Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  9 Muharram 1446 Na: 1446 / 01
M.  Jumatatu, 15 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali nchini Jordan Inatumikia Malengo ya Kikoloni ya NATO: Jaribio Lililofanywa Upya la Kuitenga Jordan kutoka kwa Ummah Wake wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Wizara ya Mambo ya Nje na Wageni ya Jordan ilitangaza kuanzishwa kwa Afisi ya Mahusiano ya NATO (North Atlantic Treaty Organization) katika Ufalme huo, ambayo itachangia kuimarisha uhusiano wa ushirikiano na muungano huo. Wizara hiyo ilitoa taarifa ya pamoja na NATO kuhusu uamuzi wa kufungua afisi hiyo jijini Amman. Taarifa hiyo inasomeka: “Katika Mkutano wa NATO mnamo 2024 jijini Washington, washirika walipitisha mpango wa utekelezaji wa kuimarisha mbinu ya ushirika katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ili kuendana na maendeleo katika mazingira ya usalama wa kikanda na kimataifa.” Taarifa hiyo ilieleza zaidi kwamba dori ya afisi hiyo itakuwa “kuimarisha mazungumzo ya kisiasa na ushirikiano katika maeneo yenye maslahi kati ya NATO na Jordan.” Pia inalenga “kufikia maendeleo yanayotarajiwa katika kutekeleza programu na shughuli za ushirikiano, ambayo ni pamoja na kufanya makongamano, kozi, na programu za mafunzo katika nyanja kama vile uchambuzi wa kimkakati, mipango ya dharura, diplomasia ya umma na usalama wa mtandao.”

NATO ilianzishwa baada ya Vita Kuu vya Pili vya Dunia ambapo nchi 12 waanzilishi zilitia saini Mkataba wa NATO mwaka 1949 kwa lengo la kuzilinda nchi za Ulaya dhidi ya tishio la Muungano wa Kisovieti wakati huo. Muungano huo kisha ulianza kucheza dori muhimu na shughuli katika kushughulikia masuala mengi ya kimataifa ndani ya mkakati mpya unaolenga kutetea maslahi ya NATO nje ya eneo la kijiografia inayohusika. Baada ya Moscow kuvamia Ukraine mnamo 2022, Finland na Uswidi zilijiunga na muungano huo, na kuleta jumla ya wanachama wake hadi nchi 32.

NATO imeanzisha kile kinachoitwa ushirikiano na miungano na maelewano ya kambi, kama vile uelewa wa Mashariki ya Kati na Muungano wa Istanbul, pamoja na ushirikiano wa hali ya juu wa watu binafsi na baadhi ya nchi kama Jordan, ambayo inafanikisha maslahi ya kimkakati kwa muungano ambao umekuwa chombo cha kikoloni mikononi mwa Amerika. Shughuli yake katika kujenga ushirikiano wa usalama na kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi wa wanachama wake katika kanda inaonekana. Malengo ya muungano huu yamepanuka na kuwa chombo cha kimataifa mikononi mwa nchi za Magharibi, ikiongozwa na Amerika, ambayo inatawala nchi wanachama wake katika maamuzi yao na vita vyao dhidi ya wapinzani kama vile Urusi na China, na kuhamasisha nchi za kikanda kama washirika na marafiki wa muungano huo ili kufikia maslahi ya serikali hiyo inayoongoza duniani. Fahamu ya Kimkakati ya NATO ya 2022 inafafanua (ugaidi) kama tishio la moja kwa moja kwa muungano huo.

Kuhusiana na dori ya afisi ya NATO jijini Amman, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema “Jordan ni mshirika wa muda mrefu na anayethaminiwa sana wa NATO,” akibainisha kuwa Afisi ya Mahusiano ya NATO jijini Amman itainua ushirikiano wa nchi hizo kwa ngazi mpya. Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan ilisema kwamba “kuanzishwa kwa Afisi ya Uhusiano ya NATO jijini Amman kunatokana na karibu miongo mitatu ya uhusiano wa kina wa pande mbili.” Sam Warberg, Msemaji wa Kanda hii wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, alibainisha katika mahojiano na Shirika la Habari la Jordan kando ya Mkutano wa NATO kwamba nchi yake inathamini dori muhimu ya Ufalme huu katika utulivu wa jumla katika eneo hili. Amesisitiza kuwa, Mfalme Abdullah wa Pili sio tu kwamba ni rafiki wa Rais Joe Biden wa Marekani bali pia ana marafiki katika matawi yote ya serikali ya Marekani katika ngazi ya shirikisho na Congress.

Kwa kuzingatia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na maoni ya kisiasa hapo juu, ni muhimu kufafanua mambo yafuatayo:

 - Huku mauaji ya halaiki mjini Gaza yakiendelea na ukatili usio na kifani unaovunja nyoyo, utawala wa Jordan bila haya na kwa utiifu unaimarisha uhusiano wa kisiasa na kijeshi na maadui wa Jordan katika NATO. Muungano huu unashirikiana na umbile la Kiyahudi katika vita vyake vya kishenzi ambavyo vinaaibisha wanadamu.

- NATO ni muungano wa kikoloni unaochukia Uislamu na Waislamu. Imeshiriki katika vita dhidi ya Waislamu nchini Iraq, Afghanistan, Libya, Somalia na Yemen. Pia ni mshirika wa Mayahudi na umbile lao haramu. Hairuhusiwi kuichukulia NATO kama rafiki au mshirika, wala hairuhusiwi kuifungua nchi kwake na kushiriki katika ushirikiano wa kijeshi na kiusalama, haswa kutokana na kambi zake zilizotapakaa kote Jordan.

- Tangu kuanzishwa kwake na tangu kukabidhiwa utawala nchini Jordan na Uingereza, na kupitia ushirikiano wake wa kimkakati na Marekani na Ulaya, serikali ya Jordan imefanya kazi ya kuikomboa nchi hiyo kutoka kwa uhusiano wake wa kimaumbile na urithi wa kihistoria na kimfumo kama sehemu ya Ummah wa Kiislamu, na kuifanya kuwa chombo cha utumwa mikononi mwa dola za kikoloni kwa maslahi yao.

- Jordan haina haja ya kushirikiana na NATO, kwani haina maadui wa pamoja na NATO kuhalalisha ushirikiano wa kijeshi au kisiasa, isipokuwa kwa umbile la Kiyahudi. Majaribio ya serikali ya kuwatia hofu watu wa Jordan kwa uwepo wa maadui na uhalalishaji wake wa ushirikiano wa kimkakati na NATO na Amerika katika “vita dhidi ya ugaidi” ni udanganyifu tu. Ugaidi wa kweli unatokana na Marekani na maumbo yake, na hivi ni visingizio tu vya serikali kupata idhini ya kikoloni ili kuendelea kushikilia madaraka.

- Kufahamu uhalisia wa NATO na ushirikiano wa hali ya juu nayo kunahitaji kutambua kwamba shughuli za ushirikiano wa kijeshi katika ardhi za Waislamu, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kijeshi ya pamoja na mazoezi-kama vile mazoezi ya ‘Eager Lion’ nchini Jordan kwa miaka mingi, matumizi ya viwanja vya ndege na bandari, na ubadilishanaji wa taarifa za usalama wa mtandao—huupa muungano huu na nchi wanachama wake uzoefu wa kiutendaji unaotafsiri mauaji na umwagaji damu zaidi wa Waislamu katika eneo na katika ardhi zote za Waislamu. Huu ni uwezeshaji wa maadui wa Ummah, pamoja na kupunguza mamlaka ya dola. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]

wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini”. [An-Nisa:141].

Enyi Watu wa Jordan, enyi Waislamu!

Utawala wa Jordan unathibitisha kila siku kwamba sio wenu na nyinyi sio wao. Haukutegemeeni nyinyi kwa utawala wake; badala yake, unategemea dola za kikoloni za kikafiri za Magharibi. Haujali tena kutumia rasilimali zote za Jordan kwa ushirikiano na miungano yenye uadui kama NATO, au katika urafiki na maadui wabaya zaidi wa Ummah kama Amerika na Uingereza, pamoja na mashirika yao makuu ya kijeshi na kisiasa. Mkuu wa serikali hii anatumia likizo ndefu akijishughulisha na ushirikiano wa kiuchumi na wa kiusambazaji na miungano inayoufanya kuwa mfumo wa lazima katika vita vya kikoloni dhidi ya Uislamu na mradi wa kuregesha Khilafah ya Kiislamu.

Enyi Watu wetu nchini Jordan, enyi Waislamu!

Juhudi za utawala huu kutaka kukutieniu hofu... maandhari ya maangamizi munayoyaona huko Gaza na Palestina, mauaji ya halaiki yanayoendelea, na madai kwamba maadamu munabaki katika ushirikiano na ukimya kuhusiana na vitendo vya utawala huu—ima kwa makubaliano yake na umbile la Kiyahudi au miungano yake na Amerika na Ulaya – muko salama na amani, si chochote ila ni mbinu ya kiuoga, ya muda mfupi ya kutishia ambayo haikudanganyi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

[أَلَيْسَ اللهُ بِكَافٍ عَبْدَهُ وَيُخَوِّفُونَكَ بِالَّذِينَ مِن دُونِهِ وَمَن يُضْلِلِ اللهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ]

Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa.” [Az-Zumar:36]. Je, hamuoni kile ambacho kikundi cha wapiganaji mjini Gaza kinafanya mbele ya vita vya kimataifa dhidi yao na subira na uthabiti wa watu wa Gaza dhidi ya mashini ya vita ya Marekani na Mayahudi? Nini kingetokea lau majeshi yetu yangewanusuru ndugu zetu mjini Gaza, ambao wamekuwa wakiomba msaada wenu kwa miezi kumi? Je, munafikiri umbile la Kiyahudi litaendelea kuwepo, au kwamba Marekani itatoa kafara askari wake kwa ajili yake? Au kwamba tawala vibaraka katika nchi za Waislamu zitabaki kuwa kandamizi juu ya Umma bila kufungasha virago vyao kukimbia?

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ]

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud:113].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu