Jumatano, 29 Rajab 1446 | 2025/01/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  13 Rajab 1446 Na: H 1446 / 072
M.  Jumatatu, 13 Januari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala Vibaraka Wana Hofu juu ya Tishio kwa Viti vyao vya Utawala lakini Hawana Wasiwasi juu ya Vita vya Mauaji ya Halaiki!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumanne na Jumatano, wizara za mambo ya nje za Jordan, Saudia, Imarati, Mamlaka ya Palestina na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zililaani uchapishaji wa akaunti rasmi unaohusiana na umbile la Kiyahudi wa ramani za kanda hiyo ambazo ni pamoja na maeneo ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Jordan, Lebanon na Syria, wakidai kwamba hayo ni ramani ya kihistoria ya umbile la Kiyahudi. Walionyesha wasiwasi wao kuhusu masuala mawili:

Mojawapo ni shambulizi dhidi ya kile walichokiita ubwana wa dola na mradi wa serikali ya Palestina. Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia ilisema katika taarifa yake mnamo Jumatano kwamba “madai kama hayo yenye itikadi kali yanaakisi nia ya mamlaka zinazokalia kwa mabavu kuimarisha ukaliaji wao wa kimabavu, kuendelea na mashambulizi ya wazi dhidi ya ubwana wa nchi, na kukiuka sheria na kanuni za kimataifa.” Huku Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE ikitoa wito katika taarifa yake wa “... kukomesha vitendo haramu vinavyohujumu suluhisho la dola mbili, na kuasisiwa kwa dola huru ya Palestina.”

La mwisho kati ya haya ni suala la kuchochea kile walichokiita misimamo mikali katika kanda hiyo, kama alivyoonya Aboul Gheit kwamba “kufeli kwa jumuiya ya kimataifa kushughulikia vitendo hivyo vya uchochezi na matamshi ya kutowajibika kunahatarisha kuzidisha misimamo mikali na kukabiliana na misimamo mikali kwa pande zote.”

Kwa hiyo, watawala hawa vibaraka walikuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho kingeweza kutishia viti vyao vya utawala, iwe ni kwa sababu ya ndoto za Torati za upanuzi wa Mayahudi au kwa sababu ya mwitiko wa Waislamu kwa uchokozi wowote mpya ambao ungeweza kuwageuzia meza, na ufalme wao ungepotea na kuanguka kwa viti vyao vya utawala.

Watawala hawa hawakuwa na wasiwasi kuhusu vita vya mauaji ya halaiki ambavyo umbile la Kiyahudi limekuwa likiendesha Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi 15, na mauaji na kujeruhi zaidi ya watoto, wanawake na wazee elfu 150. Wala hawakujali kuhusu matukio ya watoto kufa kwa njaa na baridi huko. Wala hawakujali kuhusu matukio ya mbwa wakiitafuna miili ya mashahidi mitaani. Wala hawakuwa na wasiwasi kuhusu nyumba, shule, hospitali na misikiti ya Gaza ambayo imekuwa rundo la vifusi. Hakika hayo yote hayakuwatia wasiwasi, lakini yalipokuja yale yanayoweza kugusa viti vyao vya utawala, walitangaza wasiwasi wao.

Lau wangeongeza kwenye wasiwasi na kulaani kuhamasishwa kwa Ummah na majeshi yake ili kukabiliana na mipango na ndoto za Mayahudi, basi tungekuwa na matumaini na kusema kwamba hatimaye watakomesha kiburi cha Mayahudi. Lakini walifuata wasiwasi na kushtumu kwa uovu na kupuuza, kwa hiyo wakaunyenyekea tena mfumo wa kimataifa, ambao ni ule ule uliowawezesha Mayahudi.

Mayahudi, waliwaunga mkono na kuwasaidia dhidi yetu tangu walipoanzisha umbile lao katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na wakatoa wito tena wa kutelekezwa Palestina kupitia kile kinachoitwa dola ya Palestina na suluhisho la dola mbili!

Watawala hawa ni vibaraka wa ukoloni miongoni mwetu na walinzi wa maadui zetu, Mayahudi. Hawaachi juhudi yoyote katika kuwatumikia, lakini wakoloni hao huwashughulikia kama bwana anavyoshughulika na watumwa wake. Anawalisha kadiri atakavyowaweka hai, huku akiwatupa nje kando ya barabara wanapokuwa dhaifu au hawawezi kumtumikia. Kuna mifano mingi ya hili, ambayo mengine bado ni ya hivi karibuni, kama vile Bashar al-Assad. Kwa hiyo, watawala hao hutetemeka kila wanapohisi kwamba wako karibu kutolewa kafara. Lau wangekuwa na akili, wangeutambua ukweli huu na wangeharakisha kutubu kwa Mola wao na kujikomboa kutoka katika kuutumikia ukoloni. Lakini wanawezaje kufanya hivyo na hali wamefyonzwa na uhaini na kuurithi?!

Ni wajibu kwa Ummah kuchukua hatua na kurudisha usukani wa uongozi, kuwaondoa watawala hawa kwenye vifua vyake na kuweka mahali pao Khalifa mmoja muongofu ambaye atauokoa kutokana na Mayahudi, kuuokoa na ndoto zao za Kibiblia na kutokana na tamaa na maovu yote ya ukoloni, ili uregee kuwa Ummah huru na wenye heshima.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi.” [Ar-Rum: 4]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu