Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 9 Dhu al-Hijjah 1445 | Na: Afg. 1445 H / 29 |
M. Jumamosi, 15 Juni 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan Yawapongeza Waislamu Wote kwa Mnasaba wa Idd al-Adha na Inasisitiza Umoja wa Sherehe za Kidini kama Kanuni ya Sharia!
(Imetafsiriwa)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inatoa pongezi na salamu za dhati kwa Waislamu wote duniani kote kwa mnasaba wa Idd ul-Adha. Vile vile tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) azikubali swala, ibada, mapambano na mihanga ya Waislamu wote kwa Rehema zake na aikubalie Hijja yao.
Idd ni ishara ya furaha, na umoja kati ya Waislamu duniani kote. La kusikitisha, mwaka huu, Idd ul-Adha inaadhimishwa kwa siku tofauti katika ardhi mbalimbali za Kiislamu. Serikali inayotawala nchini Afghanistan umeitangaza Jumapili kuwa siku ya Arafah na Jumatatu kuwa siku ya kwanza ya Idd, huku katika nchi nyingine nyingi za Kiislamu, kwa kuzingatia ushahidi wa Waislamu, Jumamosi inaadhimishwa kuwa Siku ya Arafa na Jumapili kuwa siku ya kwanza ya Idd al-Adha.
Hitilafu katika sherehe za kidini ni Fitna kubwa ambayo imewaacha Waislamu wa Afghanistan katika hali ya kuchanganyikiwa kuhusiana na wajibu wao wa kidini. Wakati maafisa wengi wa serikali inayotawala wapo kwenye sherehe za Hijja na wao wenyewe wanafahamu kusimama kwa mahujaji kwenye tambarare za Arafat, kwa kutambua ukweli wa Siku ya Arafah, swali linazuka: je, viongozi hawa wanasherehekea Arafah na Idd kwa fatwa zao wenyewe au kwa mujibu wa sherehe za Hajj? Kwa bahati mbaya, serikali inayotawala, kwa kuchelewesha tamko la Idd kwa siku moja nyingine, hufanya kinyume na ushuhuda wa Waislamu wengine. Kitendo hiki kinachukuliwa kama kutojali, kuzusha mifarakano miongoni mwa Umma wa Kiislamu. Walifanya kitendo kile kile cha kutokuwa sahihi na mfarakano wakati wa Ramadhan na Idd al-Fitr mwaka huu, ambacho kilirekebishwa baadaye.
Sherehe za kidini ni mambo nyeti sana na hayapaswi kuwa mada ya ushindani wa dola za kitaifa. Kanuni ya Sharia pia inasisitiza umoja wa sherehe za kidini kati ya Waislamu. Kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyoweka wazi kwamba muandamo wa mwezi kwa Muislamu yeyote mahali popote duniani, kihalali, kunawajibisha Waislamu katika nchi nyingine kuoanisha ibada zao za kidini ipasavyo. Katika suala hili, hakuna Muislamu aliye na ubora juu ya Muislamu mwengine, na hakuna ardhi iliyo na ubora juu ya ardhi nyingine. Hasa katika zama za sasa, wakati habari za ushuhuda mmoja zinawafikia watu wote ulimwenguni kote kwa sekunde chache. Ikiwa kuna baadhi ya fatwa za zamani katika suala hili, kwa hakika zilikuwa halali kutokana na hali halisi ya zama hizo na umbali wa maeneo kutoka kwa kila mmoja kwa wakati huo; lakini katika zama za sasa, kutokana na mabadiliko makubwa ya uhalisia, fatwa hizo zimepoteza uhalali wake na haziwezi kupingwa. Kanuni ya Sharia katika fiqhi ya Hanafi pia inazingatia ushuhuda wa Waislamu wawili kwa muandamo wa mwezi unaotosha kuanza au kuhitimisha sherehe za kidini, jambo ambalo linaashiria msisitizo wa madhehebu ya kifiqhi juu ya umoja na kuepuka mifarakano.
Bila shaka si chochote ila ni rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwamba amewafanya Waislamu kuwa Ummah mmoja kwa kuwaamrisha wawe na Taqwim (kalenda) ya pamoja kwa ajili ya kutekeleza ibada za kidini kama vile Hija, Saumu, Jihad, Idd na hukmu nyinginezo za Sharia, ili kutofautishwa na mataifa mengine ya ulimwengu. Ni lazima tutambue kwamba hukmu za Sharia zimewazungumzia Waislamu wote, sio taifa au ardhi maalum.
Kwa kweli, kilichokwamisha utekelezaji wa hukmu za Sharia na umoja wa sherehe za kidini miongoni mwa Ummah ni kuwepo kwa mipaka ya dola za kitaifa, kutoaminiana baina ya Waislamu, na kugombania madaraka. Mambo haya sio tu kwamba yamegawanya furaha za Ummah bali pia yametenganisha huzuni zao wenyewe kwa wenyewe. Leo hii, sera za kitaifa zimeutenga Ummah kiasi kwamba hata hawajui ni jinai gani zinazofanywa nchini Sudan, ambaye anauawa huko Kashmir; na vile vile, sababu ya Gaza inachukuliwa kuwa ni suala la ndani kwa Wapalestina. Waislamu wengi, kutokana na sera hizo zisizo za Sharia, hata wanafikiri kwamba Turkestan Mashariki ni sehemu halali ya ardhi ya China.
Ndio, Idd al-Adha inatukumbusha juu ya Nabii Ibrahim (amani iwe juu yake) - ishara ya muhanga, kutegemea (Tawakul), na mfano wa kuigwa wa Al-wala’ na Al-bara’. Kwa hiyo, ikiwa Gaza iko mbali na sisi, Tajikistan, ambayo iko karibu na Afghanistan, inatoa amri za kupinga hijab na dada zetu Waislamu wanapiga kelele kuomba msaada, lakini watawala wananyamaza kimya kutokana na manufaa ya kisiasa.
Kwa hiyo, ni faradhi kwa Waislamu kujitahidi na kupigania umoja wa kifikra, kisiasa, na kijiografia chini ya bendera ya dola moja ya Khilafah Rashida ya pili ili kulindwa kutokana na fitna, kuchanganyikiwa, na mgawanyiko huo kwa siku za furaha za Waislamu kutoka Indonesia hadi Morocco kuunganishwa. Hakika moja ya siku kuu za furaha kwa waumini ni siku ambayo Nusrah ya Mwenyezi Mungu (swt) itatolewa kwa kusimamishwa Khilafah Rashida ya pili.
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُالرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu..” [Ar-Rum: 4-5]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |