Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  7 Rajab 1445 Na: 1445 / 08
M.  Ijumaa, 19 Januari 2024

Tanzia ya Mbebaji Da’wah Mtukufu
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inamuomboleza mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir:

Ustadh Omar Arif Al-Umari (Abu Rami)

Aliyefariki kwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Ijumaa, 19 Januari 2024, akiwa na umri wa miaka 70, ambayo aliitumia kama mbebaji Da’wah, akifanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida.

Abu Rami alijiunga na safu za Hizb katika miaka ya mwanzo ya ujana wake. Alikuwa mchapakazi na mvumilivu, akijitahidi katika imani yake kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) katika kuubeba ulinganizi huu, ambao ulimsababishia kuteswa na vyombo vya usalama. Hili halikumwondolea uthabiti wake au kutokana na kueneza haki na kubeba da’wah mpaka akaugua, matokeo yake akafariki.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amsamehe na ammiminie rehema nyingi, na amlaze peponi pamoja na Manabii, wakweli, na Mashahidi, na watu wema, na hao ni maswahaba wema. Pia tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aijaze familia yake kwa subira, uthabiti, na rambirambi njema.

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah:156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu