Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Rabi' I 1445 Na: 1445/04 H
M.  Jumapili, 08 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wala Msifanye Uvivu Kuwafuatia Maadui kama Mumepata Maumivu Basi Wao Pia Watapata. Na Nyinyi Mnatumai Kwa Mwenyezi Mungu Yale Wasiyoyatumainia

(Imetafsiriwa)

Jumamosi tarehe saba Oktoba mwaka 2023, mashujaa wa ukanda wa Gaza walivuka mipaka ya umbile la Kiyahudi. Walishambulia ngome za adui na hivyo kufanya nyuso zao kuwa nyeusi. Shambulizi hili dhidi ya Jeshi la Kiyahudi limekashifiwa kote duniani ikiwemo Afrika.  Mashambulizi haya yaliyofanya na Wapalestina, Kenya kwa upande wake ikachukua maamuzi thabiti ya kusimama pamoja na umbile la Kizayuni. Katika taarifa yake Jumamosi, Nairobi ilishikilia kuwa inasimama pamoja na umbile la Kiyahudi na hivyo kulaani mashambulizi dhidi yake.   

Hizb ut Tahrir Kenya tungependa kufafanua yafuatayo:-

Ni muhimu kwa Kenya na Afrika kutambua kuwa utawala wa Kizayuni una rekodi ndefu ya matendo ya kigaidi dhidi ya Waislamu huko Gaza. Shirika la kijasusi la Kiyahudi Mossad linashirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Kenya katika mauaji ya Waislamu yanayotekelezwa na vyombo vya usalama kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Ni mamlaka hiyo hiyo ya Kizayuni iliyofanya ugaidi wa kutisha duniani pale ilipowaondoa Wapalestina wasio na hatia kutoka katika ardhi yao ya asili na kuteketeza moto vitongoji vyao! Ingawa kitendo hiki cha kikatili hakikuwahi kuitwa kitendo cha kigaidi!

Viongozi wa Ulimwengu wanajulikana kwa tabia ya kukashifu kibaguzi baadhi ya matendo huku wakiunga mkono matukio yayo hayo japo umma wa Kiislamu na watu wote duniani kattu hawatasahau kamwe vitendo vya kinyama vilivyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Vita vya Al-Karameh (Vita vya Machafuko) mnamo 1968. Je, unyama huu  haukuwa ukiukaji wa kile kinachoitwa mkataba wa amani?

Mauaji ya halaiki yafanywayo peupe pepepe na umbile la Kiyahudi, Marekani na Ulaya kupitia watawala vibaraka wao kamwe hayajawahi kuchemsha nyoyo wala mishipa ya majeshi ya Kiislamu ili kuhamasika dhidi ya umbile hili nyakuzi! Hakika tunajua kuwa wakati wa Ushindi (Nusrah) umekaribia sana In Shaa Allah. Tuna imani kwamba kitendo adhimu cha kuulingania Uislamu kama mfumo mbadala kwa mfumo wa Kirasilimali uliofeli ndio suluhisho pekee tena kwa majanga na maafa ulimwenguni.

Yaliyotokea katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni kishajiisho kwa kile kinachowasubiria maadui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na waumini mikononi mwa vijana wenye ari ya kikweli. Hakika hii ni siku ya ajabu ambayo imeonyesha wazi udhaifu na uoga wa umbile la Kiyahudi na jeshi lake!

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّآ أَذًى ۖ وَإِن يُقَٰتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ ٱلْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ

Hawakudhuruni hao maadui zenu (Mayahudi) ila udhia (mdogo). Na kama watapigana nanyi basi watawapa migongo kisha hawatonusuriwa. [Aali-Imran: 111]

Majeshi ya Waislamu na Watu wenye nguvu mna jukumu kubwa la kuwasaidia ndugu zenu wakaazi wa Ardhi Iliyobarikiwa. Watawala wa Kiislamu wamelaani shambulizi hili na vile vile wataunga mkono mashambulizi ya jeshi la Mayahudi dhidi ya kina mama na kina baba wazee. Simameni muwanusuru ndugu zenu wanapobisha mlango ili waingie ndani kupitia mlangoni. Ni Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ndio pekee itakayohamasisha kiujasiri jeshi la Waislamu dhidi ya jeshi la umbile la Kiyahudi hivyo kukomesha kiburi, jeuri na ubaguzi wa Mayahudi.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu