Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  1 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: Afg. 1445 H / 22
M.  Alhamisi, 09 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ni kwa kupitia Khilafah kwa njia ya Utume Pekee, na Umoja Halisi wa Ummah, ndipo Makabiliano Madhubuti kwa Jinai Dhahiri za Magharibi na Kutetea Damu ya Waislamu Yatapatikana

(Imetafsiriwa)

Gazeti la ‘The Guardian’ liliripoti kuwa uchunguzi wa uhalifu wa kivita wa jeshi la Uingereza nchini Afghanistan unaweza kucheleweshwa hadi 2025. Jeshi la Wanahewa la Uingereza limetuhumiwa kuwaua takriban Waislamu 80 wa Afghanistan katika jimbo la Helmand. Inaripotiwa kwamba wanajeshi hao waliwaua watu hawa wakiwa wamelala au baada ya kukamatwa kati ya 2010 na 2013. Wakili mmoja wa kesi hiyo alisema kwamba Kikosi Maalumu cha Uingereza huko Helmand kilikuwa na sera ya kuwamaliza 'wanaume wote wenye umri wa kupigana.' Wakati huo huo, mnamo 2020, uchunguzi wa jeshi la Australia pia ulithibitisha kwamba vikosi vyao viliwapiga risasi raia 39, wakiwemo watoto na wafungwa nchini Afghanistan kati ya 2005 na 2016.

Matukio hayo yaliyotajwa ni mfano mdogo tu wa maelfu ya uhalifu uliofanywa na vikosi vya kigeni vinavyokalia kwa mabavu nchini Afghanistan, ambapo ni sehemu ndogo sana ambayo imeripotiwa. Jinai za kivita za nchi za Magharibi dhidi ya Waislamu haziko nchini Afghanistan pekee bali zimekuwa zikiendelea kwa miaka 103 tangu kuanguka kwa Dola ya Khilafah, zikimwaga damu za Waislamu bila huruma kutoka Palestina hadi Iraq na kutoka Syria hadi Afrika, bila ya kuwepo jeshi wala mtawala wa Waislamu kuilinda damu hii adhimu. Imekuwa ni aina ya burudani kwa wanajeshi wa Kimagharibi. Baadhi ya wanajeshi wa Marekani na NATO wamekiri kwamba wakati wa misheni zao nchini Afghanistan, waliwafyatulia risasi raia kwa kamari na burudani.

Mahakama zilizoanzishwa nchi za Magharibi kuchunguza uhalifu wa kivita hazina uwezo wa kutoa haki, kwani washitakiwa wengi licha ya kutenda makosa mbalimbali ya kivita, wanaachiliwa huru katika mahakama za kijeshi wakiwa na tabasamu kubwa. Mnamo mwaka wa 2019, Trump aliwasamehe wahalifu watatu wa kivita waliohusika katika mauaji ya Waislamu wasio na hatia nchini Afghanistan na Syria, ingawa mahakama zao kuu zilikuwa zimetoa hukumu za kifungo cha muda mrefu.

Hapana shaka kwamba historia Magharibi imejaa jinai dhidi ya binadamu, na popote pale ambapo hatua zao za kutisha zimeanguka, zimezua hofu na uhalifu. Wakaliaji kimabavu wa Magharibi hawajajitolea kwa maadili yoyote ya kibinadamu ya kiakhlaqi. Jinai za Kimagharibi hazikomei kwenye jinai za kivita tu bali zimeongezeka tangu kuanguka kwa Khilafah, kwani fikra potovu za demokrasia na utamaduni wa umwagaji damu wa urasilimali zimechukua nafasi ya utaratibu wa kimataifa, na kuwaweka wanadamu wote, hususan Umma wa Kiislamu, chini ya uvamizi, ukoloni, dhulma, na uhalifu, na hata nchi kavu, bahari, ndege, na wanyama bila hawajasazwa na ukatili wao.

Hakika, kila Muislamu aliyeuawa si tu ni tarakimu bali ni binadamu, na kila tone la damu yao lina thamani zaidi kuliko Ka’aba, na inafaa kwamba thaqafa na mfumo wa Kimagharibi zipinduliwe kwa tone la damu ya Waislamu. Hata hivyo, inasikitisha kwamba licha ya nchi za Magharibi kutekeleza jinai za kivita dhidi ya Mujahidina na Waislamu wa Afghanistan katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, utawala wa sasa unatafuta maingiliano ya karibu na wahalifu hao, huku ukifanya mikutano ya kisiasa na kiusalama na wanadiplomasia na maafisa wa usalama wa Marekani na Uingereza. Katika mikutano hii, maombi ya uhalali wa kisiasa na misaada ya kiuchumi hufanywa. Hivyo basi, tunawakumbusha kwa ikhlasi ndugu zetu Mujahidina kwamba msimamo wenu mkali wa kijeshi katika uwanja wa Jihad imepelekea kushindwa kwa adui, ni lazima kuchukua msimamo mkali wa Kiislamu katika nyanja za siasa na diplomasia ili adui huyu mjanja na mhalifu asipate fursa ya kujipenyeza katika ardhi zetu. Sera ya Kiislamu inaamuru kukomesha aina yoyote ya miamala ya kisiasa na kiuchumi na wahalifu hao na kujitahidi kupata umoja wa kweli wa Ummah, kama jibu tosha kwa jinai za nchi za Magharibi zenye kiburi, ulinzi kwa maadili ya Kiislamu, na damu ya Waislamu bila ya umoja wa kifikra, kisiasa, kijeshi, na kijografia wa Ummah na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume haiwezekani.

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ فَإِنْ أَمَرَ بِتَقْوَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ وَعَدَلَ كَانَ لَهُ بِذَلِكَ أَجْرٌ وَإِنْ يَأْمُرْ بِغَيْرِهِ كَانَ عَلَيْهِ مِنْهُ»

“Hakika, Imam (Khalifa wa Waislamu) ni ngao kwao. Hupigana nyuma yake na hujihami kwaye (kutokana na madhalimu na wavamizi). Basi akiamrisha uchaMungu Mtukufu na akafanya uadilifu kwa hilo atapata ujira (mwema); na akiamrisha yasiyokuwa hayo yatageukia juu yake.” (Sahih Muslim)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu