Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  13 Muharram 1444 Na: 1444 / 03
M.  Alhamisi, 11 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hukumu za Kidhalimu dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir ni Ugaidi na Ukandamizaji
(Imetafsiriwa)

Mahakama ya Rufaa ilikubali uamuzi wa Mahakama ya Usalama wa Dola, iliyowahukumu Mashababu wawili wa Hizb ut Tahrir kifungo cha miaka minne jela kila mmoja; kwa tuhuma za kuwa ndani ya Hizb ut Tahrir, na uchochezi dhidi ya utawala wa Jordan, na hiyo ilikuwa ni kinyume na usuli wa kupata machapisho na vitabu vya hizb majumbani mwao, ambapo kwa hilo tunasema:

Kuasisiwa kwa Hizb ut Tahrir kama chama cha kisiasa kinachofanya kazi ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu ni moja ya faradhi za Shari‘ah ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameziamrisha. Hakuna maana katika sheria za serikali ya Jordan, wala katika mahakama zake, wala katika mfumo mzima, kwani kimsingi zimejengwa juu ya batili. Zaidi ya hayo, Hizb ut Tahrir inalingania mapambano ya kisiasa na mvutano wa kifikra, na haifanyi vitendo vyovyote vya kimada kama vile kubeba silaha. Na ulinganizi wake wa kusimamisha Dola ya Khilafah hauhusu Jordan pekee, bali unajumuisha nchi zote za Kiislamu, na popote ilipo nusra ya Waislamu yaani kuregeshwa kwa mamlaka yao, dola ya Uislamu itakuwepo, hivyo kwa nini Jordan inajitoa pweke kuwa ulinganizi huu unahujumu mfumo wake wa utawala, licha ya kuwa hizb inafanya kazi mchana peupe katika nchi nyingi za Kiislamu kwa ulinganizi wake wa kisiasa, na tawala za nchi hizo hazioni kuwa inafanya kazi ya kuhujumu utawala wao?!

Hukumu hizi za vifungo gerezani za kidhalimu kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa sababu tu ya kuwa katika chama cha kisiasa kinacholingania Uislamu na utabikishaji wa hukumu zake, ni ugaidi unaofanywa na Mahakama ya Usalama wa Dola na kuwakandamiza wale wote wanaolingania kisiasa ili kuokoa Ummah kutokana na udhibiti wa kikoloni; kisiasa na kiuchumi, na kufichua na kudhihirisha uongo wa utawala katika kile unachodai kufanya marekebisho ya kisasa na ya kisiasa na kushajiisha uundaji wa vyama vya kisiasa. Inaashiria, kama tulivyosema katika kauli zilizopita, kuwa vyama ambavyo utawala huo unavitaka ni vyama vya aina yake, vinavyokubaliana na vitendo vyake vya kisiasa vilivyoidhalilisha nchi na wananchi na kuwafikisha chini kwa kuiweka nchi rehani kwa kafiri mkoloni ambaye alijifungulia nchi hii kwa kuifanya kama kambi ya kijeshi na akalifanya jeshi limtumikie yeye.

Enyi Waislamu:

Kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu na kuregesha dola ya Khilafah ni Fardh Kifayah (faradhi ya kutoshelezana) juu yenu nyote na sio juu ya Hizb ut Tahrir peke yake. Kazi hii inabakia kuwa ni faradhi shingoni mwenu mpaka isimamishwe, na hukumu hizi za kidhalimu na za kibaguzi juu ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir ni sehemu ya vita dhidi ya Uislamu na kuziba njia yake, na ni jaribio la kutia khofu katika nafsi zenu ili kujiepusha na jambo kubwa linalolazimishwa kwenu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tangu ilipoanzishwa mwaka 1953, Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kuulingania Ummah kuregesha Khilafah. Ni chama cha kisiasa ambacho kanuni yake ni Uislamu, na matendo yake yamejulikana kwa kila mtu, na kipo katika nchi arubaini, na hakitazuiwa na kukamatwa, kukandamizwa au hukumu za kidhulma za mahakimu waliouza akhera yao. Dunia ya watawala wao, tawala dhaifu na zenye khofu zinazoogopa kulingania kwa Mwenyezi Mungu na kutabikisha hukmu zake.

[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu