Ijumaa, 08 Sha'aban 1446 | 2025/02/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  29 Rajab 1446 Na: 1446 / 12
M.  Jumatano, 29 Januari 2025

Hatari ya Uhamisho Inayotafutwa na Trump na Umbile la Kiyahudi Inalazimu Hatua Kali katika Kuamiliana nao kama Maadui
(Imetafsiriwa)

Utawala wa Jordan na kundi la watu wake wakati wote wa vita vya Kiyahudi dhidi ya Gaza walikuwa na bado wangali wanatetea kutowanusuru watu wa Gaza kijeshi, na angalau sio kufutilia mbali makubaliano ya udhalilishaji na aibu na umbile la Kiyahudi, lakini kwa busara na hekima na ujanja wa kisiasa hii ni hatua na udhoofishaji wa amani, usalama na chemchemi ya utulivu ambayo Jordan inaishi ndani yake. Mfalme alifikiri kwamba Uingereza ilimuamuru kurukuu na kujibu ajenda ya Amerika ambayo imelitawala eneo hilo tangu aingie madarakani, kufuatia mbinu ya baba yake, na kile ilichomuagiza kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya ulinzi nayo mwaka 2021 ambayo yanahujumu kila maana ya ubwana wa nchi yoyote, na kuifungua nchi kwa ujumla kwa kambi za Amerika pekee na viwanda na vikosi vyake, na kufanya miondoko ya “Simba mwenye Hamu” kwa miaka mingi chini ya jina la vita dhidi ya (ugaidi), kwa hivyo alifichua kwa njia isiyo wazi uhalalishaji wake wa mahusiano haya na maelewano na Amerika (rafiki) katika hotuba yake katika Baraza la Wawakilishi: “Sisi ni dola yenye kitambulisho thabiti, ambacho haihatarishi mustakabali wake na inahifadhi urithi wake wa Hashimiya,” na ni wazi kwamba tukio hapa ni misimamo ambayo anadhani itadhoofisha utawala wa familia ya Hashimiya.

Utawala wa Jordan pia ulifikiri kwamba uhusiano wake wa muda mrefu na umbile la Kiyahudi na viongozi wake, na uwezeshaji wao, hasa wakati wa vita vya kuiangamiza Gaza, na mahusiano yake tata na Marekani na taasisi zake za ufanyaji maamuzi, kutoka kwa Republican na Democrats, kama vile Congress, Pentagon, Usalama wa Taifa, na makampuni makubwa ya kiuchumi, na kuwapa fursa ya kuwekeza nchini Jordan yenye thamani ya mabilioni ya dolari, walidhani kwamba yote haya yangeokoa utawala wake kutokana na mabadiliko na ubadilishwaji wa sura ya matamanio ya Mayahudi, ambayo yanaungwa mkono na Trump, kwa hivyo anatoa matamshi yake ya kijambazi kuhusiana na mipango yake ya siasa na maslahi ya Amerika ambayo anataka kuyafikia Mashariki ya Kati.

Hapa anaamuru kusitishwa kwa msaada wa kila mwaka kwa Jordan, na kusitishwa mara moja kwa miradi yote ambayo Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) linachangia. Kabla ya hapo, alikuwa amemuondoa Balozi wa Marekani, Yael Lambert, na kumtaka Mfalme katika simu ya pongezi kwa kuapishwa kwake, kuwahamisha baadhi ya watu wa Gaza hadi Jordan. Aliregea katika mdundo wa Mpango wa Karne aliouzindua wakati wa muhula wake wa kwanza madarakani, na kinachomaanishwa hapa sio tu Gaza, bali pia vita vya sasa vya watu waliokimbia makaazi yao katika Ukingo wa Magharibi ambao umbile la Kiyahudi linataka kuliunganisha nalo, ili hadithi ya kuhama makaazi iendelea kutanda juu ya mazingira ya kuimaliza kadhia ya Palestina na inabadilikabadilika kati ya hali ya utulivu na kupamba moto kwa kasi kwa mujibu wa kile kinachohitajika na mazingira ya watu wenye kukataa na yanayotakiwa na harakati zake, na makubaliano ya hatua kwa hatua kwa siri na dhahiri kwa serikali, na kulingana na ukubwa wa usaliti wa Amerika au ulegevu wake, na kulingana na kiwango cha majibu na vitisho vyake kwa uthabiti wa serikali yake.

Ingawa utawala wa Jordan na msafara wake wa waandishi, vyama na wawakilishi walikataa hadharani kuhamishwa kwa Wapalestina kwenda Jordan kwa msingi kwamba kunadhuru suluhisho la kadhia yao na uanzishwaji wa dola kwa ajili yao, na pia inadhuru maslahi ya Jordan kama nchi badali na wanaona kuwa ni mstari mwekundu zaidi ya ambao vita vinaruhusiwa, kukataliwa huku hakuondoi hatari mpya kwa Jordan na Palestina, kwa sababu kunatokana na msingi mbovu na dhaifu, kwa kudhani serikali ina ukweli katika kukataa kwake  uhamishaji, kutokana na mambo mawili:

La kwanza: Bado ingali inaendelea na suluhisho la dola mbili, ambalo limekufa kiuhalisia na limeharamishwa na sheria ya Kiislamu, na ambalo linakataliwa na umbile la Kiyahudi katika wigo wake wote, na ghilba ya uhalisia wa dola ya Palestina ambayo wao wanaizungumzia kuhusu na marais wa Marekani, huku Trump akieleza kusikitishwa kwake na umbile la Kiyahudi kwamba ni dogo sana na linahitaji upanuzi, huku wakitafuta kunyakua Ukingo wa Magharibi kwa misingi kwamba ‘Yudea na Samaria’ na sehemu ya umbile lao, pamoja na matamanio yao katika sehemu nyingine za Jordan, kama Smotrich alivyofichua.

La pili: Uhalisia wa kukataa uhamishaji makaazi yao unapingana na utawala wa Jordan na wale wanaoafikiana na mkabala wake katika uzito wake wa kivitendo wa kukabiliana na njama hii ya Mayahudi na Marekani dhidi ya Jordan na Palestina. Makubaliano ya kudhalilisha ya Wadi Araba bado yapo, na kushindwa kwa utawala huu kuwaunga mkono kijeshi watu wa Gaza wakati wanahitajia sana, na uwepo wa kambi za Marekani na makubaliano ya pamoja ya ulinzi pamoja nao, na kuegemea Jordan kwa misaada ya Marekani katika utekelezaji wake katika nakisi yake inayoongezeka, haimaanishi, kwa mtazamo wa misimamo hii, hatua yoyote ya kivitendo, ya kiume na ya kiungwana ili kukomesha kiburi cha umbile la Kiyahudi na kiburi na uvivu wa Trump.

Kinachoitwa diplomasia na kukimbilia mfumo na sheria za kimataifa ni taratibu tasa na zilizofilisika ambazo hazizuii mkono wa mgusaji. Ndio jambo kubwa zaidi ambalo utawala unaweza au unataka na linaonyeshwa na waziri wake wa mambo ya nje wakati wowote mashambulizi ya Mayahudi na Amerika yanapozidi, kwa kulia na kulalamikia. Ni udanganyifu usiorudisha haki, wala hauondoi hatari, na ni kunyenyekea na udhalilifu. Kadhalika, kukimbilia makubaliano na mshikamano wa pamoja wa Waarabu katika kile kinachoitwa kushadidisha juhudi za kukabiliana na changamoto za kuhamishwa makaazi yao na kukataa kuasisiwa dola ya Palestina ni udanganyifu mkubwa na mazungumzo tu kwa matumizi ya wananchi. Tawala hizi za Kiarabu ziko sawia katika utegemezi wao kwa Wamagharibi makafiri, na hazikubaliani baina yao kwa wema kwa sababu utiifu wao kwa Wakoloni wa Magharibi ni mwingi, na shahidi bora zaidi ni kujisalimisha kwa Ibn Salman katika kulipa dolari bilioni 600 za fedha za Waislamu ili kuwekeza nchini Marekani.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tutabakia kuwa kiongozi asiyewadanganya watu wake, na wale wanaotupinga hawatudhuru chochote: Tunabainisha kuwa suluhisho la kweli, la kivitendo na la halali, linalomridhisha Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, Waislamu, watu wa Jordan, na watu wa Palestina ambao wameweka mifano ya ajabu sana katika kushikamana kwao na ardhi yao na nyumba zilizoharibiwa, ndilo suluhisho linalowezekana leo na la gharama ndogo zaidi kwa Umma. Gharama yake itakuwa ya juu kama litacheleweshwa, na linawakilishwa kwa dhati katika kutabanni hali ya kivita na umbile la Kiyahudi na kile kinachohitaji katika suala la hatua za kiutendaji kama vile kufuta Mkataba wa Wadi Araba na mikataba yote iliyohitimishwa nalo. Majeshi yetu yako katika viwango vya juu zaidi vya utayari wa mapigano, pamoja na usaidizi mkubwa wa watu wengi katika kuchukua hatua kali kama hiyo.

Suluhu zito na kali linahitaji kukata mahusiano ya kijeshi, kiuchumi, kiusalama, kijeshi na kisiasa na Marekani, kufuta makubaliano ya ulinzi wa pande zote na Marekani, na kufunga kambi zake, kwani ni adui mlafi na muungaji mkono wa umbile la Kiyahudi, na maslahi yake yanagongana na maslahi ya Umma wa Kiislamu. Serikali hauruhusiwi kuzungumza kuhusu ubwana juu ya ardhi yake na kuichukulia Amerika kama nchi rafiki, wakati inaituhumu kwa usaidizi na kutishia kwa nchi badali na uhamisho, isipokuwa izingatie kutotekeleza maagizo ya Trump kuwa ni njia inayoiogopa, na hivyo kupata ghadhabu ya Umma, ambao umekuwa tayari na kusadikishwa juu ya njia ya hatma yake isiyoepukika kwa kuliondoa umbile la Kiyahudi na kufukuza nguvu zote za ukafiri na ukoloni, na kuuunganisha katika dola ya Kiislamu ambayo utiifu wake ni kwa Mwenyezi Mungu pekee. Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko Marekani, na Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko umbile la Kiyahudi.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma'idah 5:51]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu