Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  20 Jumada II 1443 Na: Afg. 1443 H / 10
M.  Jumapili, 23 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Joe Biden Lazima Aangalie Mifarakano ya Ndani ya Marekani badala ya Kuzungumza Upuuzi kuhusu Afghanistan!
(Imetafsiriwa)

Katika mkutano na waandishi wa habari, Rais wa Amerika Joe Biden alisema kuwa Afghanistan haiwezi kuunganishwa chini ya serikali moja, na ndiyo maana ardhi hii imegeuka kuwa makaburi ya himaya.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan inalaani matamshi ya hivi karibuni ya rais wa Marekani kwa maneno makali iwezekanavyo, na kuyataja kuwa ni aina ya matamshi ya kipuuzi yenye lengo la kuripoti kushindwa na kutoroka kwa fedheha kwa Marekani kutoka Afghanistan. Matamshi ya Biden yanadhihirisha wazi uadui mkubwa wa watawala wa Marekani dhidi ya watu wa Afghanistan.

Badala ya kutoa matamshi hayo yanayokinzana na ya kipuuzi juu ya Afghanistan, Rais wa Marekani anapaswa kuzingatia kushughulikia migawanyiko ya kisiasa, rangi na kifikra ndani ya Marekani. Kwa kuwa pengo kati ya tabaka la matajiri na maskini limeongezeka sana nchini Marekani. Ubaguzi wa rangi na utawala kamili wa tabaka la Wazungu Weupe juu ya Waamerika Wenyeji Weusi ni janga dhahiri ambalo ni sawa na moto kwenye majivu ambayo moto wake utageuka kuwa maafa makubwa hivi karibuni, na kuipelekea Amerika kutoka kwenye majivu na kuingia motoni. Mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi, na afisa wa polisi mweupe mnamo 2020 yalionyesha wazi mgawanyiko mkubwa wa kijamii katika jamii ya Amerika. Kinyume chake, baadhi ya majimbo ya Marekani, ikiwa ni pamoja na California, yanatafuta kujitenga na uhuru. Wamarekani wanaonekana kuwa wanyonge kabisa kwani hakuna mfumo au thamani kati yao ya kuwaleta pamoja. Kwa sababu hii, wanasiasa na wasomi wa Marekani hujaribu kila wawezalo kuwatambulisha maadui wa bandia kwa watu wao kwa kuwakuza kwa njia yenye kupotoa rai jumla kutoka kwa matatizo na sintofahamu za ndani ya Amerika.

Japokuwa, bila shaka mtu hawezi kukataa kwamba hakuna matatizo ya kikabila nchini Afghanistan, lakini historia na tafiti zinaonyesha kwamba sehemu kubwa ya migogoro hii inatokana na umbali mkubwa wa watu kwa maadili muhimu ya Uislamu, kuwepo kwa fikra potovu ya Utaifa kama pamoja na utabikishaji wa sera za kikoloni za Uingereza na Marekani. Kama ilivyokuwa katika karne ya 19, Uingereza ilitia saini mikataba mbalimbali pamoja na kuainisha Afghanistan katika jiografia iliyokumbwa na mzozo, huku Marekani ikifuata sera hiyo hiyo yenye mwelekeo wa kikabila kutoka kwa Kongamano la Bonn hadi siku za mwisho za kutoroka kwake.

Kwa hakika, Umma wa Kiislamu una imani moja, Kibla kimoja, Mtume (saw) mmoja na Kitabu kimoja; na kwa sababu hii, Mujahidina kutoka katika ulimwengu wote wa Kiislamu walishiriki katika Jihad ya Afghanistan - na ilitokana na umoja huo uliopelekea kushindwa kwa Marekani. Bila shaka, Waislamu wa Afghanistan wanaweza pia kuwakilisha umoja wa Jihad kupitia mchakato wa ujenzi wa dola. Hili litawezekana tu iwapo serikali hiyo itaegemezwa kwenye imani ya Kiislamu na watawala wake kuchukua mamlaka kupitia njia ya bay'ah. Kama vile historia ya dhahabu ya Uislamu inavyotufahamisha kuhusu zama za ajabu za Waislamu ambazo kwazo Khilafah ilikuwa umeunganisha makabila, rangi na ardhi tofauti chini ya mwavuli mmoja mkubwa. Kwa hiyo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah inakaribia kuibuka tena kwa njia ya Utume na kujibu midomo iliyopotoka ya wakoloni wanaozidi kuporomoka, In Sha Allah!

 [فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيبًا]

“Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Israa: 51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

أفغانستان#         #Afghanistan         #Afganistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu