Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  7 Jumada II 1443 Na: Afg. 1443 H / 08
M.  Jumatatu, 10 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umoja wa Mataifa Umeanzisha Mchezo wa Kisaikolojia na Kisiasa kwa Watu wa Afghanistan Chini ya Pazia la Misaada ya Kibinadamu.

 (Imetafsiriwa)

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa dolari bilioni 1.5 zimekusanywa kushughulikia hali ya watu wa Afghanistan. Pia aliongeza majira ya baridi kali yanayafanya maisha kuwa magumu kwa Waafghani.

Baada ya kutekwa Afghanistan na Imarati ya Kiislamu, taasisi za Kimagharibi zimekuwa zikizungumzia mara kwa mara janga la kibinadamu nchini Afghanistan, zikitoa machozi ya mamba huku mara kwa mara zikizungumzia misaada hewa kupitia kuongeza takwimu zisizo na maana za kushughulikia mahitaji. Kwa hakika, Umoja wa Mataifa na taasisi za Kimagharibi, kwa jina la misaada ya kibinadamu, zimeanzisha aina ya mchezo wa kisaikolojia na kisiasa kwa watu wa Afghanistan.

Sehemu kubwa ya msaada unaozungumzwa na Umoja wa Mataifa ni msaada hewa ulioahidiwa ambao una masharti ya kisiasa. Dola za kikoloni, kwa jina la misaada ya kibinadamu, zinajaribu kulazimisha ajenda zao za kisiasa na kijasusi kwa watawala wa sasa wa Afghanistan ili kutumia msaada huu kama kichocheo cha shinikizo la kisiasa ili hatimaye kuzuia kuanzishwa kwa mfumo wa Kiislamu na utabikishaji wa Sharia ili ulinganizi wa Uislamu usiende zaidi ya eneo la Afghanistan.

Kinyume chake, historia ya misaada ya kigeni na ya kibinadamu pia inathibitisha ukweli kwamba misaada hiyo haijawahi kuleta ustawi wa kiuchumi na ukuaji wa nchi, lakini kwa hakika imeweka mizani ya utegemezi na kurudi nyuma kwa nchi hizo.

Uislamu wetu mwema kamwe hauturuhusu kupokea misaada ya kifedha na/au mikopo kutoka kwa dola za kikafiri na taasisi za kikoloni kwa sababu daima kuna malengo fulani ya kisiasa, kiuchumi na kijeshi nyuma ya misaada hiyo ambayo inawaruhusu makafiri kutawala na kupata ushawishi wao juu ya Waislamu. Kwa hivyo, makubaliano na mapatano yoyote, ikiwemo kutafuta misaada ya kifedha na kibinadamu, kuchukua mikopo kutoka kwa serikali za Magharibi na taasisi za kimataifa zinazopelekea kutawaliwa na ushawishi na vile vile kuweka matakwa ya kisiasa ya Waislamu mikononi mwa makafiri, hairuhusiwi katika mtazamo wa Kiislamu.

 [وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini!” [An-Nisaa: 141].

Hivyo basi, njia pekee ya kutoka kwa matatizo ya sasa ya kiuchumi ni kwa kuiunganisha Asia ya Kati na Asia ya Kusini chini ya bendera ya Uislamu na Afghanistan kuwa kitovu cha Dola ya Kiislamu. Maeneo haya mawili ambayo idadi kubwa ya Waislamu wanaishi sio tu yana uwezo mkubwa wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi bali yana uwezo wa kuwa na dola kuu. Kuunganishwa kwa ardhi hizi chini ya mwavuli mmoja [Uislamu] kutawatoa Waislamu wa eneo hilo kutoka kwenye mfadhaiko, na kuwapelekea Waislamu kujitosheleza kiuchumi kwa kutumia maliasili nyingi na nafasi ya kipekee ya kistratejia. Kwa hivyo umefika wakati sasa wa kuvunja mipaka iliyolazimishwa na kuitupilia mbali sera ya maombi kwa kusonga pamoja kuelekea maisha yenye heshima chini ya mwavuli wa utawala wa Kiislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu