Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  30 Jumada II 1442 Na: 1442/08
M.  Ijumaa, 12 Februari 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Tokea Kuvunjwa kwa Khilafah, Kubomolewa kwa Majumba ya Ibada Yamekuwa ni Maafa kwa Waislamu Wote.

Kwa hoja ya ukarabati wa Reli ya Nairobi hadi Kisumu, Shirika la  Reli la Kenya lilibomoa msikiti wa Jami’a  na majumba ya wakaazi wa eneo la Kibos kwenye Jimbo la Kisumu hali iliowaacha familia nyingi bila makao. Msikiti uliojengwa yapata miaka 83 iliyopitia, ni mojawapo ya misikiti mikongwe na kituo muhimu cha ibada mjini Kisumu.

Sisi, Hizb ut-Tahrir / Kenya tunakashifu vikali kitendo hiki cha kidhulma na cha kihuni kilichofanywa kinyume na amri ya mahkama iliyotaka kutobomelewa msikiti huo na maeneo ya makazi. Ni dhahiri shahiri kwamba serikali imefeli kujenga mahusiano mema na umma hususan Waislamu. Serikali imeshindwa kudhaminia utunzi wa mali na majumba ya Ibada.

Kitendo hiki dhidi ya Uislamu kwa hakika kinachukiza Waislamu na hupelekea hasira za Mwenyezi Mungu.

((وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهاَ))

Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia Misikiti ya Mwenyezi Mungu kwamba humo lisitajwe jina lake na akajitahidi kuiharibu. [Al-Baqara: 114]

Kubomolewa kwa misikiti ni miongoni mwa maafa makubwa kwa umma mzima wa Kiislamu wala sio kwa jamii tu ya Kiislamu ya Kinubi. Hii ni kwa kuwa sisi ni umma mmoja na kwamba nafasi ya misikiti kwetu ni kubwa mno kwani ni majumba ya Mwenyezi Mungu (swt). Kitendo hiki cha kuchukiza kwa hakika kinaonesha wazi uadui dhidi ya Waislamu unaotokamana na uadui wa kimataifa ikizingatiwa kuwa vitendo kama hivi vimekithiri huko china ambako utawala wake unaochukia Uislamu umekuwa ukivunja misikiti. Tusije tukasahau pia kwamba msikiti mtukufu wa Al-Qudus bado unakaliwa na Mayahudi ambao usiku na mchana huchimba mahandaki ndani yake.

Miaka mia moja ya ukumbusho wa kuvunjwa kwa Khilafah, Waislamu wamekosa mlinzi halisi wa matukufu yao yakiwemo misikiti. Ni miaka mia moja ya vurugu, mashambulizi na ubomoaji. Tukio hili lazima lichachawize Waislamu kuzidisha juhudi zao katika kuungana na wale wanaofanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah Raashidah chini ya mfumo wa utume katika mojawapo ya nchi za Kiislamu. Ni serikali ya Khilafah ndio ambayo itahifadhi mali ya watu, maisha na nyumba za ibada kwa Waislamu na Wasokuwa Waislamu ulimwengu mzima.

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu