Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  21 Jumada II 1443 Na: 1443 / 13
M.  Jumatatu, 24 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uundaji Vyama vya Kisiasa chini ya Mwavuli wa Mfumo na Katiba iliyotungwa na Mwanadamu ni Kuisaidia Serikali na Kuipatia Uhai, Haiamshi wala Kukomboa Taifa lolote.
(Imetafsiriwa)

Hatua za pamoja za chama ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko yoyote katika jamii. Mfano wetu na kiigizo chetu, Muhammad (saw) alianzisha jambo hili. Kazi yake ya kusimamisha Dola ya Kiislamu na kusimamisha Dini duniani ilikuwa ni kitendo cha pamoja. Mtume (saw) alikuwa akiwakusanya Maswahaba zake na kuwafundisha Uislamu katika nyumba ya Al-Arqam bin Abi Al-Arqam, walikuwa ni kundi lenye maana yote ya neno chama. Muhammad (saw) na Maswahaba zake walifuata njia hiyo hiyo mpaka wakasimamisha dola ya Kiislamu mjini Madina, hali ya heshima na utu, yenye uadilifu na huruma, ambayo ilikua mpaka ikatawala dunia kwa zaidi ya miaka elfu moja, ambapo hukmu za Uislamu zilitabikishwa, mpaka nguvu za ukafiri na ukoloni zilipoungana na kupigana dhidi yake na kuuangamiza.

Tangu wakati huo, zaidi ya miaka mia moja iliyopita, Waislamu wamekuwa wakiishi kwa kutawanyika katika ardhi zote, hakuna dola inayowaunganisha wala Uislamu hautabikishwi juu yao. Na wamekuwa kwenye mkia wa mataifa, na dola zao za kitaifa, zilizoasisiwa na wakoloni makafiri, ziko katika kuporomoka; hii ni kwa sababu ya watawala na tawala za vibaraka ambazo zimepandikizwa na mkoloni huyu.

Serikali nchini Jordan, kama ilivyo kwa serikali zote zilizopo katika nchi za Kiislamu, ilikuwa na bado ingali na nia ya kuhakikisha kuwa hakuna vyama makini na vya ikhlasi vinavyoegemezwa katika msingi wa kubadili fikra, vipimo na ukinaifu wa wananchi hususan vyama vya kisiasa vya kimfumo vinavyofanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, kupitia kuregesha Dola ya Khilafah upya. Kwa niaba ya nchi kubwa za kikoloni, iliapa kuwapiga vita na kuwakandamiza wanachama wao na kuwafunga, kwa sababu wanajua kwamba kwa kuregea Dola ya Khilafah, kutengwa na kufukuzwa kwao katika nchi za Kiislamu kutatokea, na utakuwa ndio mwisho wa utegemezi wa tawala hizi.

Lakini baada ya mapinduzi ya Ummah, harakati zake, na utambuzi wake unaoongezeka, wakiwemo watu wa Jordan, kutokana na dori za kufedhehesha za utawala huo, ambazo zimedhihirika mbele ya watu wote, hata mbele ya vituo viovu vya watawala na zana zao, huku utawala ukikusudia kutekeleza, katika dori za mwisho ulizokabidhiwa kwake kwa kuitumia Jordan na watu wake kwa suluhisho la Amerika na Uingereza kwa umbile la Kiyahudi, iwe ni suluhisho au makubaliano ya kisiasa, kiuchumi au kiusalama, ambayo ibara zake zimetekelezwa ardhini kwa miaka. Ili kuendelea kutawala, tawala hizi na mabwana zao kutoka kwa makafiri wa kikoloni huko Amerika na Ulaya, walionekana kuanza kile kinachoitwa mageuzi ya kisiasa na usasa ya mfumo wa kisiasa na marekebisho ya kina ya kikatiba, chini ya kifiniko cha kuhuisha maisha ya kisiasa na kuwashajiisha watu kujihusisha na vyama na maisha ya chama, na kurekebisha taratibu za uchaguzi ili ziwe za haki na uwakilishi zaidi kama wanavyodai.

Ili kukabiliana na mwito huu wa uwongo na wa kupotosha wa serikali kwa kile kinachoitwa usasa wa mfumo wa kisiasa na mageuzi ya kisiasa, tunaangazia yafuatayo:

1- Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha Waislamu waanzishe makundi ya kisiasa miongoni mwao, walinganie Uislamu na waamrishe mema na kukataza maovu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Aal-i-Imran: 104].

Matakwa haya ni faradhi ya kutoshelezana (fard kifayah), na kama Shariah inavyosema, kundi hili au chama hiki lazima kiwe na msingi wa Uislamu, na lazima kiwe cha kisiasa; kwa maana ya kuwa kazi yake ni kuamrisha mema na kukataza maovu, yaani kuwawajibisha watawala na kuwalinda watawaliwa.

2- Kuanzishwa kwa vyama katika Uislamu hakuhitaji ruhusa kutoka kwa mtawala, bali ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ambayo ni faradhi, na aya imefunga kuwa makundi yawe ya Kiislamu, na uwepo wake ni lazima uhakikishe kazi inayotakiwa kwao katika aya hiyo tukufu, inayoashiria kuruhusiwa kwa wingi wa vyama.

3- Mkoloni na serikali zinazotawala daima zimejenga fikra ya kujiweka mbali na siasa na vyama, ili wao peke yao wasimamie mambo ya Ummah kwa maslahi yao na ya mabwana zao. Hii ni kuwafukuza watu kutoka kwa vyama tiifu vya kisiasa, na kutokana na hatua za kisiasa. Ni serikali hii, kwa vitendo vyake vya ukandamizaji, ambayo imewazuia watu kujiunga na vyama, kwa kutumia mbinu za kuwafunga, kuwatesa na kuwapiga vita watu katika riziki zao. Haionekani kuwa makini na yenye ikhlasi katika kutoa wito wa ushiriki wa chama, isipokuwa kufikia kikomo kinachohitajika cha uwepo wao, mbele ya utiifu wake kwa nguvu za shinikizo la wakoloni, na kutumikia serikali katika dori zake zilosalia.

4- Haijuzu muundo wa chama kwa Waislamu kuwa katika misingi isiyokuwa Uislamu kama itikadi na mfumo, kwani vyama hivyo vimeegemezwa katika misingi ya demokrasia ya kisekula, kama ilivyo nchini Jordan, inayotenganisha dini na maisha. Ni vyama vya serikali na sio vya Ummah, kwani demokrasia sio dini ya Ummah, bali ni dini ya makafiri wa kikoloni, kwa sababu ni sheria zilizotungwa na mwanadamu, sheria za matamanio ya mabunge, sasa basi vipi ikiwa demokrasia ni fisidifu, na ufisadi wake umeongezeka kwa mfumo kupitia kughushi vyombo vyake vya bunge, kamati, serikali na marekebisho ya katiba!

5- Serikali ya Jordan haikubali vyama isipokuwa vya aina yake na kwa mujibu wa katiba, haswa katiba iliyorekebishwa na masharti yaliyowekwa na utawala huo kuhakikisha unaendelea kutawala; kwamba hivi lazima viwe vyama vya "kikatiba" au vyama vya aina ya utawala, au chini ya udhibiti na mamlaka ya utawala ikiwa ni nje ya udhibiti wake. Na kuanzishwa kwa Baraza la Usalama wa Kitaifa ni kwa ajili tu ya lengo hili. Kwa kuzingatia kuviruhusu vyama kulingana na kipimo cha mamlaka iliyopo, inawezekana katika siku zijazo kuunda serikali, kwa kisingizio cha kusasisha mfumo wa kisiasa na mageuzi ya kisiasa, ili kukidhi maagizo ya mkoloni Magharibi.

6- Umma unawezaje kuviamini vyama hivi wakati kuna vyama zaidi ya 53 vilivyopewa leseni, cha hivi punde zaidi ni kukipa leseni haraka chama kinachojumuisha wabunge 48, wakiwemo viongozi 9 na manaibu 39, pamoja na mawaziri wa zamani? Zaidi ya vyama 17 vimeomba leseni kwa mujibu wa katiba au sheria ya chama ijayo iliyofanyiwa marekebisho?! Wanatafuta - wapende wasipende - kuwa sehemu ya mchezo wa serikali inayotawala na ufisadi wake, utegemezi wa Magharibi, kuwalaghai raia wake na ukaribu wake na maadui wa Umma huu kama vile umbile la Kiyahudi, Amerika na Uingereza. Wanawezaje kukubali kufuata mkondo wa serikali, na kuwa chini ya udhibiti wa serikali na vyombo vyake vya ukandamizaji vinavyotekeleza kila aina ya vikwazo, ikiwa watakengeuka kutoka kwa udhibiti wao? Hii inaashiria ombwe la kifikra, kujisalimisha, na kujifungamanisha na serikali katika uharibifu wake wa nchi, kupora mali yake, na kuiweka rehani kwa maadui zake.

Enyi Watu… Enyi Watu wa Jordan:

Chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu, ambacho kilianzishwa kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na sio leseni kwa mujibu wa kipimo cha watawala, bali ndicho chenye kuwawajibisha watawala na kudhihirisha njama zao dhidi ya Ummah kwa mwamko wake wa kisiasa na Shariah dhidi ya nchi za kikoloni za Magharibi na njama zao na kuzifichua, kinachofanya kazi kwa bidii na ikhlasi kusimamisha dola ya Kiislamu ili kuregea mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kuwa ndio mradi wa Umma katika ardhi za Kiislamu, na kinabeba njia moja na kauli moja katika nchi zote za Waislamu, ni Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake.

Dola ya Kiislamu ya Khilafah ndio dola itakayorudisha heshima kwa nchi na waja wa Mwenyezi Mungu, na ndiyo itakayowaunganisha katika dola moja ambayo ina khalifa mmoja, ambaye mambo yote yako mikononi mwake mwenyewe, sio mikononi mwa watu maadui zake, na wala haiwaogopi maadui zake, kwa hivyo haijisalimishi kwao, na kukanyagwa mbele yao na kudhalilishwa nao. Bali, inauongoza Ummah kufukuza ushawishi wa Marekani na Uingereza na kuyaelekeza majeshi kuliondosha umbile la Kiyahudi. Inatembea kwa kasi kuelekea mwinuko na mwamko kati ya mataifa ili kuturudisha kwenye nafasi yetu ya juu katika fahari na tamkini. Ndani yake kutakuwa na ubwana wa Shariah na mamlaka ni kwa Ummah, na mfumo wa utawala ndani yake unatokana na itikadi yake. Kwa hivyo, Waislamu wataishi ndani yake katika uhalisia unaoendana na fikra na hisia zao za Kiislamu.

Hivyo, Hizb ut Tahrir, iliyoasisiwa kwa msingi huu, inastahiki kukumbatiwa na Ummah. Bali ni wajibu kwa Ummah kuikumbatia na kutembea nayo, kwa sababu ndicho chama pekee kinachokumbatia fikra yake, kinachotambua njia yake, kinafahamu lengo lake, kinashikamana na njia ya Seera ya Mtume (saw) bila ya kujitenga nayo, na bila ya kuzuiwa kufikia lengo lake. Kinatoa wito kwa vyama katika mchakato wa kuasisi kwao vifuate mfano wake, katika msingi na madhumuni ya kazi yake, ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuaminiwa na Umma.

]وَمَن يَتَوَلَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْغَالِبُونَ]

“Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda” [Al-Ma’ida: 56]

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu