Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  29 Jumada II 1445 Na: 1445/09 H
M.  Alhamisi, 11 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sera ya Afya bila Afya

(Imetafsiriwa)

Wizara ya Afya imefichua kuwa Ksh.20 bilioni zimepotea kupitia mpango wa Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) kupitia madai fidia za kirongo na upasuaji ghushi, miongoni mwa shughuli nyingine za ulaghai zinazofanywa na vituo vya afya. Waziri wa Afya Wafula Nakhumicha, alifichua kashfa hiyo iliyoathiri vituo vya afya, akisema kuwa kati ya hospitali 67 zilizokaguliwa nchini, 27 zimesimamishwa kazi kutokana na hasara ya Ksh.171 milioni kupitia mpango wa NHIF.

Tungependa kutaja yafuatayo:

Ni dhulma kubwa kwa viongozi wa serikali waliopewa dhamana ya kuwakilisha maslahi ya umma, badala ya kufanya kazi ya kuboresha hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida wanashindana vikali juu ya ubadhirifu wa rasilimali za umma.

Sekta ya afya mithili ya sekta yoyote ya umma katika serikali zote za kibepari haijasimamiwa vya kutosha, kwani nia pekee ya ufanisi na utendaji mzuri ni faida. Kwa kuzingatia hili, afya kimsingi sio kipaumbele katika uongozi wowote wa kibepari. Kwa hivyo sio lengo la serikali hizi za kibepari kutunza ustawi bali ule tu wa kundi fulani la watu wenye ushawishi na ukwasi pekee. Zaidi ya hayo, sera ya bima ya afya yenyewe ni dhihirisho wazi la Serikali kujitenga na kushughulikia masuala ya umma ikiwa ni pamoja na afya. Chini ya sera hii mbovu, mwananchi wa kawaida analazimika kulipia huduma za afya kabla ya kuugua.

Kwa kuwa Kenya inafuata mfumo mbovu wa Kibepari ambao umejaa hamu kubwa ya kujilimbikiza mali kwa njia zote basi "vita dhidi ya ufisadi" kamwe havitashindwa. Mfumo huu umegubikwa na kukithiri katika ushibishaji wa mali pasina na uroho kuwa ndio kigezo pekee cha maisha huchochea jamii hasa viongozi wa serikali kuwa na ari ya kujilimbikizia mali kwa njia za kifisadi.

Uislamu umeiweka sekta ya matibabu kama moja ya mahitaji ya kimsingi kwa umma ambayo yanahitaji umakini mkubwa. Uislamu hauoni huduma za afya au huduma yoyote ya umma kama upendeleo au fadhla bali kama kipaumbele ambacho serikali inawajibika kuzitoa kwa raia wake wote.

Ama kuhusu ufisadi unaofanywa na maafisa wa serikali, jambo hili linaweza tu kushughulikiwa ipasavyo kupitia Dola ya Khilafah ambapo raisi wa dola (Khalifah) anatekeleza sheria za Mwenyezi Mungu (Shariah). Sheria zinazoamua jinsi Serikali inavyokusanya na kutumia rasilimali zake. Aidha Uislamu umeamuru kwamba mali ya afisa wa serikali inatakiwa kubainishwa kabla na baada ya kushika wadhifa na baada ya kuuacha. Ongezeko lolote lisilo la kawaida la utajiri wa mtawala au afisa yeyote wa serikali huchukuliwa na kuingizwa kwenye hazina ya dola (Baitul Mal).

Tunasema ni Khilafah pekee kwa njia ya Utume ndiyo itamaliza kero la ufisadi nchini Kenya na ulimwengu kwa jumla.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu