Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: 03:03:12 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  8 Rajab 1444 Na: 1444 H / 026
M.  Jumatatu, 30 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Lini Wanawake wa Kiislamu Watampata Mwenye Kuitikia Wito wao?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi, Wizara ya Afya ya Palestina ilitangaza vifo vya Wapalestina 9, akiwemo mwanamke mzee, na wengine kujeruhiwa na vikosi vya Kiyahudi, baada ya kuvamia mji wa Jenin na kambi yake.

Mauaji mapya yaliongeza kwenye msururu wa mauaji yaliyofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi dhidi ya watu waliobarikiwa wa Palestina tangu Ummah ulipotawanywa na kugawanyika katika siku ambayo mama mlezi, Dola ya Khilafah ilipokosekana. Katika mauaji haya, Mayahudi wanyang'anyi hawatofautishi kati ya kijana, mwanamke au mtoto. Katika mauaji haya, watu 9 waliuawa shahidi, akiwemo Magda Obaid, 61, mama wa wasichana 6 na mvulana mmoja. Alipigwa risasi shingoni ndani ya chumba chake katikati ya kambi ya Jenin alipokuwa akijaribu kutazama kile kilichokuwa kikitokea nje ya nyumba hiyo baada ya kusikia milio ya risasi. Shahidi Magda anatoka eneo la Hadera katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu mwaka 1948, na alikuja kuishi katika kambi ya Jenin miaka 25 iliyopita, akitokea mji jirani wa Ya`bad. Hizi ni kambi ambazo watu wengi wamekimbia makaazi yao ndani na nje ya Palestina, baada ya kampeni ya mauaji ya kikabila iliyofanywa na Mayahudi baada ya kuinyakua Palestina, na kukosa hali ya chini ya maisha ya staha.

Ukiukaji na matukio yote ya mauaji na uharibifu yanafanyika chini ya macho na masikio ya walimwengu wote, iwe ni wale wanaoimba kuhusu haki za binadamu, au wale wanaojifinika kwa guo la Uislamu na kuutetea miongoni mwa watawala wa Ruwaibidah (wajinga), ambao ni vibaraka wadhalilifu, wanaojibu kwa miitiko dhaifu ya kulaani au kukashifu.

Enyi Waislamu, Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina: umbile la Kiyahudi lililojengwa juu ya msingi wa kuua, dhulma, uporaji wa ardhi, ujenzi wa makaazi, uambatanishaji ardhi, Uyahudi, ukiukaji matukufu na upakaziaji uongo historia, haliwezi kuzuiwa kwa kulaaniwa, kushutumiwa, hotuba tupu, malalamiko kwa Baraza la Usalama, kuridhika na kunyenyekea kama ambavyo mamlaka ya Dayton inavyofanya, bali kwa kuling'oa kutoka kwenye mizizi yake mikononi mwa jeshi kubwa linaloongozwa na mtawala wa Kiislamu anayemcha Mwenyezi Mungu.

Ni jeshi tu mithili ya jeshi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), mjini Madina, jeshi la al-Mu'tasim, na jeshi la al-Mansur bin Abi Amir pekee ambayo yalijitokeza yote kuwanusuru wanawake wa Kiislamu, waliokuwa wakililia msaada wa watawala walinzi na mashujaa na wanajeshi waumini waliokuwa wakiilinda Dini yao, utu wao, na heshima yao, ndio watamnusuru shahidi huyo na wanawake wengine wa Kiislamu. Je, ni lini mutajibu wito huu?! Je, ni lini mutaitekeleza aya hii adhimu?!

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72].

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu