Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  22 Shawwal 1444 Na: 1444 / 15
M.  Ijumaa, 12 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Huwezi Kupeana Usichokuwa Nacho
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumanne na Jumatano, Mei 9 na 10, 2023, Baghdad ilikuwa mwenyeji wa kongamano lake la kwanza wa kimataifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya, katika uwepo wa wawakilishi wa nchi nane: Saudi Arabia, Misri, Lebanon, Jordan, Kuwait, Syria, Iran, Uturuki na mabaraza na afisi za Kiarabu na kimataifa. Kama kawaida, mkutano haukutoa suluhisho lolote kwa sababu walitafuta mbali na sababu za jambo hili na kuenea kwake kwa njia ya kutisha. Baada ya uvamizi wa Marekani mnamo 2003, Iraq ilikuwa ni kivuko cha usafirishaji wa dawa za kulevya, na kisha kwa mlanguzi na mtumiaji! Katika takwimu, Kurugenzi ya Kupambana na Dawa za Kulevya katika Wizara ya Mambo ya Ndani ilifichua kukamatwa kwa karibu watuhumiwa 17,000 wa ulanguzi wa dawa za kulevya, upigiaji debe na utumiaji vibaya, katika mwaka wa 2022.

Iraq baada ya kukaliwa kwa mabavu, imekuwa eneo la kawaida kwa wote, hasa kwa vile sehemu kubwa ya mipaka na vivuko vya nchi kavu kwenye mpaka wa Iran upande wa mashariki, na Syria upande wa magharibi, ambapo aina mbalimbali za madawa ya kulevya husafirishwa kwa magendo siku nzima inadhibitiwa na wanamgambo wenye silaha (mtuhumiwa wa kwanza wa upigiaji debe dawa za kulevya). Bali, kuna maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa wanamgambo hao, kama vile Jurf al-Sakhar, baada ya watu wake kutelekezwa na kuzuiwa kuingia humo kwa takriban miaka minane kwa uamuzi wa makundi haya, na kuibuka kwa maelezo mengi kuhusu maumbile ya shughuli za makundi hayo ndani ya mji na mabustani yake yenye miti mingi, miongoni mwao ni kilimo na utengenezaji wa madawa ya kulevya, pasi na afisa yeyote katika serikali zilizopita, hadi serikali ya sasa, kusubutu kuingia mjini humo na kukanusha au kuthibitisha taarifa zinazosambazwa kuhusu kile kinachoendelea ndani yake.

Kwa hivyo ni masuluhisho gani yanayotarajiwa kutoka kwa mkutano kama huo?! Serikali ya Iraq haina uwezo wa kukabiliana na ongezeko la tatizo la madawa ya kulevya nchini humo kutokana na ufisadi na udhaifu wa muundo wa usalama. Mfano wa ufisadi ni kile Al-Arabiya ilichochapisha mnamo tarehe 28/2/2022: "Mnamo Januari 2018, mamlaka ya usalama ya Iraq ilikamata genge la ulanguzi wa dawa za kulevya katika mji mkuu, Baghdad, likiwa na watu watatu, mmoja wao akiwa mtoto wa gavana wa wakati huo wa Najaf, Louay Jawad al-Yasiri. Walikuwa na kilo nane za dawa za kulevya, na mahakama ilitoa kifungo cha maisha kwa ajili yao." Kisha: "Watatu hao walipata msamaha wa rais mnamo tarehe kumi ya Januari 2022, kwa njia ambayo haikutangazwa, huku afisa mmoja mkuu wa polisi akiiambia France Press kwamba "mtoto huyo wa gavana aliachiliwa wiki tatu zilizopita na tulikabidhi amana zake zote kwake baada ya amri ya rais."

Mwakilishi Mishaan Al-Jubouri aliandika, "Kujiuzulu kwa gavana wa Najaf kulikubaliwa mnamo Jumatano 1/4/2022, na pendekezo la kumsamehe mwanawe, ambaye alipatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya na genge lake, lilitolewa mnamo 1/5, na amri ya kuwasamehe ilitolewa tarehe 1/10."

Enyi Waislamu: Kuenea kwa madawa ya kulevya, upotovu na kila aina ya machafu kunatokana na mfumo muovu wa kibepari na demokrasia yake fisidifu, hivyo wanadamu wanatarajia nini kutokana na mfumo ambao umewekwa na mtu mwenye kikomo, mapungufu na mahitaji? Na kipimo chenye kutumikia matendo yake binafsi, na uhuru wa dini, umiliki, maoni na uhuru wa kibinafsi ndani yake ni kamili hayana mipaka?!

Tatizo hili na matatizo mengine yanayoletwa na mfumo wa kibepari hayashughulikiwi kupitia makongamano ambayo kwayo wawakilishi wa nchi ambazo ni vibaraka wa Magharibi hukutana, wakiwa na shauku ya kutabikisha hadhara yake na kueneza mawazo yake. Bali, suluhisho lake ni kuung’oa mfumo huu ambao umewahuzunisha wanadamu na kuijaza dunia dhulma na ufisadi, na kusimamisha mfumo wa uadilifu wa Uislamu ambao Muumba, Mwenyezi, Mtukufu, ameukubali kwa ajili ya furaha ya wanadamu. Kwa hivyo kwa ajili ya kuifanyia kazi faradhi hii kubwa, tunakuiteni nyinyi Waislamu, kuishi maisha ya staha duniani na kupata radhi za Mola wenu Akhera.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu