Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  9 Muharram 1443 Na: 02 / 1443 H
M.  Jumanne, 17 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miaka Ishirini ya Uvamizi Imeiacha Afghanistan ikiwa Magofu na Wanasiasa wa Denmark Wanashiriki Kamili katika Uovu Huu!

(Imetafsiriwa)

Baada ya miaka ishirini ya uvamizi, mataifa yanayopigana ya Magharibi, ikiwemo Denmark, yameondoka Afghanistan. Kwa miaka ishirini, dola za Kimagharibi zimesababisha mauaji ya mamia ya maelfu ya watoto, wanawake na wanaume wasio na hatia, na kuilipua mabomu nchi hii hadi kuwa magofu. Vita hivi vifasiriwa kwa ujanja kama vita dhidi ya ugaidi na kudaiwa "kuwaokoa" watu wa Afghanistan, haswa wanawake wa Afghanistan.

Uvamizi huu mkali, ambao Denmark imekuwa sehemu yake katika kuihudumia Amerika, imeshirikiana na walanguzi wa dawa za kulevya na wababe wa kivita, kuunda magereza ya mateso na kufanya uhalifu wa vurugu wa kivita. Vita hivi vya Miaka Ishirini vimekuwa jinamizi moja refu kwa watu wa Afghanistan, na nchi hii imesalia katika machafuko ya kihistoria na mateso. Wakati huo huo, imeipa Taliban udhibiti kamili wa nchi hii, kama ilivyofanya kabla ya vita vya msalaba vya 2001.

Ni ngumu kuona jinsi ushiriki wa Denmark katika vita hivi umeiacha Afghanistan katika hali nzuri kuliko kabla ya wanasiasa wa Denmark kuchagua kujiunga na vita hivi vya Kiamerika na kutuma wanaume na wanawake wachanga wa Kidani kufa kwa ajili ya hili. Uhalisia ni kwamba ushiriki wa Denmark unaacha msusuru mbaya wa vifo, uharibifu na ugaidi wa serikali nyuma yake!

Bado, kungali hakuna uchunguzi wa kibinafsi unaopaswa kufuatwa kati ya wanasiasa wa Denmark, lakini badala yake usisitizaji wa kijeuri juu ya kuhadithiwa upya kwa namna Taliban ilivyowatendea wanawake, ili kuhalalisha kushiriki vitani, ambapo inapaswa tu kuhakikisha kuwa simu imechukuliwa jijini Washington wakati simu inapokuja kutoka Copenhagen!

Wala hakuna uchunguzi wowote wa kibinafsi kati ya vyombo vya habari vya Denmark, ambavyo kwa upendeleo vimejifanya kama washikilia kipaza sauti kwa wanasiasa kwa miaka 20 iliyopita. Vyombo vinavyoitwa "huru" vya habari vilivyoasisiwa vya Kideni vimepuuza kwamba Denmark, kama sehemu ya uvamizi huu wa kikatili, imeshiriki katika mauaji ya watu wengi na badala yake imethibitisha simulizi ya uwongo kwamba Denmark ilituma wanajeshi kuwaokoa wanawake masikini waliovaa burqa wa Afghanistan.

Lakini, wasiwasi wa wanasiasa wa Denmark kwa wanawake nchini Afghanistan hausikiki tu kuwa mtupu, lakini pia ni kielelezo cha kiburi cha kithaqafa ambacho hujitokeza wakati ambapo vurugu zinafanywa kwenye katiba kuzuia uhuru wa wanawake wa Kiislamu nchini Denmark, huku utunzi wenyewe hiyo simulizi  ukizama katika kashfa za MeToo!

Ushiriki wa Denmark katika uvamizi wa Afghanistan ni kasoro ya kihistoria, ambayo inawekwa wazi zaidi tu na ukwepaji mkali uwajibikaji na majaribio ya kuondoa umakini kutoka kiini cha jambo hili, ambalo tunalishuhudia kwa sasa kutoka kwa serikali ya Denmark na wanasiasa wanaohusika.

Badala ya kukubali kushindwa na kosa la kihistoria, wanasiasa wanarudia kwamba hawakuipiga bomu nchi hii bure, na kwamba wanajeshi wa Denmark hawakufa bure, labda zaidi katika jaribio tupu la kujidanganya wenyewe.

Historia, hata hivyo, inalaani washiriki wote wa vita hivi vya msalaba vya umwagaji damu kama wahalifu wa vita hivi wenye kejeli ambao wanastahili kushtakiwa hadharani na kuadhibiwa vikali kwa mauaji yao ya halaiki ya wanaume, wanawake na watoto wa Afghanistan.

 #أفغانستان                    #Afganistan             #Afghanistan 

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu