Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  28 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 016
M.  Jumatatu, 24 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Taarifa za Josep Borrell Zinafichua Udhaifu wa Muungano wa Ulaya
(Imetafsiriwa)

Mwakilishi Mkuu wa Muungano wa Ulaya kwa Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama, Josep Borrell, alitoa hotuba mnamo Alhamisi, Oktoba 26, 2022, ambayo ilijumuisha taarifa za ubaguzi wa rangi kwamba "Ulaya ni bustani na ulimwengu uliosalia ni msitu." Aliendelea naye na kuelezea kile ambacho nchi za Ulaya zinapaswa kufanya. Alisema: “Kichaka kinaweza kuvamia bustani hiyo, watunza bustani wanapaswa kuitunza, lakini hawatailinda bustani hiyo kwa kujenga uzio, bustani ndogo nzuri iliyozungushiwa kuta ndefu ili kuzuia kichaka haipaswi kuwa suluhisho. Wasimamizi wa bustani lazima waingie msituni, Wazungu wanatakiwa wajihusishe zaidi na ulimwengu uliosalia, la sivyo ulimwengu uliosalia utaivamia Ulaya." Kisha akaomba radhi kwa kauli hizo baada ya kupokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa nchi, ikiwemo UAE, na alidai kuwa alieleweka makosa na kwamba maneno yake yametolewa nje ya muktadha miongoni mwa vyombo vya habari.

Taarifa hizi zinafichua shakhsiya halisi ya Ulaya; mafanikio barani Ulaya na ukoloni kwa ulimwengu uliosalia. Ama kauli mbiu yao ya amani na utulivu, lengo lake lilikuwa kusimamisha vita vya dunia vilivyotokea baina ya nchi za Ulaya katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Ama ulimwengu uliosalia ina mizinga na makombora, ufisadi na uporaji wa mali!

Tangu kuanzishwa kwake, Muungano wa Ulaya umekumbwa na majanga ya mizozo na migawanyiko miongoni mwa watu wake, wa kwanza wake ni kwamba ni muungano na sio kitengo kimoja, jambo linalo ulazimisha kushughulikia kila wakati ukaidi wa vitambulisho vya watu. Kwa hiyo, hakuna nchi iliyoweza kuongoza uongozi wa muungano huu katika historia yake. Badala yake, wakati wowote nchi inapojaribu kunyakua uongozi wake, mzozo hutokea ambao hufichua udhaifu wake, na kuondoka kwa Uingereza (Brexit) kutoka muungano huo mwaka wa 2020 ni mojawapo tu ya madhihirisho ya udhaifu wake. Na sasa hofu na uoga unawajia watu wa bara la Ulaya, huku wakikabiliwa, kama wengine, na kupanda kwa bei ya juu ya mafuta na gesi baada ya kufungwa kwa mabomba ya Nord Stream 1 na 2, na kusitishwa kwa mtiririko wa gesi kioevu kutoka Urusi, ambayo ilisababisha kufungwa kwa tanuri za mkate na tahadhari kali za kiuchumi katika ngazi ya watu binafsi katika maandalizi ya kile chengine ambacho msimu wa baridi kitaleta kutokana na gharama kubwa za upashaji joto.

Ndiyo, hali hii inaogofya kwa watu ambao mababu zao waliwalemeza mzigo wa vita viwili vya dunia, huku vizazi vyao vya sasa vikiacha kupigana na kufikiria juu yake na vimebadilisha vita kwa kufurahia maisha na starehe zake. Pia inaogofya kwa watu wanaohisi kuwa umaskini unabisha hodi kwa pamoja mlangoni kwao.

Kama ilivyodhihirika wakati wa kuibuka kwa janga la virusi vya Korona mnamo 2020, kwamba Ulaya "bustani" imekuwa tupu kwenye viti vyake vya enzi, na huku bustani ikigeuka kuwa maghala, na kila ghala linaendeshwa na serikali ya kitaifa ya nchi za Muungano na kuchukua tahadhari za kiafya kama kisingizio cha kufunga mipaka yake na majirani zake, ambayo ilizuia misaada ya matibabu kutembea bila vizuizi, kwa hivyo uhalisia wa kile kinachoitwa umoja wa watu wa Ulaya umejitokeza.

Unafiki wa Kimagharibi uliojitokeza katika mitazamo ya Ulaya hivi karibuni hauna kifani, kwani unadhihirisha ukweli wa kanuni ya kibepari ambayo nchi hizi inashikilia, na ambayo kwayo misimamo inabadilishwa kwa mabadiliko ya maslahi na manufaa. Kwa vile kanuni hii haijui thamani zaidi ya thamani ya kimada, haizingatii maadili ya kibinadamu, ya kiakhlaqi au ya kiroho. Ushahidi wa hili ni faili za kiuchumi zinazozinasibisha nchi hizi na Iran hata kabla ya janga la virusi vya Korona. Lugha ya pesa au urahisi wa kuzifikia rasilimali na malighafi ndio lugha na dini ya nchi za kibepari, kama inavyoonyeshwa katika mikataba ya kuuza ndege za Ulaya kwa Iran.

Pia, katika miaka ya hivi karibuni, kumeibuka matatizo katika Muungano wa Ulaya yanayohusiana na utamaduni unaotokana na kanuni iliyotabanniwa na nchi za muungano huu, ambayo ilizifanya kuhitaji kuanzisha sera ya uoanishaji ya kipekee, inayowalenga Waislamu, haswa katika kujaribu kuwaingiza ndani ya mfumo wa maadili ya Kimagharibi badala ya kujaribu kuishi nao bila ya kuingilia faragha zao za kidini na kitabia.

Kwa hivyo, "bustani" haina tena maadili inayoyahifadhi na kuimba kuyahusu, kama vile kuhifadhi utamatuni anuwai na kuhudumia kila mtu. Badala yake, maadili haya hujitokeza katika mitaani mwetu na kutoweka ghafla inapobidi!

Enyi Waislamu:

Josep Borrell si afisa wa kawaida wa Ulaya, anahusika na sera za kigeni za Muungano wa Ulaya, ambapo inafanya taarifa zake kuelezea mtazamo wa maafisa wote wa Ulaya, bali mtazamo wa Magharibi kwa ulimwengu, hasa nchi za Kiislamu. Mtazamo wa kikoloni uko tayari kuchoma kile inachokiona kama "pori" mradi tu itumikie maslahi yake. Lazima muharakishe urejeshaji wa Khilafah, kwani majeshi ya Khilafah pekee ndiyo yaliyokuwa ngao ya ulinzi dhidi ya matamanio ya Ulaya na vita vyake mtawalia vya msalaba. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ)

“Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Aal-i Imran 3:118].

Ama Josep Borrell na warithi wake kutoka miongoni mwa watawala wa Ulaya, tunawahutubia kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(فَعَسَى رَبِّي أَن يُؤْتِيَنِ خَيْراً مِّن جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَاناً مِّنَ السَّمَاء فَتُصْبِحَ صَعِيداً زَلَقاً * أَوْ يُصْبِحَ مَاؤُهَا غَوْراً فَلَن تَسْتَطِيعَ لَهُ طَلَباً * وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَى مَا أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَى عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَداً * وَلَمْ تَكُن لَّهُ فِئَةٌ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِراً)

“Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, naye akapitisha kudra yake kutoka mbinguni kukilitea hicho chako, na kikageuka ardhi tupu inayo teleza. Au maji yake yakadidimia wala usiweze kuyagundua. Yakateketezwa matunda yake, akabaki akipindua pindua viganja vyake, kwa vile alivyo yagharimia, na miti imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingeli mshiriki Mola wangu Mlezi na yeyote! Wala hakuwa nacho kikundi cha kumsaidia badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujisaidia.” [Al-Kahf 18:40-43].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu