Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  9 Jumada I 1441 Na: 1441 H / 008
M.  Ijumaa, 03 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tuhuma za Putin dhidi ya Hizb ut Tahrir

Mnamo 10 Disemba 2019, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitoa hotuba ya kwanza kuhusiana na chama cha kimataifa cha Kiislamu cha kisiasa cha Hizb ut Tahrir. “Shirika hili liliasisiwa mnamo 1953 huko Jerusalem kutoka katika miongoni mwa watu wenu, kadhi wa mahakama ya Shariah. Katika nakala zake msingi za kisheria, moja kwa moja linatangaza umuhimu wa kubuni Khilafah kwa kuchukua madaraka na kupigia debe fikra zake katika nchi tofauti duniani, na dola ya Kirusi haikusazwa. Shirika hili linafanya kazi zake kihalali ndani ya nchi nyingi,” – alisema hayo katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu akijibu kauli ya wakili maarufu Yuri Kostanov, inayofichua ukandamizaji wa wanachama wa Hizb ut Tahrir kwa kuwatupa jela kwa miaka zaidi ya 25 na licha ya kukosekana ushahidi kuwa Hizb ut Tahrir inahusika na mashambulizi ya kigaidi. Kwa kuongezea, Putin alianza kwa kuleta hoja alizoandaliwa na vitengo vya usalama kuhusu umuhimu wa kuitambua Hizb ut Tahrir kuwa shirika la kigaidi. Kwa mfano, alisema Ujerumani na nchi za Shanghai Cooperation Organization (SCO), shirika linadaiwa kutambuliwa kama shirika la kigaidi, licha ya kwamba inafahamika maarufu kuwa Urusi ndio nchi pekee duniani ambapo Hizb ut Tahrir inatambuliwa kama shirika la kigaidi. Hata hivyo, alitoa hoja zaidi kwa kusema, “Amali zote za shirika hili zimefungika katika kuwakataza wanachama wa kundi lao wasiingie dini nyingine, kuingilia mambo ya kibinafsi na kifamilia na mfano wa haya. Lakusikitisha ni kuwa kumekuwepo na natija mbaya kutokana na unezaji wa fikra zao kuhusiana na yale wanayoyakataza kwa mfano, kutiwa damu. Na wamezuia watoto wao wasitiwe damu na ilhali walihitajika ili kuokoa maisha yao. Tukio baya la hivi majuzi lilitokea katika Muungano wa Urusi katika eneo la Kabardino-Balkaria mwaka jana. Mtoto alifariki. Pale ambapo msaada ulitolewa kwa nguvu kwa wafuasi wa kanisa hilo, hususan harakati hii na kupelekea kufaulu kuwaokoa watoto sehemu hiyo,” – Putin alihitimisha kwa hisia huku wasikilizaji wakiwa wameshtuka. “Kwa mara nyingine nataka kusema kwamba uamuzi huu ulitolewa na Mahakama ya Upeo ya Muungano wa Urusi kwa kufuata kiukamilifu sheria iliyoko nchini Urusi, na hivyo basi ni dharura kutekelezwa.”

Licha ya kwamba sisi katika Hizb ut Tahrir hatutafuti kuwaridhisha madhalimu ndani ya nchi za Waislamu na viongozi wa nchi za Ukafiri, lazima itambulike kwamba hakuna hata mmoja kati yao amekuwa na kiburi cha kuilaumu Hizb ut Tahrir kwa kile kinachoitwa “ugaidi,” kwa sababu inajulikana kwamba chama chetu hakiko katika mapambano ya kimamlaka. Lakini Putini, kwa uongo wake anadai kwamba Urusi inaifuata Ujerumani na nchi za SCO katika kuitambua Hizb kama shirika la kigaidi, akijifedhehesha mwenyewe na wala sio kuidunisha Hizb ut Tahrir.

Tunataka kusisitiza kwamba mjadala juu ya ukosefu wa haki na kutiwa korokoroni kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir umefikia kiwango kikubwa ndani ya Urusi kiasi kwamba taasisi za usalama zilitarajia swali hili kuulizwa katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu, na kumuandalia Putin jibu la uongo, karibia lote likijumuisha uzushi na udanganyifu. Putin alikiita chama chetu kanisa na kukilaumu chama kwa kupiga marufuku kutiwa damu, kiuhadaifu akichanganya Hizb ut Tahrir na Kanisa la Jehovah Witness.  Ima ilikuwa ni uwasilishaji wa kimakosa kutoka kwa Huduma za Usalama za Muungano (FSB) au ilikuwa ni makossa ya Putin – yote haya yanaonyesha kwamba kukosekana kwa mjadala wowote wa kuilaumu Hizb na kile kinachoitwa “ugaidi” miongoni mwa FSB na Putin.

Uongozi wowote uliopo nchini Urusi, sera yake msingi ni dhidi ya Uislamu nchini na kwingineko. Leo, huduma maalumu ndio mabwana wa nchi, na kwa mujibu wa hilo, ndio wanaoshinikiza mapambano dhidi ya Uislamu na kuhuishwa kwake. Ni muhimu pia kutambua kwamba, kufanyiakazi sera ya dhidi ya Uislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, huduma maalumu zimeboresha vyeo vyao na kupata mgao mkubwa wa bajeti kwa maana kwamba zinaongozwa sio tu kwa chuki zao dhidi ya Uislamu bali pia kwa uchu wa uongozi na ulafi. 

Urusi inauogopa Uislamu kwa sababu karne kadhaa imepigana vita vya kiuvamizi na kuziteka ardhi nyingi za Kiislamu ambazo inataka kuzihifadhi. Na lau mwanzoni Urusi ingefanyiakazi sera ya kuwafanya watu kuwa Wakristo, ingeli watesa, waua wale ambao wangeliingia katika Uislamu na kuwafurusha, leo inawanyima Waislamu haki zao kwa visingizio vya uongo na mashtaka ya kubuni. Mamlaka za Kirusi zinawasiwasi na Waislamu milioni 20 walioko nchini Urusi, wanataka watu hawa kusahau mustakbali wao na thaqafa yao adhimu ili wajiingize na wawe watiifu kuhudumikia “Kaisar wa Kirusi.” Hivyo basi kauli hii ya Putin na mapambano yake ya kidhalimu dhidi ya Hizb ut Tahrir ni muendelezo wa vita vya kihayawani dhidi ya Uislamu ambao kwamba dola ya Kirusi imekuwa inapigana nao kwa karne kadhaa. Leo, Kremlin haiwezi kuupiga marufuku Uislamu nchini na hivyo inadanganya kuhusu tishio la ugaidi, likijumuisha kutoka kwa Hizb ut Tahrir kwa sababu wanaona tishio kupitia wanachama wa chama chetu wanaona tishio la kurudi kwa Waislamu katika mfumo wao msingi – Uislamu.

Urusi haitoweza kuizamisha nuru ya ukweli si kwa ukandamizaji, wala uongo wake, wala njama zake za kijanja au kiini macho! Inawatesa Waislamu ndani ya Siberia, eneo la Volga, ndani ya Milima ya Ural, ndani ya Caucasus, wanawaua Waislamu Chechnya na Afghanistan! Mwenyezi Mungu anawaruhusu kutenda maangamivu yao mpaka muda maalumu ambapo watajutia uhalifu wao dhidi ya Waislamu na Mwenyezi Mungu hakika atakiweka kila kitu mahali pake.

Mwenyezi Mungu Muweza asema:

[وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao” [14:42].

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu