Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  3 Rajab 1444 Na: 1444 / 12
M.  Jumatano, 25 Januari 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara ya Netanyahu ni Shambulizi kwa Watu wa Jordan
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo mashirika rasmi na vyombo vya habari vya serikali vinakusanya maoni ya umma dhidi ya serikali ya Netanyahu yenye msimamo mkali - na serikali zote za kigaidi na itikadi kali - tangu kushinda uchaguzi, na uhamasishaji huu wa vyombo vya habari unaanza na kulaani uvamizi wa Ben Gvir wa Msikiti wa Al-Aqsa. Na kuitwa kwa balozi wa Kiyahudi, na kufuatiwa na polisi wa Kiyahudi kumzuia balozi wa Jordan kuzuru Msikiti wa Al-Aqsa, na Wizara ya Mambo ya Nje ya kukanusha hilo, na kisha Bunge likacheza dori yake katika kudhihirisha hasira na kufa ganzi kupitia baadhi ya wabung, na hatusahau uhamasishaji wa vyombo vya habari na makala katika magazeti rasmi, kama vile makala ya maoni [katika Kiarabu] “Wanasiasa: Serikali ya Israel yenye msimamo mkali imeliweka eneo hili kwenye shimo la volkano ambayo inaweza kulipuka wakati wowote.” Na kama vile hotuba za Wizara ya Wakfu za Kidini zenye kichwa, “Msikiti Uliobarikiwa wa Al-Aqsa ni haki kamili ya Muislamu.”

Kwa kuzingatia uhamasishaji huu wa kirongo, ziara ya mhalifu Netanyahu na ujumbe wake wa usalama, na mapokezi yake katika Ikulu ya Kifalme, yalikuwa ya dhati na ya kupendeza, kulingana na madai ya Waziri wa Mambo ya Kimkakati Ron Dermer, ambayo inaripotiwa ilisababisha ahadi ya Netanyahu wakati wa mkutano wake na Mfalme ili kuhifadhi hali halisi ilivyo katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Ziara na mapokezi ya Netanyahu nchini Jordan, Hashd na Rabat, licha ya yale tunayoyasikia na kuyaona kutoka kwa utawala huo, vyombo vyake na wasaidizi wake, na kwa kuzingatia kuendelea kwa uhalifu wa umbile la Kiyahudi, inaashiria yafuatayo:

1- Kwamba hakuna kurudi nyuma kwa utawala kutokana na uhusiano wake wa kimkakati na kutumia dori ya Jordan, ambayo ilipangwa na ukoloni wa Kimagharibi katika kuasisi umbile la Kiyahudi katika Ardhi Iliyobarikiwa, na kulipatia njia za uhai kupitia makubaliano baina ya kikanda ya kiuchumi, kisiasa na kiusalama, na kuhalalisha mahusiano kwa gharama ya Jordan, watu wake, ubwana wake, hadhi na heshima yake, bila kujali ni kiasi gani Mayahudi walifanya uovu na kupitiliza mipaka.

2- Nyuma ya mkutano huu, serikali hiyo inalenga kuthibitisha ulinzi wake juu ya Msikiti wa Al-Aqsa na kudumisha hali iliyopo ndani yake kwa kuzingatia wasiwasi na kutengwa kupitia kushindana na baadhi ya nchi jirani juu ya ulinzi huu, kwa badali ya utulivu na uratibu wa usalama katika maeneo yaliyokaliwa kimabavu. Mkutano huo ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Ndani na Usalama wa Ukingo wa Magharibi na Jerusalem katika umbile la Kiyahudi. Pete na Mkurugenzi wa Ujasusi wa Jordan.

3- Watu wa Jordan hawaoni uhusiano wowote pamoja na umbile la Kiyahudi isipokuwa ni udhalilifu na fedheha, na kwamba hawatanufaika na mapatano hayo yanayodaiwa kuwa ya amani nalo isipokuwa ufukara, kujisalimisha na kupotez nchi, na hawaoni suluhisho la kadhia ya Palestina zaidi ya kupigana na Mayahudi, yaani suluhisho la kijeshi, na wanaamini kuwa wana uwezo wa hilo kwa vifaa na idadi.

4- Katikati ya mashambulizi ya kisiasa na kidiplomasia duniani na maandamano makubwa ya Mayahudi wa ndani dhidi ya serikali ya Netanyahu na wanachama wake kutoka vyama vya kidini, ziara hii inapata afueni fulani na inaondoa shinikizo la kisiasa juu yake, sio kuipendelea Palestina na watu wake, lakini badala yake kutekeleza mipango ya kikoloni ya kuimaliza kadhia ya Palestina, na uratibu wa awali kabla ya mtanziko wa ziara ya waziri. Ziara ya Waziri ya Mambo ya Nje wa Marekani Blinken inayotarajiwa kwa umbile la Kiyahudi, ambayo lengo lake linatarajiwa kuwa kuweka shinikizo kwa serikali ya Netanyahu na kupiga breki juu ya kile kinachoweza kutishia maslahi na mipango ya Marekani kwa eneo hilo.

Enyi Watu wa Jordan: Tunathibitisha kwamba umbile la Kiyahudi ni adui kwenu, kwa watu wa Palestina, na kwa Waislamu wote, na linaendeleza uchokozi wake wa wazi dhidi ya watu wa Palestina na halijali sheria ya kimataifa, Suluhisho la dola mbili, suluhisho la dola moja, au hata watawala wenu, haijalishi wanalitambua kwa kiasi gani, wanalikubali, na kuridhiana na umbile hili. Hakuna suluhisho kwa hilo isipokuwa kulitokomeza, na hili litakuwa tu kwa kupitia majeshi ya Waislamu kwa nafasi zao kama Waislamu, kwani ni umbile dogo mno lau si kupewa njia za nguvu kutoka kwa wakoloni wa makafiri na tawala tegemezi katika nchi za Kiislamu.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu