Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Pande Zinazozozana Zinawaongoza watu wa Yemen kutoka Moto hadi Moto, Kuwatumikia Wakoloni...Enyi Watu wa Yemen, Jihadharini na Moto wa Bwana wa Ulimwengu
(Imefasiriwa)

Watu wa Yemen wanaendelea kukumbwa na moto wa mzozo baina ya Uingereza na Amerika, ambao umekuwa ukitanda nchini mwao kwa karibu miaka mitatu. Mzozo huu na mapigano yameharibu mazao na wanyama. Na licha ya mateso ya watu wa Yemen kutokana na njaa, umaskini, ukosefu wa huduma za kimsingi, kusimamishwa mishahara, uporaji wa bidhaa za nchi, kuenea kwa magonjwa na kupanda kwa bei, wale wanaozozania ushawishi na utajiri wa nchi kuwatumika wakoloni Makafiri hawajali mikataba au heshima juu ya watu hawa, kwa sababu wanawaongoza watu wa Yemen kutoka moto hadi moto na kutoka kwa vita kwenda kwa vingine, wote ili kukidhi mabwana zao Waingereza na Wamarekani. Uingereza ambao unasaidia mrengo wa Hadi, na ambayo pia ulikuwa unasaidia mrengo wa marehemu Ali Saleh kupitia Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), bado unajaribu kutunza maslahi yake kupitia mawakala wake mbele ya mawakala wa Kiiran wanaoungwa mkono na Amerika kama vile Mahouthi katika harakati za kaskazini na harakati za kujitenga kusini mwa Yemen. Amerika ikaagiza Saudi Arabia kuzindua oparesheni kali ya dhoruba ili kuwapa uhalali wa kuwa katika hali ya kukandamizwa ilhali wao ndio walikuwa wakandamizaji, kwani oparesheni hii haikuundwa kuwaondoa Mahouthi…Na leo tunaona matokeo ya hii dhoruba kali ilivyofanya kazi kuimarisha Mahouthi, hususan baada ya kumuua Ali Saleh (kibaraka wa Uingereza) ambaye UAE ilikua inaandaa jukumu lake la kishujaa la kufanya kazi kupindua Mahouthi na kuungana na mrengo wa pili wa Uingereza: mrengo wa Hadi. Lakini, Amerika kupitia Mahouthi waliharibu mpango huu kwa kumuua Ali Saleh, hivyo Uingereza ukawa na mrengo mmoja tu, haukua na nguvu kusonga mbele ama kuwa na ushawishi dhidi ya vibaraka wa Amerika nchini Yemen.

Ali Saleh, kibaraka wa Kiingereza ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 33, alitumikia maslahi ya Muingereza na kueneza ufisadi katika nchi yenye utajiri, na haijalishi jinsi utawala ulijifanya umeuvaa Uislamu, bado unabakia ni utawala kijamuhuri uliojivika usekula ambapo watu waliishi mbali na Uislamu na vipengee vyake na iliandamana na watu kutoka vita hadi vita. Watu wamekuwa wakimuomboleza Ali Saleh kama mtu na sio kama utawala, na walifanya kutokana na hisia na kushtushwa na mauaji yake kwa njia ya uchochezi na ya kinyama na Mahouthi ambao ni wabaya kuliko yeye machoni mwa watu…

Pande zote zinazozozana hazina haja na Uislamu isipokua chuki za kimadhehebu zinazotumiwa kuwaleta wafuasi na kuwahimiza kupigana. Lakini jambo la kusimamisha Uislamu kama njia ya maisha itakayo simamia mambo ya maisha, hilo haliwahusu na si katika malengo yao. Bali wanatafuta kupigana chini ya kauli mbiu ya “vita dhidi ya ugaidi”, kutumikia Amerika na Magharibi, na wanakubaliana juu ya nidhamu ya Kijamhuri na dola ya kisekula ya kidemokrasia!!

Mahouthi, ambao hawakuorodheshwa na Amerika kwenye orodha ya magaidi, kama vile haikujumlisha mama yao Iran na vyama vyake, na imekua kimnya juu ya yale wanayofanya, na imekua ikifanya kazi kuwahalalisha, kwa kisingizio kuwa wao ni wachache na wanakandamizwa. Hivyo basi, watu huwakuta wakitukuza nyumba ya Mtume (saw), ingawa vitendo vyao na nidhamu wanazotumia kusuluhisha mambo yao ni sawa na nidhamu zinazotumiwa na waliokua kabla yao, na hazihusiani na Uislamu. Bali, ni dola za ukandamizaji za kipolisi zinazokosea Uislamu pale wanapouonyesha kama mradi wa mauwaji na mapigano na vita vya kimadhehebu!!

Ama kusini mwa Yemen, harakati ya kujitenga ya mrengo wa Muamerika inawatingisha vibaraka wa Uingereza, licha ya kua UAE inajifanya kuwa inawajali na kuwaunga mkono, ili kuwadhibiti na kujua kile wanachokipanga na kuwaharibia mipango yao. Ni aibu kupata hawa wanaojitenga wakiwa dhidi ya wimbi la Ummah wenye kiu ya Umoja, na kuondoa mipaka ya kikoloni na kuiokomboa Al-Aqsa kutoka kwa utawala wa mayahudi; wakati huu, wanataka kujitenga jambo ambalo ni haram kisheria na kukataliwa na hali halisi, na tunatamani wangekua na busara.

Enyi watu wa Yemen! Mumeangamizwa na vita, vita ambavyo hamuna chochote kuhusiana navyo, ila viko dhidi ya maslahi yenu, hivyo basi vinawachoma na kueneza uharibifu kwa kile kilichobaki katika nchi yenu. Tunawaomba mufanye kazi kukomesha vita hivi na mizozo kwa ufahamu uliotokamana na Iman na hekima yenu munayojivunia. Laajabu munawawacha watoto wenu waangamie katika vita hivi, na kuwahimiza katika vita kama watu wa Jahiliya waliowauwa watoto wao kwa kuogopa umaskini. Hayo yote kwa sababu ya ukosefu wa ajira, umaskini na njaa iliyo sababishwa na hawa watu wanaozozana, waliowafikisha katika hali hii, hamuelewi?!

Hao wanaopigania mamlaka na utajiri wa nchi ni magonjwa yasiyopona. Wasipokubaliana wanawaua, wakikubaliana, wanapora mali yenu na kuwatia njaa, na hakuna suluhisho kwenu au uokovu isipokua kufanya kazi kuregesha Khilafa ya Uongofu ya kwa njia ya Utume. Ndio itakayounganisha kutawanyikana kwenu, kumaliza shida zenu na kuondoa chuki na dharau za kimadhehebu, ukabila na ubaguzi wa rangi waliopanda mioyoni mwenu. Juu ya yote hayo, itaregesha utawala wa Mwenyezi Mungu na Shariah Yake katika maisha yenu ili Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wawe radhi na nyinyi, na wakaazi wa Ardhini na Mbinguni wawe radhi na nyinyi, na mutakua watu wa Imani na hekima wa kweli wakati ambao Imani na hekima zimepotea ikiwa ni natija ya kuacha dini yenu na kuyatia sumu mazingira ya nchi kwa mawazo ya Kimagharibi na nidhamu zake fisadi zinazo zilizogonga eneo lenu la Iman na hekima kwa kuwatia upofu.

Enyi watu wa Yemen! Suala lenu ni kutawala na kutekeleza Uislamu katika maisha halisi, si suala la mzozo juu ya utawala ama madaraka bila njia dhahiri na katiba madhubuti, kwa hivyo musiruhusu miito ya usekula, dola za kiraia, madhehebu na maeneo, na matokeo ya Umoja wa Mataifa kuwaongoza. Mukitaka haya, Mwenyezi Mungu atawaekea wakoloni na dola zao za dhuluma ndani na nje, na mutatawanyika vibaya kama mababu zenu wa zamani, ambao Mwenyezi Mungu (swt) aliwaambia:

[فَقَالُوا رَبَّنَا بَاعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَاهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ]

“Lakini wakasema: Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu. Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru.” [Saba: 19].

Watu wa Yemen waliishi kama sehemu ya Ummah wa Kiislamu chini ya kivuli cha dola ya kwanza ya Kiislamu iliyoanzishwa na Muhammad (saw). Ummah wa Kiislamu ulikuwa taifa moja, chini ya kiongozi mmoja na bango moja. Waliishi maisha yenye hadhi na kwa kweli walikuwa watu wa Iman, hekima, huruma na rehema kwa njia ngumu na hali nzito, lakini fikra za Kiislamu na vipengee vyake ndivyo vilivyo badillisha maisha yao na kuboresha Tabia zao. Lakini baada ya kuja mkoloni na kutuwekea hadhara yake tukawa hivi tulivyo!!

Tunawaomba mufanye kazi ya mageuzi makubwa juu ya hawa watu wajinga wanaocheza kamari na hatima yenu na kuwaongoza kwenye uharibifu dhahiri, na musikae nyuma ya watawala wanaojisalimisha kwa ukweli unaodhalilisha. Na tunawaonya musichukue maisha yenu kutumikia mipango ya makafiri. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[ولَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113]

Namujue kua njia ya mabadiliko ambayo lazima yafuatwe katika kubadilisha ukweli wenu wa machungu ni njia ya bwana wa mtume, Muhammad (saw) aliyeanzisha kupitia hiyo mamlaka ya Uislamu na dola ya kwanza Madina, na kwa hilo washindanie wenye kushindana.

H. 22 Rabi' I 1439
M. : Jumapili, 10 Disemba 2017

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Yemen

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Miaka Tisini na saba ya Kejeli na Hasara »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu