Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  13 Jumada I 1439 Na: 1439/009
M.  Jumanne, 30 Januari 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuziboev Sulton, Shahidi Mwengine Ndani ya Gereza la Katili Rahmon
- Ingawa Hatumtakasi Yeyote Mbele ya Allah

 (مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا)

“Miongoni mwa Waumini wapo wanaume waliosadikisha waliyo muahidi Allah. Baadhi yao yamekwisha kufa na baadhi yao wanasubiri, wala hawakubadilisha (ahadi) yao hata kidogo”  [33:23]

Hivi majuzi, mwanachama mwengine wa Hizb ut Tahrir – Kuziboev Sulton, Allah Amrehemu, alifariki ndani ya gereza la Rahmon, katili wa Tajikistan. Sulton alitumia miaka 18 kati ya umri wake wa miaka 47 ndani ya magereza yenye ulinzi mkali, kwa sababu ya kujitolea kwake katika kazi ya kulingania kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kwa ushirikiano na Hizb ut Tahrir. 

Kuziboev Sulton, Rahimahullah, alizaliwa mnamo 1971, baba wa watoto wanne, aliye hitimu na shahada mbili za juu za elimu (ndani ya gereza, mahabusu walimwita "kamusi-elezo inayotembea"). Alijiunga na Hizb na kuanza kueneza da'wah ya Kiislamu mnamo 1999, na kufikia mnamo Januari 15, 2000, aliwekwa kuzuizini na huduma maalumu za usalama za katili Rahmon na kupewa mateso makali, ambapo baadaye alitiwa katika gereza lenye ulinzi mkali katika korokoro nambari 3/7. Akiwa gerezani, Sulton alipata ugonjwa, uliogeuka baadaye kuwa maradhi mabaya ya mifupa miguuni mwake, alifanyiwa upasuaji na hatimaye kutembea kwa kuchechemea hadi kifo chake.  

Mnamo 2004, Sulton aliachiliwa huru baada ya kumalizika kwa kifungo chake na mara moja akaendelea na amali zake za kueneza da'wah ya Kiislamu nchini Tajikistan, ambapo aliwekwa tena kizuizini mnamo 2005. Wakati huu alihukumiwa kifungo cha muda mrefu, na kuwekwa katika mojawapo ya magereza mabaya zaidi nchini Tajikistan – korokoro nambari 3/3 (inayofahamika zaidi kama "eneo la matofali" kwa kazi zake za sulubu za utengezaji matofali). Gerezani humo mahabusu hufanyiwa upekuzi mara sita, na wanachama wote wa Hizb ut Tahrir huchukuliwa kama "wenye uwezo wa kutoroka". Katika korokoro hii, Sulton aliambukizwa maradhi ya pepo punda. Wakati wa kifungo cha Sulton alipo kuwemo ndani ya hospitali ya gereza hilo, mwajiriwa katika afisi ya Raisi Rahmon alimuahidi kumuacha huru mara moja lakini kwa sharti moja: Sulton aahidi kuachana na ulinganizi wa Kiislamu. Ndugu yetu alikataa kutoa ahadi hiyo, na kwa sababu hiyo alisalia korokoroni humo huku akiendelea kuugua maradhi hayo kwa miaka mingi ambapo, licha ya kila kitu na dhurufu alizokuwa nazo, aliendelea na ulinganizi huu na kamwe hakuuacha hata siku moja mpaka kufariki kwake (Rahimahullah).

Sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia ya ndugu yetu Sulton, Rahimahullah. Twamuomba Allah Subhanahu wa Ta'ala aipe familia yake msimamo, subra na ukakamavu. Twamuomba Allah Subhanahu wa Ta'ala amkubali Sulton kama Shahidi ingawa hatumtakasi yeyote mbele ya Allah. Twamuomba Allah Al-Aziz Al-Jabbar kumuangamiza katili Rahmon na serikali yake, na wasaidizi wake wote na washirika wake, twamuomba atuharakishie kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Kiislamu na kusimamishwa kwa Imam wa Umma huu – ngao ambayo nyuma yake munapigana na kujihami. Kwa yakini hili ni jepesi mno kwa Allah Subhanahu wa Ta'ala!

 Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu