Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  12 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 04 / 1444 H
M.  Alhamisi, 01 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uhalifu wa Kivita wa Mkongwe wa Vita Aliyepambwa Zaidi wa Australia ni Akisi ya Sera ya Vita ya Serikali

(Imetafsiriwa)

Madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya mkongwe wa vita aliye hai nchini Australia, Ben Roberts-Smith, yalipatikana kuwa "kweli kabisa" na jaji wa Mahakama ya Shirikisho. Jaji huyo alihitimisha kuwa madai ya kuwashambulia na kuwaua Waafghani wasio na hatia na wasio na silaha yalithibitishwa, na kwamba alileta fedheha kwa nchi yake na jeshi la Australia kwa kuvunja 'kanuni za maadili na kisheria' za ushiriki wa kijeshi.

Hizb ut Tahrir / Australia ingependa kusema yafuatayo:

1. Uhalifu wa asili ulikuwa ni vita vyenyewe. Serikali ya Australia kwa upofu lakini kwa hiari ilifuata mashini ya kivita ya Marekani katika uvamizi na kuikalia kimabavu Afghanistan. Hii ilisababisha kuuawa kwa maelfu ya watu wasio na hatia, kuwafukuza wengine wengi zaidi, kuivuruga na kuipora nchi nzima kwa sababu ya sababu zisizo na msingi.

2. Inatarajiwa tu kwamba wanajeshi, walioshajiishwa na sera za serikali na simulizi za uwongo, wawe na tabia inayoakisi wakubwa zao huko Canberra.

3. Kimsingi fedheha iliyoletewa Australia na serikali iliyochagua kuvamia na kusababisha mambo ya kutisha yasiyoelezeka katika nchi nyingine. Uamuzi wa kwenda vitani ulisababisha kusambaratishwa kwa miji yote, kutumiwa kwa silaha za uharibifu zaidi kuwahi kupatikana tangu Hiroshima, uanzishwaji wa vyumba vya mateso, Kambi ya anga ya Bagram, programu za uwasilishaji na chati za kuua, huku wafu wakionyeshwa kama kumbukumbu tu kwa wanajeshi waliopotoka. Huu ndio urithi wa serikali wa vita vya Afghanistan, ambao hauwezi kutenduliwa kwa kumtoa kafara mwanajeshi mmoja au wanajeshi wachache.

4. Hizb ut Tahrir imeonya mara kwa mara dhidi ya matokeo ya vita kuanzia siku ya kwanza. Hizb ut Tahrir daima ilishikilia kwamba uvamizi na kuikalia kimabavu Afghanistan kutakuwa ni kushindwa vibaya na kwamba jinai za uvamizi wa washirika daima zitakuwa ni doa la jinai kwa wasimamizi wa amri ya baada ya WWII.

5. Ulimwengu unahitaji sana njia badali ya mwenendo kwa ile inayoonyeshwa na dola kuu za ulimwengu za leo. Mataifa haya yanafanya bila ya kuadhibiwa kuangamiza nchi nzima kwa jina la maslahi ya kitaifa ambayo kwa kweli huwanufaisha mabepari wachache tu. Mtindo huo badali wa tabia ni ule unaoegemezwa juu ya Uislamu ambao unaainisha chimbuko la sheria lisiloweza kuathiriwa na matakwa ya kipote cha wachache.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu