Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  15 Rabi' II 1446 Na: 02 / 1446 H
M.  Ijumaa, 18 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Biden Asherehekea Kuuwawa kwa Yahya Al-Sinwar!

(Imetafsiriwa)

Katika taarifa yake ya kina, Rais Joe Biden alithibitisha kwamba ujasusi wa Marekani ulisaidia “Israel” kumpata na kumlenga Yahya Al-Sinwar, pamoja na viongozi wengine wa Hamas waliojificha chini ya ardhi. “Kwa marafiki zangu wa Israel, hii ni siku ya afueni na tafakari, sawa na mandhari nchini Marekani baada ya Rais Obama kuamuru uvamizi wa Osama Bin Laden mwaka wa 2011,” Biden alisema. “Yahya Al-Sinwar alikuwa kizuizi kikubwa cha amani. Kizuizi hicho sasa kimeondoka, lakini kazi nyingi inabaki mbele.” (Habari za ABC)

1- Huku ni kukiri kwa moja kwa moja katika kuhusika kwa Marekani katika mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita unaofanywa mjini Gaza na Lebanon. Suala sio tu kuhusu Yahya Al-Sinwar bali kuhusu vifo vya Wapalestina zaidi ya 42,000, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee; waandishi wa habari 111; wafanyikazi 224 wa kibinadamu, wakiwemo 179 kutoka UNRWA; na kuhamishwa kwa zaidi ya raia milioni 2. Ni kuhusu watu 6,000 hadi zaidi 20,000 waliopotea, 99,153 na zaidi waliojeruhiwa vibaya sana, na 9,312 na zaidi waliowekwa kizuizini; Inahusu hospitali, shule, vyuo vikuu, maeneo ya ibada, na miundombinu iliyoharibiwa kwa kisingizio cha kujilinda.

2- “Joe Muuaji ya halaiki”, hakuna mtu aliyeshuhudia watoto wachanga wa “Israeli” waliokatwa vichwa, kama unavyodai, lakini ulimwengu uliona wakimbizi wa Kipalestina wakichomwa moto wakiwa hai katika kambi ya hospitali inayodaiwa kuwa mahali salama. Raia, wakiwemo wanawake na watoto, walilengwa na silaha zilizopigwa marufuku zilizotolewa na Marekani kwa “Israel”. Ulimwengu sasa unashuhudia njaa inayosababishwa na mwanadamu, ikitekelezwa na jeshi la Kizayuni linaloungwa mkono na meli kubwa za jeshi la wanamaji la Marekani, huku serikali nyingi za Ulaya zikiunga mkono au zinasalia kushiriki katika ukatili huu. Matukio ya kutisha ya mauaji ya Holocaust ambayo hayatatokea tena katika Ulaya yanarudiwa kwa mikono ya wahasiriwa wake wa zamani.

3- Tunawakumbusha wahalifu hawa wote kwamba Ummah wa Kiislamu unaamka, na haki itadumishwa. Nyinyi na wale wote wanaounga mkono mauaji haya ya halaiki mtawajibishwa. Tunakuonyeni kwa yale anayoyasema Mwenyezi Mungu:

[وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ ۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]

Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim: 42].

4- Tunawaambia wale wote wanaokabiliana na jinai hizi nchini Marekani na nchi za Ulaya endeleeni na juhudi zenu za kuwafichua na kupambana na wahalifu wa kivita na kuachiliwa huru kutoka kwa madhalimu wanaotumia jina lenu na rasilimali zenu katika jinai hizo.

Pia tunakuombeni mufikirie juu ya suluhisho la kweli la kimfumo ambalo Uislamu na Quran vinatoa kwa wanadamu wote, kama chanzo cha rehma kwa wanadamu.

5- Tunawaambia Waislamu: unganisheni juhudi zenu, ondoeni tawala vibaraka zilizopandikizwa na dola za kikoloni, na simamisheni mfumo adilifu wa Kiislamu (Khilafah) unaoleta rehma kwa wanadamu, unaoongozwa na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake Muhammad (saw). Hapo tu ndipo utukufu wa uhai, ukombozi wa kweli, na maendeleo ya halisi yatapatikana. Na kumbukeni Anayoyasema Mwenyezi Mungu:

[فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِۦ رُسُلَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٖ]

Basi usimdhanie Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kuwavunjia ahadi yake Mitume wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda, na ni Mwenye kulipiza.” [Ibrahim: 47].

6- Ama kuhusu waliouwawa, ni bishara njema:

[وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ]

“Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.” [Aali-Imran 3:169].

7- Tunaukumbusha ulimwengu mzima yale Ayasemayo Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَا ٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ ٱلَّذِى ٱرْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًۭا ۚ يَعْبُدُونَنِى لَا يُشْرِكُونَ بِى شَيْـًۭٔا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ]

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surat Al-Noor: 55].

Kwa kutamatisha Mwenyezi Mungu Atangaza:

[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰٓ أَمْرِهِۦ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu