Afisi ya Habari
Kenya
H. 21 Muharram 1443 | Na: 1443/02 H |
M. Jumapili, 29 Agosti 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mateso ya Waislamu ya Muda Mrefu nchini Nigeria Yatakoma kwa Kuisimamisha tena Khilafah kwa Mfumo wa Utume
Siku ya Ijumaa tarehe 13 Agosti,2021 zaidi ya Waislamu 22 waliuwawa na wengine 14 kujeruhiwa katika shambulizi jipya katika mji wa Jos katikati ya Nigeria. Kulingana na taarifa ya polisi, genge la washambuliaji wanaoshukiwa kuwa na kundi la Irigwe lilo na wafuasi wengi wa Kikristo liliweza kushambulia msafara wa Waislamu waliokuwa wameabiri mabasi matano wakiwa wametoka kwenye sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu zilizofanyika jimbo jirani la Bauchi. Kulingana na duru nyengine za habari, kundi hilo lilitumia mapanga, visu na mawe.
Mauaji haya ya kutisha ya Waislamu kwa mara nyengine tena yamefichua namna Nigeria inavyokumbana na changamoto kubwa ya usalama iliozidisha na kutanua fikra za ubaguzi wa maeneo. Viongozi wa Kiserikali na Usalama wanaishia tu kukashifu hatua ambayo kamwe haitosaidia kuficha kufeli kwa serikali katika kuhakikishia raia wake usalama na na amani wala kufeli kwake katika kuwatia mbaroni washambulizi.
Mji wa Jos na maeneo mengine ya kati na kaskazini mwa Nigeria yamekuwa ni maeneo yanayoshuhudia mirindimo ya mapigano makubwa katika vijana wa Kiislamu na wakikristo mara kwa mara. Mwezi Septemba 2001 mapigano katika ya Wakristo na Waislamu katika mji huu wa Jos yalipelekea mauaji ya watu 913 hii ni kulingana na shirika la Human Rights Watch. Chanzo hasa cha ghasia hizi ni kutokana siasa, na ugavi mdogo wa rasilimali na suala la ufisadi serakalini yote haya yakiwa yamechochea pakubwa Nigeria kuwa na umasikini. Isitoshe, kuna sera za kiubaguzi ndani ya majimbo hadi kwenye serikali kuu sera za kuwagawanya raia katika misingi ya kikabila kiasi cha kuchukuliwa kuwa baadhi ya makabila sio mafukara katika maeneo wanayoishi.
Mateso yanayopitiwa na Waislamu nchini Nigeria yamekuwa ni ya kila mara na yamekuwa ya kihama kutoka utawala mmoja kwa mwengine. Katika kipindi cha utawala wa Good Luck Jonathan, alitumia mbinu za kikatili za kujaribu kutokomeza matakwa ya Waislamu. Naye Muhamad Buhari, akachukua mkakati mwengine wa kiusalama kwa kuondoa wanajeshi katika maeneo ya mashambani yaliyofanya maeneo mengine kama mji huu wa Jos yawe ni rahisi kukumbwa na mashambulizi na uvamizi wa wanamgambo na magenge ya mauaji. Na kwa kisingizio cha kupambana na Boko Haram, serikali ya Nigeria ikidai kuwa inalinda maisha ya raia lakini wakati huohuo inajizatiti katika kuendeleza unyanyasaji wake dhidi ya Waislamu. Tukiangalia kwa kina zaidi, tutakuta kwamba suala la utovu wa usalama na mapigano ya ndani kwa ndani nchini Nigeria yametengezwa na mataifa ya Kimagharibi hususan Amerika na Uingereza ili waweze kupata mwanya kuingia ndani yake kwa lengo si jengine ila kupora utajiri wa mafuta ya Nigeria. Uingereza kwa kutaka kupora utajiri wa Nigeria ikapandikiza na kuweka mizizi ya migawanyiko ya kikabila kimakusudi. Hata hivyo, licha ya miradi yote hii miovu, Jamii ya Kiislamu imekuwa ikijipinda katika kuhifadhi utambulisho wake wa Kiislamu.
Tunasema, ni jambo linalouma kuona mauaji haya ya kinyama dhidi ya Waislamu yakifanywa katika taifa ambalo Uislamu ulikuwa na athari kubwa. Uislamu una tarekh kubwa Nigeria na ulienea pakubwa na tunaendelea kuwa na imani kwamba kwa kuisimamisha Khilafah chini ya mfumo wa Utume maafa haya ya muda mrefu ya Waislamu na athari ya mataifa ya kimagharibi yatasita.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |