Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  16 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 039
M.  Jumamosi, 19 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wafu Wetu wako Peponi Wafu Wenu wako Motoni
(Imetafsiriwa)

Ulimwengu ulipokea habari za kuuawa kishahidi kwa shujaa Yahya Sinwar; ambaye alikuwa mwiba ubavuni na donge kwenye koo ya umbile la Kiyahudi na wale waliokuwa nyuma yake, waliopanga Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo Oktoba 7, 2023, operesheni ambayo ilitikisa umbile la Kiyahudi, kutishia uwepo wake, na kutuma ujumbe wa vitisho kwa viongozi wa nchi za makafiri; maana yake ni kwamba Waislamu wanakuja!

Shujaa huyo shahidi alikuwa mmoja wa walengwa wa vita vya umbile la Kiyahudi dhidi ya Gaza, kutokana na kero lililojaza nyoyo za Mayahudi kutokana na Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa. Aliuawa kishahidi, Mwenyezi Mungu amrehemu, akitazama mbele wala asirudi nyuma, na wala sisi hatumsifu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Shahidi huyu, Mwenyezi Mungu amrehemu, na ndugu zake, wapiganaji, wamepata mafanikio makubwa dhidi ya maadui na wakaikanyaga ardhi iliyowakasirisha makafiri. Alitia matumaini kwa Umma wa Kiislamu, akaukumbusha kwamba ni Ummah wa risala na taifa bora lililoletwa kwa ajili ya wanadamu. Lengo la kulitokomeza umbile la Kiyahudi likawa ni uhalisia mbele ya macho ya Waislamu, wakingojea saa ambayo Mwenyezi Mungu (swt) atawakirimu kwa kuwang'oa watawala wajinga (Ruwaybidha) wasio na maana wanaowadhibiti, na watatoka na majeshi huku wakiimba Allahu Akbar, ili kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka uwepo wake na kukata kamba ambayo kwayo nchi kubwa zinawapa mahitaji yao.

Kinachochukiza ni kile alichofanya rais kikongwe wa Marekani kwa kumpongeza Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi kwa mauaji ya Yahya Sinwar. Kwa kufanya hivi, anauchokoza Umma wa Kiislamu na kuuchochea dhidi yake na nchi yake. Hebu raisi huyo kikongwe na ajue, na hebu utawala wake ulio nyuma yake na ujue kuwa muda wa kuhesabiwa unakaribia, Mwenyezi Mungu akipenda, kisha Khalifa wa Waislamu atakufundisheni mafunzo yatakayokusahaulisheni minong'ono ya Shetani!!

Ujumbe ambao tunaurudia katika tukio kama hilo ni kwamba Umma wa Kiislamu una lengo, na ni lazima uchukue hatua za uhai na kifo kuelekea hilo, ili lengo lake lipate ushindi, bendera yake inyanyuliwe, na wale waliouawa shahidi miongoni mwao kwa ajili yake waweze kupata shahada. Wakati wowote kiongozi anapouawa kishahidi, mwingine humrithi, na wakati wowote askari anapouawa, makumi ya watu huchukua mnafasi yake. Hata kama wana uchungu, maadui zetu wana uchungu kama sisi. Lakini sisi tunataraji kwa Mwenyezi Mungu yale wasiyoyatarajia, sisi tuna yakini na ushindi wa Mola wetu Mlezi (swt), kwani Yeye ndiye aliye sema:

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Ghafir: 51].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu