Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  8 Shawwal 1445 Na: Afg. 1445 H / 14
M.  Jumatano, 17 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuwekwa Kizuizini kwa Msemaji na Wanachama Kadhaa wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan na Watawala wa Sasa kwa Uhalifu wao wa Kulingania Khilafah!

(Imetafsiriwa)

Ustadh Saifullah Mustanir, Mkuu wa Afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan, na wanachama kadhaa wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan wamewekwa kizuizini na vikosi vya usalama tangu mwisho wa mwezi wa Shaaban 1445 H. Lile linaloitwa dhambi lao pekee au uhalifu wao imekuwa kulingania na kujitahidi kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Uzuizi huu ulifanywa baada ya mkutano uliopewa kichwa cha “Khilafah; Urithi wa Kisiasa wa Utume” uliofanyika kuashiria mwaka wa 103 wa Kuanguka kwa Khilafah - mkutano ambao pia ulifanyika katika nchi zingine za Kiislamu na mikoa kadhaa ya Afghanistan.

Ustadh Saifullah Mustanir ni mmoja wa wana waheshimika na mashuhuri wa Ummah huu ambaye alikuwa akijitahidi kwa ajili ya mwamko wa Khilafah. Wakati wa uvamizi wa Mareka, Ustadh Saifullah Mustanir alikuwa mmoja wa mabingwa hodari katika eneo la fikra na siasa, ambaye kwa bidii aliendelea kufichua uhalifu mbaya wa uvamizi huo na rekodi nyeusi za Jamhuri kwa kuandika mamia ya taarifa kwa vyombo vya habari, makala, uchambuzi wa kisiasa na kuhudhuria mahojiano ya runinga. Kwa bahati mbaya, chini ya serikali tawala, Ustadh Saifullah Mustanir na wabebaji wengine wa Da’wah wa Hizb wamefungwa kwa dhambi la kujaribu kuregesha izza ya Ummah na kuukumbusha Ummah juu ya kuanguka kwa Khilafah, ambalo ni tukio la uchungu katika historia ya Waislamu. Je! Ni dhambi na/au uhalifu kulingania kuregeshwa kwa Khilafah na kujitahidi kwa ajili ya umoja wa kifikra, kisiasa na kijiografia wa Waislamu?! Ikiwa jibu ni ndio, kwa msingi wa hukmu gani ya sharia? Kwa kweli, dola zinazojiita za Kiislamu zenye zinapaswa kukumbuka siku hii na kuelezea umuhimu wa Khilafah kwa Ummah - sio tu kwamba hili halijafanywa, lakini pia wale ambao wamefanya kitendo hiki kama faradhi ya Kiisilamu wametiwa makosani!

[أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ]

Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? Mna nini? Mnahukumu vipi?” [Al-Qalam: 35-6].

Tunatamani lau wale waliotoa ilani hii ya kukamatwa wangesikiliza ujumbe wa wabebaji Da’wah wa Hizb ut Tahrir bila upendeleo wa aina yoyote kwa kutafakari sana juu yake kwa muda kidogo; Katika hali hiyo, bila shaka wangewaunga mkono katika kubeba juhudi hii adhimu na ujumbe mzuri badala ya kuwakamata wabebaji Da’wah. Kwa kweli, mapambano yanayofanywa na Hizb ut Tahrir ni jukumu lililoagizwa na Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na hii ni faradhi kwa kila Muislamu kufanya bidii yao ya juu kabisa kusimamisha Khilafah; kuhakikisha utekelezaji kamili na ufikishaji wa Uislamu; kuondoa mipaka bandia, na kuleta umoja wa Ummah.

Hizb ut Tahrir ni changamfu kifikra na kisiasa katika nchi zaidi ya 40 ulimwenguni. Leo, Waislamu na Mujahidina wa Afghanistan, haswa Ulamaa, wazee wa makabila, viongozi wa kijihadi na kisiasa, na vijana, wanaielewa Da’wah ya Hizb ut Tahrir na wanajua vyema fikra zake, kusudi lake na njia yake. Wale ambao wamezidiriki njia za Hizb ut Tahrir bila ubaguzi wanaelewa wazi kuwa ujumbe na amali za Hizb ut Tahrir sio tishio kwa Waislamu wa Afghanistan; Badala yake, ni ujumbe wa wema (khair) ambao hauna mizizi tu katika Uislamu lakini pia ni chanzo cha ushindi na mwamko.

Serikali inayotawala lazima ihifadhi maadili ya Uislamu na kuwepesisha juhudi za wabebaji Da’wah katika jamii. Kinyume chake, pamoja na kukamatwa huko, inathibitisha kwamba serikali tawala ni kikwazo kwa Da’wah ya wema (Khair). Hivyo basi, tunawaomba ndugu zetu Mujahidina wawaachilie huru wabebaji Da’wah wa Hizb ut Tahrir haraka iwezekanavyo kwa sababu hakuna sababu ya Kiislamu inayohalalisha kukamatwa kwao.

[وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]

Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa!” [Al-Buruj: 8]

Ni muhimu kukumbuka kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) kukamatwa kama huko hakuwezi kuzuia hatua za pamoja na amali za vyombo vya habari za Hizb ut Tahrir kwa njia yoyote na kwa mbinu yoyote - lakini kwa kila siku inayopita, nguvu na nguvu ya Da’wah huongezeka kwa neema ya Mwenyezi Mungu (swt) al-Qawwi na al-'Aziz, na Alhamdulillah. Maelfu ya Waislamu wa Afghanistan na wabebaji Da’wah hutoa Dawah hii yenye fadhila ndani na nje ya Afghanistan. Majaribio kama hayo ya kikatili tayari yameshafanywa na watawala wa Kiarabu wakandamizaji, watawala wa Asia ya Kati na hata na Jamhuri iliyoporomoka, lakini vitimbi vyao viovu (Makr) wamewarudia wao wenyewe. Kwa hivyo, msizuie Da’wah ya Hizb ut Tahrir, ili msiwe maregeleo ya

«صدوا عن سبیل الله» na kubeba mzigo mzito kesho Akhera na muwe miongoni mwa wale wanaozuia Da’wah ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume – Khilafah ambayo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Wake (saw). Tunatambua kuwa serikali tawala nchini Afghanistan ina uwezo wa kugeuka kuwa Khilafah ikilinganishwa na serikali zingine zozote ulimwenguni, kwa hivyo tunatarajia kwamba msingi wa Khilafah kwa njia ya Utume utawekwa mikononi mwa Mujahidina wa Afghanistan kwa kutupatia Nusrah ya Kisharia.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao.” [An-Nur: 55]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu