Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  3 Rajab 1437 Na: 1437/09 H
M.  Jumapili, 10 Aprili 2016

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni Nani Aliye Mbora katika Hukmu Kando na Mwenyezi Mungu kwa Watu Wenye Yakini?

Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) hatimaye imewaondolea mashtaka yote ya jinai dhidi ya Naibu Rais wa Kenya, William Samoe Ruto na mtangazaji wa redio Joshua arap Sang. Wawili hao ni miongoni mwa wengine sita ambao mwanzoni walituhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu uliomjumuisha Rais Uhuru Kenyatta, ambaye mashtaka yake hatimaye yaliondolewa mapema. Uamuzi huu ulipokewa na kukubaliwa kwa pamoja kutoka kwa takribani wanasiasa wote nchini Kenya huku waathiriwa wa mauaji ya halaiki ya uchaguzi mkuu wa 2007 wakipigwa na butwaa kwa uamuzi huu. Kutokana na haya, Chama cha Kisiasa cha Kiislamu Hizb ut Tahrir Kenya kingependa kwa ikhlasi kutaja yafuatayo:

Azimio hili, kwa hakika limeonyesha kuwa ICC bali mahakama zote ambazo ziko kwa sasa, hazina nguvu katika kufuatilia kesi dhidi ya mauaji ya halaiki na dhulma nyinginezo. Dalili ya hili inaweza kuthibitishwa waziwazi kupitia hatua dhaifu iliyochukuliwa na ICC ya kuyategemea mashirika ya haki za kibinadamu katika ukusanyaji wa taarifa muhimu! Wanaharakati wa mashirika haya wanaweza kushawishiwa kupitia shinikizo kutoka kwa wanasiasa.

Inaonekana dhahiri kuwa ICC sio mahakama imara ya kutafuta haki; bali ni chombo cha kisiasa ambacho hutumiwa kufikia malengo ya kisiasa. Katika bara la Afrika ikiwemo Kenya, ICC hutumiwa na Wamagharibi, ambao ndio wafadhili wake wakuu ili kudumisha ukoloni mambo leo katika juhudi za kumdhibiti hasimu wake wa kikoloni – Marekani. Mabepari wa Kimagharibi ndio ambao huiamulia ICC ni kiongozi yupi wa kumpeleka katika mahakama hiyo na yupi wa kumuachilia huru, maadamu kwa kufanya hivyo hatimaye itadhamini kiu yao ya kumakinisha na kudumisha udhibiti wake imara wa kisiasa kwa watawala wa nchi zinazo endelea, kutumia mbinu ovu kama mauaji ya kisiasa ili kufikia malengo yao. Historia inafichua waziwazi namna gani viongozi mbali mbali wa kisiasa kutoka nchi tofauti walivyo malizika kwa mauaji maovu ya kisiasa.   

Hakika, mauaji yanayotokea baada ya chaguzi nyingi za kidemokrasia, yana dhihirisha waziwazi sifa kuu ya wanasiasa wa kidemokrasia kuwa hawajali kumwaga damu au kuua watu wasio na hatia ili kubakisha nyadhifa zao za kisiasa. Idadi kadhaa ya maisha ya wasio na hatia yamekuwa yakipotea wakati wa chaguzi hizi hapa barani Afrika. Katika ulimwengu wa Waislamu, dola za Kimagharibi zimekuwa zikianzisha mauaji ya halaiki ya kuendelea chini ya kisingizio cha kulinda Demokrasia.

Wakati sasa umewadia kwa mujtama wa Kenya kuhisi hatari inayokuja inayoletwa na mfumo wa Kimagharibi wa kirasilimali na nidhamu yake ya utawala ya Demokrasia na namna mahakama zao zinavyocheza na maisha ya watu na hata kuwahatarisha. Ili kukomesha dhulma zote hizi ovu, njia pekee mbele ni kuachana kikamilifu na mfumo huu muovu na kufuata mfumo mbadala uliobora ambao si mwengine ila ni Uislamu huku mahakama zake zikiwa zimejaa uadilifu bila ya kujali ima mhalifu ni tajiri, tabaka lao la kijamii au ufahari. Yote haya yatatekelezwa chini ya nidhamu ya utawala ya Khilafah kwa njia ya Utume. Ni nani mbora wa hukmu kando na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa watu wenye yakini?  

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu