Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  14 Jumada II 1436 Na: 1436/11 H
M.  Ijumaa, 03 Aprili 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Shambulizi la Garissa Lisitumiwe Kueneza Ajenda ya Kikoloni ya Chuki Dhidi ya Uislamu

Chama cha Kisiasa cha Kiislamu Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki kimeshtushwa na mauaji ya kinyama ya wanafunzi 147 mjini Garissa, eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Shambulizi hilo limewahuzunisha wengi nchini Kenya hususan ikizingatiwa kuwa ndilo la kinyama zaidi kuliko yote yaliyotokea katika miaka ya hivi karibuni ikiwemo uvamizi wa Westgate, na mauaji ya Mpeketoni. Huku kukishuhudiwa umwagikaji damu isiyokuwa na hatia, tungependa kutaja yafuatayo:

(1) Kwanza vyombo vya usalama ni lazima vibebe mzigo mkubwa zaidi wa lawama, hii ni kwa sababu licha ya kudai kufanya mabadiliko makubwa ikiwemo kuondolewa kwa uongozi wake wa juu, bado mauaji kama haya yangali yanaendelea. Ni wajibu juu ya serikali kudhamini usalama wa raia wake ima ni madukani, shuleni na mabarabarani. Bado tunapenda kuonya vikali kuwa tukio hili lisitumiwe kama chombo cha kueneza chuki miongoni mwa wasiokuwa Waislamu dhidi ya Waislamu au kabila fulani dhidi ya jingine. 

(2) Ama Al Shabaab kudai kuhusika, hili halina umuhimu. La muhimu zaidi ni matokeo ya shambulizi hili la kinyama. Tumeona punde tu baada ya mashambulizi kama haya kutokea, namna usalama wa serikali unavyo wanyanyasa Waislamu kwa ukatili usiosemeka kwa kisingizio cha kupambana na ule unaoitwa msimamo mkali au ugaidi kwa jumla. Yote haya, nchi za Kimagharibi huanzisha shambulizi la kimakusudi katika jaribio la kuendeleza ajenda yao ya kikoloni katika nchi kadha wa kadha zinazo endelea. Dola hizi za kikoloni, hupatiliza fursa ya matukio haya, kama njia ya kufikia malengo yao na ajenda zao za kikoloni, hususan, ukitilia maanani kugunduliwa kwa madini na mafuta eneo lote la Afrika Mashariki. Si ajabu serikali ya Uingereza ilitabiri kutokea kwake na Amerika ikaionya serikali ya Uganda juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi. Kwa ufupi, nchi za Kimagharibi zinatangaza vita dhidi ya Uislamu duniani na hutumia visingizio vingi katika kampeni hii ya kinyama.   

(3) Tunaamini kuwa, lau Kenya ingekuwa na sera thabiti ya ndani na nje, haya yasingetokea. Serikali yoyote inayopenda kuweka amani kwa raia wake, basi ni lazima ihakikishe kuwa sera zake zote ni nzuri. Inasikitisha kwamba sera za nchi nyingi za Kiafrika ikiwemo Kenya ni mbovu; zilizo katika hatari ya kushawishiwa na nchi za kikoloni za Kimagharibi na dhamira zao za kibepari. Ni kupitia sera hizi ambapo Amerika na Uingereza zinang'ang'ania rasilimali asili za Somalia huku zikidai kupigana dhidi ya ugaidi. Baya zaidi, zinajaribu kuzishawishi nchi nyinginezo kusaidia dhidi ya ugaidi, katika hali nyingi ikisababisha hasara kubwa kama ile inayoshuhudiwa hivi sasa. Hii ni dhahiri shahiri huku idadi ya Wakenya wakikosa imani na oparesheni Linda nchi ndani ya Somalia. 

(4) Mwisho, tunafupisha kwa kusema kuwa Uislamu kama mfumo, unataka damu, mali na heshima ziheshimiwe. Hiyo ndio sababu unaharamisha umwagaji damu, huku ukiitaka serikali ya Kiislamu (KHILAFAH) kulinda usalama wa raia wake wote bila ya kujali dini, rangi wala asili yao. Sisi Hizb ut Tahrir tunalingania Uislamu kama mfumo na njia kamili ya maisha kwa lengo la kurejesha maisha kamili ya Kiislamu chini ya Dola ya Kiislamu Khilafah kwa njia ya Utume ambayo italinda damu, mali na heshima ya raia wake wote wawe ni Waislamu au wasiokuwa Waislamu.  

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu