Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  14 Muharram 1446 Na: 02 / 1446 H
M.  Jumamosi, 20 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kama Umma Mmoja: Waislamu Wanasimama pamoja na Watu wa Bangladesh Dhidi ya Dhalimu Sheikh Hasina

(Imetafsiriwa)

[إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]

“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Quran 21:92]

Watu wa Bangladesh—zaidi ya 92% yao ni Waislamu na sehemu ya mojawapo ya Waislamu wengi zaidi duniani—wamejitokeza katika maandamano ya amani yanayoongozwa na wanafunzi dhidi ya dhalimu Sheikh Hasina.

Maandamano ya hivi punde yalizuka baada ya serikali inayoongozwa na Hasina kujaribu kuongeza mgawo wa nafasi za kazi serikalini kwa kuwapendelea wafuasi watiifu wa serikali badala ya wagombea wenye sifa stahiki. Sera hii ni ya hivi punde tu katika mfululizo wa vitendo vya rushwa na uonevu vinavyofanywa na serikali ya Awami League tangu iingie mamlakani mwaka wa 2009.

Bangladesh chini ya utawala huu dhalimu imekumbwa na chaguzi za udanganyifu wa kura, rushwa iliyokithiri serikalini, kuteswa na kuuwawa viongozi wa kisiasa na kidini, sera za kibaguzi dhidi ya Waislamu wa Rohingya wanaotafuta hifadhi, hatua za kuhalalisha mahusiano na umbile la Kizayuni, ushirikiano na Waziri Mkuu wa India Modi, mwenye chuki na Uislamu, na kuporomoka kwa uchumi, kwa kutaja machache tu. Watu wa Bangladesh, kama vile wengine wote katika Ummah, wamechoshwa na madhalimu wao, wanaoungwa mkono na wasaidizi wao wa kikoloni.

Wiki chache zilizopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong alikutana na Sheikh Hasina “kuimarisha uhusiano wao wa kiuchumi,” akipuuza ufisadi na ukatili wa serikali ya Hasina. Hili halishangazi, kutokana na historia ndefu ya viongozi wa nchi za Magharibi kuwaunga mkono madikteta katika ulimwengu wa Kiislamu ili kupata rasilimali na masoko ya Umma. Hivi majuzi, Australia imeonyesha uungaji mkono wa jumla kwa umbile la Kizayuni katika mauaji yake ya kutisha ya halaiki mjini Gaza.

Vurugu za kikatili zilizofanywa dhidi ya waandamanaji wa amani nchini Bangladesh ni mfano mwingine wa mapambano ya Ummah kujiondoa katika mifumo ya kigeni na madikteta wao waliowekwa na wakoloni. Wakoloni hawa walitugawanya, wakatupa kitambulisho kipya, wakatuweka dhidi yetu sisi kwa sisi, na kupora mali zetu baada ya uvamizi wao katili katika ardhi zetu.

Suluhisho pekee linalowezekana ni kuungana kama Umma mmoja chini ya mfumo wa kisiasa ulioteremshwa kwa kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw). Mfumo unaowapa watu mamlaka ya kuchagua na kuingia madarakani mtawala wamtakaye ambaye anatawala kwa Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Mfumo unaoweka maliasili katika umiliki wa raia wake na sio mashirika ya kimataifa ambayo mirabaha yake inawekwa mfukoni na mafisadi. Mfumo ambao kipaumbele chake kiuchumi ni kuhakikisha ugavi wa haki wa mali ili mahitaji ya kila mwananchi yakidhi. Mfumo unaowaleta pamoja watu kwa msingi wa malengo na mfumo wa imani ikinaishayo akili ambao unasimamiwa kwa lazima na kulindwa na Ummah kwa kuwahisabu watawala kwa upotovu wowote kutokana na yale waliyowekewa bay’ah juu yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالأَقْرَبِينَ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقَيرًا فَاللّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلاَ تَتَّبِعُواْ الْهَوَى أَن تَعْدِلُواْ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu.” [Quran 4:135].

Bila kujali tofauti zetu za kijiografia, kila Muislamu anasimamia haki na uadilifu kwa ajili ya ndugu na dada zetu nchini Bangladesh wanapokabiliwa na vurugu za kutisha huku kukiwa na kukatwa kwa mawasiliano na kutumwa kwa jeshi dhidi yao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aukomboe Ummah kutoka katika dhulma za watawala wanaoungwa mkono na wakoloni na atujaalie kiongozi muongofu na muadilifu.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake.” [Quran 12:21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu