Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Ramadan 1443 Na: 1443 H / 029
M.  Jumapili, 03 Aprili 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bangladesh Yazifunga Shule za Waislamu wa Rohingya
Yatishia Kuwavua Kitambulisho Chao na Kuwahamisha hadi Kisiwa cha Mbali Endapo Zitafunguliwa
(Imetafsiriwa)

Maafisa nchini Bangladesh wanatishia kuwanyang'anya wakimbizi wa Rohingya hati zao za utambulisho na kuwahamisha kwa nguvu hadi katika kisiwa cha mbali ambacho hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara, endapo watakiuka marufuku jumla kwa shule walizozianzisha, kulingana na shirika la Human Rights Watch. Ripoti iliyotolewa na shirika hilo ilisema kuwa wakimbizi wanahitaji hati za utambulisho zinazoitwa "kadi za data" zilizotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kwa ushirikiano na serikali ya Bangladesh ili kupata misaada na huduma za kimsingi. Tangu Disemba 2021, mamlaka za Bangladeshi zimepiga marufuku shule zilizoanzishwa na walimu wa Rohingya ili kufidia ukosefu wa elimu rasmi na ya sekondari katika kambi za wakimbizi, kufungwa kwa shule za Kiislamu, na kupigwa marufuku mashirika ya kibinadamu kutoa elimu kwa watoto wakimbizi wa Rohingya nje ya madarasa ya msingi na yasiyo rasmi na ngazi ya msingi.

Utaratibu mpya wa uhalifu unafanywa na mamlaka za Bangladesh dhidi ya ndugu na dada zetu wa Rohingya ambao wametafuta hifadhi huko ili kuepuka ukatili na uhalifu wa Wabudha dhidi yao. Inawazuia na kuwashinikiza katika riziki zao ikiwa ni pamoja na riziki za familia zao kwa kutishia kuwapokonya vitambulisho vyao vinavyotumika kupokea msaada. Juu ya hayo wanatishia kuwahamishia katika kisiwa kingine cha mbali ambacho hukumbwa mafuriko na vimbunga vya mara kwa mara, ambacho ilihamisha watu 20,000 hapo awali, si kwa jengine isipokuwa kwamba wakimbizi hao wa Rohingya walitaka kuwafundisha watoto wao juu ya Dini yao na sayansi za kiulimwengu, hivyo wakaanzisha shule za kujaza upungufu wa idadi ya shule, ambapo mamlaka ilizifunga, na kuwatishia walimu na walezi kutofundisha kwa siri majumbani mwao.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetahadharisha kuwa takriban watoto 30,000 watanyimwa elimu kutokana na hatua hizo, jambo linalomaanisha kupotea kwa kizazi kizima, kana kwamba watoto hao hawajaonja ukandamizaji na dhuluma za kutosha wanazokabiliana nazo nchini mwao, pamoja na uchungu wa hifadhi na ugumu wa njia yake, na ugumu wa kuishi katika kambi, kiasi kwamba wananyimwa elimu baada ya kupata njia ya kuifikia.

Mamlaka za Bangladesh zinadai kwamba zimechukua hatua hizi kwa lengo la kuziondoa shule "zinazopigia debe itikadi kali na kushiriki katika vitendo haramu." Kwa hiyo, walimwaga hasira zao kwa shule za Kiislamu na kuzifunga. Ni kisingizio dhaifu na kipimo kilichowekwa wazi katika vita na uadui wake kwa Uislamu na Waislamu na ukaribu wao kwa makafiri katika vita vyao viovu dhidi ya Uislamu na Waislamu chini ya kauli mbiu ya "Kupambana na Ugaidi na Itikadi kali."

Imedhihirika kwa kila mwenye macho na utambuzi kuwa utawala wa Kibengali na tawala nyinginezo katika nchi za Waislamu zimesaliti na kula njama dhidi ya masuala yao. Ni wakati muafaka sasa wa kuzipindua tawala hizi vikaragosi na kuzibadilisha kwa mfumo wa Kiwahyi, unaotabikisha Dini na kuwapa haki waliodhulumiwa na kukomesha mateso yao. Ni Khilafah Rashida ya pili pekee ndio inayoweza kufikia hili. Basi jitokezeni muisimamishe.

Enyi watu wenye nguvu na ulinzi: Mnusuruni Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na waumini, na Mwenyezi Mungu atawanusuru hapa duniani na kesho Akhera.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu