Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  28 Shawwal 1444 Na: 02 / 1444 H
M.  Alhamisi, 18 Mei 2023

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ]
[وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Australia inaomboleza kuondokewa na mmoja wa wanaume ambaye alikuwa akipendwa sana na Waislamu kwa jumla na hasa wabebaji da’wah (Mwenyezi Mungu amrehemu):

Ndugu Ismail Al-Wahwah (Abu Anas)

Ambaye amefariki dunia kwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu (swt) leo, Alhamisi, tarehe 28 Shawwal 1444 H, sawia na tarehe 18 Mei 2023 M, baada ya kuvumilia maradhi na baada ya kutumia maisha yake katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt).

Abu Anas alijiunga na Hizb ut Tahrir mwishoni mwa miaka ya 1970 ambapo tangu hapo alifanya kazi bila kuchoka katika nchi nyingi za makaazi, mara nyingi akilazimishwa kuhama na tawala. Aliishi na kulingania haki nchini Palestina, Jordan, Yemen, Ujerumani, Denmark na Australia, daima akiwa juu ya neno na bila kuogopa lawama ya mwenye kulaumu wala ukandamizaji wa dhalimu.

Wale waliokutana naye wangetoa ushahidi wa mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na Ummah wa Muhammad (saw), akifanya kazi popote aliposafiri katika hali zote ili kuukomboa Ummah kutokana na uvamizi wa kigeni na kurekebisha hali yake kupitia kuregesha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Abu Anas (Mwenyezi Mungu amrehemu) alijitolea mhanga kwa kufungwa na kuhangaishwa mara nyingi na tawala dhalimu na mikono yao mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi kwa ajili ya kuwawajibisha madhalimu, bila kuyumba hata kidogo licha ya vitisho vya mara kwa mara na mateso ya kimwili.

Tunatoa rambirambi kwa familia ya marehemu na kwa wabebaji da’wah wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amfinike kwa rehema yake pana, ammiminie radhi na msamaha wake (swt) na amruzuku mabustani yake mapana pamoja na mitume, wakweli, mashahidi, na watu wema. Hatimaye tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awalipe mema familia na jamaa zake na awape subira na faraja.

Hakika macho yanabubujika machozi na moyo unahuzunika, lakini hatutasema isipokuwa yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi.

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu