Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  19 Dhu al-Hijjah 1438 Na: 1438/058
M.  Jumapili, 10 Septemba 2017

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amerika Inaisukuma Asia Kusini na Kusini Mashiriki Katika Ghasia, Huku Viongozi wa BRICS Wakiushutumu Uislamu!

Uislamu Ndio Msingi wa Utulivu Katika Maeneo Haya na Ulimwengu, Badala ya kuwa ni Sababu ya Wasiwasi!

 (Imetafsiriwa)

Kuhusiana na kile kinachotutia wasiwasi katika ufafanuzi na majibu ya Tangazo la Xiamen lililo fanywa  na nchi wanachama wa BRICS lililo tolewa kama nakala ya mwisho mnamo Jumatatu, 4 Septemba 2017, linalo taja kuwa nchi wanachama, "zinaelezea wasiwasi mkubwa juu ya mvutano unaoendelea kwa sasa na kadhia ya nyuklia ya muda mrefu katika eneo la Korea, na kusisitiza kuwa ni sharti utatuliwe tu kupitia njia za amani na mazungumzo ya moja kwa moja kwa pande zote husika. "kinachotutia wasiwasi katika jibu hili sio kutokana na Amerika kulisukuma eneo la Asia Kusini na Kusini Mashariki katika cheche za ghasia, ili kuliingia eneo hilo kama msaidizi wa serikali zinazo tishiwa na pia kama onyo dhidi ya "serikali jeuri", kwa kutumia uharibifu wa Korea Kaskazini kama kisingizio, huku ikijua kwamba majaribio ya kijeshi si chengine isipo kuwa ni kama "fataki" tu kufikia malengo ya kisiasa na ya vyombo vya habari, na wala sio kule kuingia kwa viongozi wa BRICS ndani ya mtego wa Amerika, kwa kurudia kama kasuku yaliyosemwa kuhusu uzito wa vitendo vya Korea Kaskazini…

Lakini, kinachotutia wasiwasi katika jibu hili ni yale yaliyo semwa ndani ya nakala ya mwisho, kuwa harakati nyingi za Kiislamu, za kihakika na za kindoto, zinatia wasiwasi nchi hizi na miongoni mwa harakati hizo ni Hizb ut Tahrir. Sisi katika Hizb ut Tahrir hatukubali kufanywa mada ya tuhuma na chama chochote, hususan kutoka nchi zilizo na uadui kwa Uislamu na fikra ya kurudisha utawala wa Kiislamu, kama vile Urusi, India na China. Kwa hivyo tunaulekeza ufafanuzi huu kwa Ummah wa Kiislamu ili ujue njama zinazo pangwa dhidi yake na dini yake tukufu, pamoja na watu waliopotoka wa BRICS, wanao tawaliwa na kikundi cha warasilimali wachache walafi, ambao wanalenga tu kuongeza utajiri wao na kudumisha utawala na athari yao, kupitia kuwanyanyasa na kuwadhulumu watu wao, huku wakiwapotosha, na kuwaweka mbali na ukombozi kupitia dini tukufu ya Uislamu. Kwa Ummah wa Kiislamu na kwa watu hao tunasema:  

Kwanza: Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa mfumo wake ukiwa ni Uislamu. Inabeba Uislamu kama mradi ulio staarabika, kama badala ya nidhamu zilizo tungwa na watu ambazo hazikuleta jengine isipo kuwa maangamivu kwa wanadamu. Chama hiki ni kundi miongoni mwa Ummah wa Kiislamu, linalofanya kazi kuukomboa kutokana na kutawaliwa na nchi za kimagharibi, ambazo zina ulafi juu ya utajiri wake. Chama hiki kinafanya kazi na Ummah kulingania Uislamu kama hadhara badala kwa watu, wanaotawaliwa na dhulma ya urasilimali. Chama hiki hufanya haya kwa kutekeleza amri ya Allah (swt), ilioufanya kuwa Ummah bora kwa wanadamu wote na bora kwa watu, hususan walio dhulumiwa na kunyanyaswa, kama vile watu wa mataifa ya BRICS.

Pili, "Ugaidi" ni jambo lililoundwa makhasusi na Amerika ambalo hutumiwa kote ulimwenguni, zikiwemo nchi za BRICS kama kisingizio cha kuushambulia Uislamu na kuwaandama wabebaji ulinganizi, ili kuzuia kurudi kwa Uislamu, dini ya rehma kwa wanadamu, na kurudi kwake katika utawala,kutakako fichua urongo na kufeli kwa nidhamu zilizo tungwa na wanadamu, na kumthibitishia kila mmoja kuwa Uislamu ndio mkombozi wa kweli wa watu kutokana na dhulma za urasilimali, pamoja na warasilimali na ulafi wao, miongoni mwao wakiwa ni watawala.

Tatu: Ulimwengu na eneo la Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia hayajawahi kuona usalama na amani kama yalivyo shuhudia wakati ambapo Uislamu ulipo tawala eneo hilo, lilishuhudia usalama na amani kwa muda mrefu. China, kwa karne kadhaa ili lazimika kuvunjilia mbali jeshi lake, kwa sababu haikuwa ikihisi tishio lolote la nje. Eneo hili halijawahi kupata mafanikio kama lilivyo kuwa wakati Uislamu ulipo kuwa ukitawalishwa katika eneo hili, wakati ambao India ndio iliyo kuwa kapu la chakula na ilikuwa ikiupa mikopo Ufalme wa Uingereza kuuokoa kutokana na ufisadi wa mabwana wake wa kiuchumi. Chini ya nidhamu za kibinadamu, ikiwemo urasilimali na ukomunisti wa kichina, eneo hili liligeuzwa kuwa uwanja wa riadha ya kisilaha, huku ikiwaumiza watu wa eneo hili ambalo zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni iko hapa. Iliwageuza kuwa masikini, licha ya utajiri wao mkubwa wa mali ghafi na nguvu kazi.   

Nne: Kila mmoja ni lazima atambue kuwa Uislamu unaobebwa na Hizb ut Tahrir kwa ufahamu sahihi ndio hadhara badala kwa wanadamu. Ndio njia pekee ya kuwakomboa watu wa eneo hili kutokana na njaa na umasikini wanaoishi ndani yake. Uhakika wa Uislamu, hukmu zake na nidhamu zake, katika kusimamia mambo ya watu huthibitisha kwa kila mwenye hisia kuwa hukmu za Kiislamu ni za kipekee katika kuangalia mambo ya watu, na kwamba huleta furaha, utulivu na haki kwa watu. Historia inathibitisha hili, na hili limefafanuliwa kwa kina na chama hiki, katika thaqafa yake iliyo chapisha katika vitabu vyake na tovuti zake.

Tano: Tunatoa wito kwa Ummah wa Kiislamu kuileta dini hii katika ngazi ya utawala. Hii ni kwa kupitia kuwafanya watu wenye nguvu na uwezo kutoa Nusra (usaidizi wa kinguvu) kwa Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa kinacho tambua jinsi ya kutawala kwa dini tukufu ya Uislamu ili Ummah urudi tena kuwa muangaza unaoongoza ulimwengu. Tunawakaribisha watu wa eneo hili, wanafikra, wale walio na hamu ya kuboresha hali ya watu wao, kuchukua dini hii ya ustaarabu ya Uislamu, kama itikadi, mfumo wa maisha na nidhamu ya serikali, na kuwataka viongozi kuchukua itikadi ya Uislamu na nidhamu yake ya utawala, ili waepuke hali mbaya wanayoishi ndani yake na kujiokoa na adhabu ya Jahannam:

 قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ

Sema: Enyi watu wa Kitabu! Njooni katika neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.     [Al-Imran: 64]

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu