Jumatatu, 27 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  22 Rabi' I 1446 Na: Afg. 1446 H / 09
M.  Jumatano, 25 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sera ya Kinafiki ya Iran: Kuwasaliti Mashia ili Kuitumikia Marekani

(Imetafsiriwa)

Katika siku chache zilizopita, zaidi ya Waislamu 500 nchini Lebanon wameuawa shahidi kutokana na mashambulizi ya umbile la Kiyahudi, huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa. Mashambulizi haya yamechukua aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mlipuko wa vifaa vya mawasiliano kama vile pager na mifumo ya walkie talkie, pamoja na mashambulizi ya angani yanayolenga wanawake, wanaume na watoto. Matukio haya yamechochea wimbi la hisia miongoni mwa Waislamu nchini Afghanistan vilevile.

Kwa bahati mbaya, katika zama za sasa, hakuna Khalifa katika ardhi za Kiislamu wa kutenda kama ngao dhidi ya ukandamizaji wa Wazayuni. Kama matokeo, majibu ya mashambulizi haya, kama matukio mengine kama hayo, yamefungwa tu kwa shutma za kimaneno. Katika kukemea matukio haya, hakuna tofauti inayoonekana baina ya watawala wa nchi za Ulaya na wale wa ardhi za Kiislamu.

Hata hivyo, watawala kama wale wa utawala wa Iran na makundi tanzu wanashughulika na kupotosha rai jumla na kukaa kimya mbele ya ukatili huo. Wakati jinai za kikatili na mauaji ya halaiki mjini Gaza hazijasababisha majibu kutoka kwa watawala wa Iran, ni dhahiri kwamba jinai za Lebanon hazitawasukuma pia. Kwa miaka mingi, utawala wa Iran umekuwa ukichana koo lake kwa kauli mbiu za kuwaunga mkono Waislamu, hasa Mashia, lakini wakati wa kuchukua hatua madhubuti unapowadia, mtu anaweza kuona tu midomo yao ikiwa imezibwa na usaliti wao ukiwa wazi. Kwa uhalisia, utawala wa Iran si wa Kiislamu wala hauhisi huruma kwa Mashia. Iran ni dola ya kitaifa ambayo ipo katika eneo hili kuhudumia maslahi ya Marekani, kwa kutumia kauli mbiu kama mtetezi wa Mashia kama kauli mbiu ya kuendeleza sera zake yenyewe. Sera hizi huhadaa idadi ya watu wenye fikra duni ambao hawana ufahamu sahihi wa hali ya kisiasa.

Kwa hakika, dola yoyote ya kitaifa inayonyanyua bendera ya Uislamu inakosa uwezo wa kufanya jambo kwa ajili ya Waislamu. Serikali hizi kwa miaka mingi zimejihusisha na kupanda mbegu ya mgawanyiko kati ya Umma wa Kiislamu chini ya majina ya Sunni na Shia - kwani leo hakuna serikali ya Kisunni iliyochukua hatua kwa watu wa Gaza, na hakuna serikali ya Kishia iliyochukua hatua kwa watu wa Lebanon. Hii ni kwa sababu matendo haya (kuwalinda Waislamu) yangegongana na maslahi yao ya kitaifa na matakwa ya Marekani. Wakati Marekani ilipotaka kuyakandamiza mapinduzi ya Syria, watawala hao hao wasaliti wa eneo hilo walijitokeza na kuyafutilia mbali mapinduzi hayo. Iran ilishirikiana na Wamarekani katika vita vya Afghanistan na Iraq na hata kwa fahari inakiri ushirikiano huu. Kadhalika, wakati maslahi ya Marekani yalipohitaji, Iran ilisaidia makundi fulani vibaraka chini ya bendera ya Ushia na utaifa; lakini leo hii, huku sera za Marekani zikibadilika, Iran vile vile imerekebisha sera zake ipasavyo. Uhalisia huu unaonyesha kwamba serikali hizi zinafanya kazi kwa kuzingatia tu maslahi yao ya kitaifa na amri za dola za kigeni, hususan Marekani, si kwa ajili ya maslahi ya Uislamu na Waislamu, si Shia wala Sunni.

Kwa hivyo, hakuna mtu au kikundi chochote kinachopaswa kuweka matumaini yao katika uungaji mkono wa watawala hao, haswa watawala wa Iran. Watawala hao wako tayari kusaliti kikundi, kabila, au dini ili waendelee kuishi. Kinyume chake, Hizb ut Tahrir ina uongozi usiowadanganya watu wake, haujachafuliwa na umadhehebu, na inawataka Waislamu wote kusimamisha Khilafah ya Rashidah ya Pili. Ni kwa kusimamishwa Khilafah kwa njia ya Utume tu ndipo kunaweza kuwa na utawala wa kweli ambao utazingatia ulinzi wa Waislamu, Sunni na Shia, kama sehemu ya misheni yake msingi na wajibu wa Kiislamu. Kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam (Khalifah) ni ngao, ambaye kwa amri yake Waislamu hupigana, na kwa mkakati wake Waislamu hulindwa kutokana na madhara ya adui.” (Abu Dawood)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu