Jumatano, 12 Ramadan 1446 | 2025/03/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  8 Ramadan 1446 Na: H 1446 / 31
M.  Jumamosi, 08 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuanzia Mjumuiko wa “Matembezi kwa ajili ya Khilafah” yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir, watu wanaopenda Uislamu wanawaita watoto wao wa kiume katika jeshi kujitokeza ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume;
Na ili kuiridhisha Marekani na India, vibaraka wao wamewashambulia kikatili watu waliofunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan walioshiriki katika mjumuiko wa “Mtembezi kwa ajili ya Khilafah”

(Imetafsiriwa)

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 tarehe 3 Machi, 2025, ya kuondolewa kwa Khilafah tukufu, Hizb ut Tahrir, Wilayah Bangladesh, iliandaa mjumuiko wa “Matembezi kwa ajili ya Khilafah” mnamo siku ya Ijumaa, Machi 7, 2025, baada ya Ijumaa, kutoka kwenye Lango la Kaskazini la Baitul, wakitaka kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume. Maelfu ya watu wanaopenda Uislamu kutoka matabaka mbalimbali walishiriki kwa hiari katika mjumuiko huu, wakipuuza vitisho vya vibaraka wa Marekani-India. Kutokana na mkusanyiko huu, watu wanaopenda Uislamu waliwaita watoto wao wanaotumikia jeshi kutoa nusrah (msaada wa kimada) kwa uongozi wa dhati wa Hizb ut Tahrir, katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

Mnamo tarehe 3 Machi 1924 M (28 Rajab, 1342 H), chini ya njama ya Mkoloni Kafiri Uingereza, kibaraka wao Mustafa Kamal Pasha alitangaza kufutwa kwa mfumo mtukufu wa Khilafah wa Umma wa Kiislamu. Wakoloni wa Kikafir wa Magharibi, hasa Uingereza na, baadaye Marekani, kisha wakaweka mfumo wa ukafiri wa kirasilimali wa kisekula na matabaka ya vibaraka wa kisekula wanaotawala juu ya Umma wa Kiislamu. Hivi leo, Umma wa Kiislamu umegawanyika katika zaidi ya mataifa hamsini bila mlinzi, Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa unakaliwa kwa mabavu na umbile la Kiyahudi lililolaaniwa, damu ya Waislamu inamwagika nchi baada ya nchi, ikiwemo na Palestina-Kashmir-Rohingya, Iman na heshima ya Waislamu zinachafuliwa, na mali zao na ubwana wa ardhi zao zinafujwa. Licha ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao mnapigana nyuma yake na mnajilinda kwaye (Sahih Muslim).

Kama ilivyo katika nchi nyingine za Waislamu, wanasiasa wa kisekula wa Bangladesh wanaondoa aibu yao ya mwisho (jani la mkuyu) na wanaonyesha utumwa wao kwa maadui wa wazi wa Umma wa Kiislamu, hasa Marekani-Uingereza na mshirika wao wa kikanda India. Kwa hivyo, watu hawana hamu na kinachojulikana kama mageuzi na sarakasi za uchaguzi. Mwenyezi Mungu (swt) anatahadharisha kuhusu vibaraka hao kwa kusema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surah Maidah: 51].

Katika ombwe hilo la kisiasa nchini, tunakaribisha hamu ya mabadiliko ya vijana wanaoongoza vuguvugu la kupinga ubaguzi. Hata hivyo, tunataka kuwaonya kwamba mfumo wa kisekula wa kirasilimali wa Magharibi ni wa kidhalimu na wa kibaguzi; kwa hiyo, chama chao kipya kitashindwa kutimiza matumaini na matarajio ya wananchi kwa kuubakisha mfumo huu uliofilisika. Tunapenda kuwakumbusha kwamba nukta yamaregeleo yao ni tarehe 3 Machi, 1924, yalipoanza mapinduzi ya kuregesha Khilafah ya Umma wa Kiislamu, na kwamba mafanikio ya mapinduzi haya yatakuja tu kwa kuiregesha Khilafah kwa mujibu wa njia ya Utume.

Kwa hiyo, urithi wa Waingereza wa 1947 haupaswi kuwa kigezo chao, vyenginevyo katika historia watakumbukwa kama Vijana wasaliti wa Kituruki - ambao walitumiwa kama farasi wa Trojan na Magharibi kuivunja Khilafah. Tunatoa wito kwao kuungana na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ili kuikomboa Bangladesh mpya kutoka kwenye makucha ya Wakoloni wa Marekani-Uingereza na mshirika wao wa kieneo India. Mtume wetu kipenzi, wa Mwenyezi Mungu (saw), alisema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “...kisha utawala wa kiimla utakwisha, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” (Hadith: Musnad Ahmad).

Enyi Maafisa Wenye ikhlasi katika Jeshi! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«... وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “...mwenye kufa bila ya kuwa na kiapo cha utiifu (Bay’ah”) shingoni mwake, hufa kifo cha Kijahiliya.” (Sahih Muslim). Nyinyi ni wana wa Umma wa Kiislamu ambao wana uwezo wa kijeshi mikononi mwao, ambao kupitia kwao mnaweza kuwakomboa Waislamu kutoka katika Jahiliyyah hii. Jibuni matakwa ambayo watu wanayataka kwenu kupitia mjumuiko wa leo wa “Matembezi kwa ajili ya Khilafah” na mutoe Nusrah (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah. Fuata nyayo za mtangulizi wenu, Sa’ad bin Mu’adh (ra). Lazima mjue kwamba pale majeshi yakiongozwa na Sa’ad bin Mu’adh (ra) mjini Madina yalipoondoa usaidizi wao na ulinzi kutoka kwa kiongozi kafiri Abdullah bin Ubayy na kumpa itifaki Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Abdullah bin Ubayy aliyekosa nguvu alipoteza uwezo wake na akawa mtazamaji tu. Kwa kweli, ni katika ushindi wa Uislamu pekee ambapo watu wataungana na kusherehekea wito wa kweli wa Takbir.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu