Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  9 Muharram 1444 Na: 1444 H / 002
M.  Jumapili, 07 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu: Ukanda wa Gaza Hashem Unapigwa Mabomu

Na Majeshi ya Kiislamu Yamewekwa katika Kambi zao Wakisahau kuwa Wajibu wao ni Kuinusuru na Kuwahami Watu wake
(Imetafsiriwa)

Mayahudi wamekuwa wakiishambulia kwa mabomu Gaza tangu Ijumaa, 05/08/2022, mbele ya macho ya ulimwengu. Wanawaua watu wake na kuharibu majengo yake. Na jeshi la Misri al-Kinana limelala fofofo ndani ya kambi zake, huku jana wakiwa katika kilele cha shughuli zao, wakianzisha operesheni ya kijeshi baada ya operesheni katika eneo la Sinai, ambalo liko kwenye mpaka wa Gaza!

Na kama vile Qur’an Tukufu ilivyowasifia, na matukio yanayoshuhudiwa dhidi yao, Mayahudi ni watu waoga, na lau kama hawangeamini kwamba Rais wa Misri Al-Sisi, anayeitwa “Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi”. asingetoa amri zake za kuhama jeshi la Kinana, wasingethubutu kuikaribia Gaza. Lakini kama katika mishipa yake damu ya ulinzi kwa Waislamu inazunguka, kusingekuwepo na Yahudi ndani ya Ardhi Iliyobarikiwa yote, hata hivyo anashughulika na kutumia mali ya Misri katika kujenga makasri yake katika mji mkuu mpya wa utawala, kusafirisha majeneza ya Mafirauni, na kuwakandamiza watu wanapomhisabu.

Kwa upande wa jeshi la Uturuki la Erdogan, ambalo lilizindua Operesheni Tawi la Mzaituni huko Afrin, lilisahau zaituni za Gaza, lakini hata kusahau zaituni zote za Ardhi Iliyobarikiwa na lilikuwa na linashughulika na kutumikia maslahi ya Amerika nchini Syria, Libya na nyenginezo.

Ama Jeshi la Jazirat al-Islam (Bara Arabu), lilisahau kwamba umbali kati ya Kambi ya Anga ya Tabuk na Gaza ni robo ya umbali kati ya Riyadh na Yemen. Labda uharibifu wa Yemen, kama Amerika ilivyoomba, ni wa juu zaidi (kwa umuhimu) kuliko uharibifu wa Mayahudi! Ama kuhusu mfalme mtarajiwa wa familia ya tawala ya Al Saud, aliusaliti Uislamu alipofungua nchi kwa sherehe chafu kimaadili, na hata familia yake haikuepukika na usaliti wake alipochukua pesa zao na kuipa Amerika, na leo anajaribu kuandaa mazingira ya kutangaza uhalalishaji wa mahusiano na Mayahudi.

Enyi Waislamu: Jambo hili liko wazi na halihitaji maelezo mengi. Kuzuiwa kwa Mayahudi na kukombolewa kwa Ardhi Iliyobarikiwa kunahitaji nusra ya majeshi ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ قَاتِلُواْ الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُواْ فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ]

Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mungu. [At-Tawba: 123].

Ama wale wanaopinga, wanaozuia, au wanaotelekeza wito wa majeshi wa kupigana na Mayahudi na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa, basi na wajihadhari na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt), kwani hali yao ni hali ya wale ambao Mwenyezi Mungu aliowaeleza (katika ayah):

[وَلَوْ يَشَاء اللَّهُ لانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ]

Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao. [Muhammad: 4].

Hivyo basin a waachane na uzushi huu na wajihadhari na ghadhabu za Mwenyezi Mungu.

Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi: Mwenyezi Mungu (swt) huleta matukio kama hayo kama fursa kwa wale walio katika nafasi yenu kuingilia kati na kuinusuru Dini yao na kuwaokoa ndugu zao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia [Al-Anfal: 72].

 

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu