibuni! '(Mediaumat.com, 07/07/2011)

H. 7 Sha'aban 1432
M. : Ijumaa, 08 Julai 2011

Hizb-ut-Tahrir
Uzbekistan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Barua kwa Raisi wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu