Ijumaa, 01 Sha'aban 1446 | 2025/01/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  27 Rajab 1446 Na: H 1446/06
M.  Jumatatu, 27 Januari 2025

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut Tahrir / Kenya Iliandaa Msururu wa Amali katika Kumbukumbu ya Miaka 104 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 104 ya kuondolewa kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir/Kenya ilifanya kampeni nchi nzima katika mwezi mtukufu wa Rajab 1446 H. Kampeni hii iliyoanza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab ilihusisha shughuli mbali mbali; Darsa, Semina na Visimamo. Hii ilikuwa ni kuukumbusha Ummah kuhusu hali yake ya kusikitisha ambayo umekuwa ukikabiliana nayo tangu kuondolewa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M.

Wakiwa na idadi ya watu karibu bilioni 3, Waislamu wanafanana na povu la baharini kwa sababu ya kutokuwepo kwa Khilafah kama mlinzi na ngao yake! Ummah umepoteza utu, heshima na mlinzi wake. Umbile halifu la Kiyahudi linaloungwa mkono na tawala za Magharibi zenye kiu ya umwagaji damu limefanya mauaji ya halaiki kwa watu wa Gaza. Na nchini Syria, mapinduzi yaliyobarikiwa yamefanikiwa kumng’oa kiongozi mbaya lakini nchi za Magharibi zinafanya kazi kuregesha uongozi mwengine wa kiliberali na wa kisekula.

Kuvunjwa kwa Khilafah ni tukio la giza na la kuhuzunisha zaidi ambalo limeuacha Ummah kutawanywa na mradi wa kikoloni wa Sykes-Picot badala ya umoja wao, na ardhi zao zikabadilishwa na ukoloni. Damu ya Waislamu iliyomwagwa huko Ash-Sham ngome ya Uislamu kamwe haijachemsha mishipa ya Majeshi ya Waislamu kuwanusuru Mujahidina. Wale wanaoitwa viongozi kwa upande wao wamenyamaza kimya cha wafu!

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu