Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Enyi Majeshi (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?”
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Matembezi yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 28 Machi 2025 sawia na tarehe 28 Ramadhan 1446 kuanzia Msikiti wa Al-Fath yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuinusuru Gaza dhidi ya uadui wa Marekani Mzayuni, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunis na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka Tunisia ya kijani. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likisomeka, “Enyi majeshi! (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?)”