Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  7 Rajab 1441 Na: 1441 H / 011
M.  Jumatatu, 02 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
                             Chini ya Kisingizio cha Hali za Kibinadamu                    Upatanishi Unafanyika huko nchini Syria na Muuaji wa Watoto na Wanawake
(Imetafsiriwa)

Zaidi ya raia 20 waliuawa Jumanne iliyopita katika mashambulizi yaliyotekelezwa na vikosi vya kijeshi vya Syria kwa kuwalenga raia ikijumuisha shule. Shirika la Ufuatilizi wa Haki za Kibinadamu liliripoti kwamba takribani watoto tisa na walimu watatu waliuawa katika kuzidi kwa mashambulizi katika mkoa wa Idlib kaskazinimagharibi mwa nchi.

Ni muhimu kutambua kwamba mnamo Septemba 2018, mkoa wa Idlib ulibadilishwa na kuwa eneo la kusitisha vita kwa ridhaa ya Uturuki, Urusi na Iran – washikadau maarufu wa kimataifa katika mzozo – uadui uliharamishwa na pande zote ziliruhusiwa kuasisi vituo vyao vya uchunguzi wa kijeshi. Makubaliano haya yalikiukwa mnamo Aprili iliyopita, pale ambapo Syria na vikosi vyake vilianza mashambulizi ili kuyateka maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya upinzani katika mikoa ya magharibi ya Aleppo na Idlib. Kisha wakaanzisha tena mashambulizi mnamo Disemba iliyopita ili kuendelea kusonga mbele kusini mwa mkoa wa Idlib na kuviteka vijiji vingi na miji mingi ndani yake. Mabomu yalianza upya licha ya kuwepo makubaliano ya kusitisha vita mnamo Januari 12 baina ya Uturuki na Urusi. Dhalimu wa Ash-Sham alitoa ahadi wiki iliyopita kwamba ataendelea na mashambulizi, akisema kwamba vita bado havijaisha, lakini pia “ushindi wa kukatikiwa” haujamitia.

Kwa mujibu wa afisaa wa haki za kibinadamu wa UN, takribani raia 300 wameuawa kutokana na mashambulizi ya mwaka huu ndani ya eneo hilo, na takribani watu 900,000 kaskazini-magharibi mwa Syria wamelazamishwa kuwacha nyumba na makaazi yao kwa kipindi cha miezi mitatu, ikijumuisha takribani watoto 500,000 na kutafuta makaazi karibu na mpaka wa Uturuki ambapo wanahisi kuwa wagonjwa na wamekwama. Hawawezi kuingia Uturuki; na hawawezi kurudi nyumbani kwao ili kupata msaada muhimu kutokana na kuzidi kwa hali mbaya ya hewa na upungufu mkubwa wa mahitaji msingi ikijumuisha chakula, maji safi, madawa, nguo za joto, mafuta na mahema. Idadi ya waliofariki imerikodiwa ikijumuisha watoto kutokana na hali ya baridi. Umoja wa Mataifa ilisema mnamo Jumatatu iliyopita kwamba mapigano mapya “yalikuwa hatari mno karibu” na kambi za waliofurushwa, ikiashiria kutarajiwa “umwagikaji damu mkubwa.”

Kwa kuzingatia kwamba Urusi imezidisha mashambuliz yake na kimya cha Uturuki kuhusiana na mabomu, mauaji na oparesheni za kijeshi zinazotekelezwa na vikosi vya utawala dhalimu ndani ya eneo hilo, kuna mazungumzo mengi hivi majuzi kuhusiana na ugumu wa hali ya kibinadamu kwa raia, ima kutokana na mashambulizi ya Urusi na vikosi vya utawala au hali ya waliofurushwa walioko peupe, yote haya yakiwa ni katika utangulizi wa kuanza kwa mchakato wa Amerika wa suluhisho la kisiasa, ambao ni upatanishi na muuaji wa watoto, wanawake na wazee na kurudi katika utumwa tena, kama ambaye hakukutokea chochote. Gazeti la Uingereza la Guardian lilimnukuu mwanadiplomasia akisema kwamba “lipo pendekezo la kufahamikiana upya baina ya Urusi na Uturuki na utawala wa Assad, ambalo kwa mujibu wake eneo la kizuizi litapunguzwa na kuwa sehemu ya kilomita 25 na kisha kuiruhusu Uturuki kuchukua mlima wa Rif’at. Msemaji wa rais wa Uturuki Ibrahim Kalin alisema: “Mashambulizi kwa Idlib lazima yasitishwe haraka iwezekanavyo na tunasubiria hili lifanyike kupitia makubaliano ya kusitisha vita na hili ndio azimio letu msingi kutoka kwa upande wa Urusi.”

Wametumia mtazamo wa kibinadamu na hatari kwa raia kama kisingizio, ilhali wao ndio ambao wamekuwa wakiua watoto nchini Syria kwa takribani miaka tisa sasa hadi leo, ndani ya Aleppo, Idlib na maeneo mengine. Wanachinjwa, wanauawa na kupigwa mabomu ya kila aina ya silaha, katika makaazi yao, shule, hospitali, kambi na sehemu za wazi, mipakani na mbele ya macho na masikio ya watawala wa nchi za Waislamu ambao wametosheka na kutoa tu hotuba za kujirudiarudia za vitisho ambazo watu wamezizowea kama vitisho na ahadi za mtawala wa Uturuki Erdogan kwamba atatumia nguvu za kijeshi kuvifurusha vikosi vya Syria, isipokuwa wajitoe mwishoni mwa Februari! Vitisho hivi vya kupotosha, lau ni muhimu (kwa yeyote), bali vinakuza umaarufu wake ambao uko katika tishio baada ya kupoteza takribani asilimia 10 za kura ikilinganishwa na 2014.

Mwishoni mwa tarehe ya Februari, ambayo utawala wa Uturuki uliipa utawala wa kihalifu kukamilisha oparesheni yake, “Rais wa Uturuki alitangaza mnamo Jumamosi iliyopita katika mkutano wa 5 Machi akiwa pamoja na viongozi wa Urusi, Ufaransa na Ujerumani ili kujadili hali ya mkoa wa Idlib.” Hivyo basi, mikutano na makongamano yanafanyika kwa siku hata miezi, yote chini ya kisingizio cha kusitisha umwagaji damu ya raia na kuwabunia eneo salama. Hata hivyo, wanalenga kupata muda zaidi wakisubiri makubaliano ya nyuma ya pazia yakiwa na muonekano mpya, ili kulazimisha sera ya “uhalisia mashinani” kwa kurudisha udhibiti wa utawala wa Assad kwa mara nyingine katika ardhi yote ya Syria na kufutilia mbali kujitolea muhanga kukubwa miongoni mwa mukhlisina, ili kusitisha ukandamizaji wa kidhalimu wa utawala wa Baath.  

Enyi Majeshi ya Waislamu:

Mwenyezi Mungu (swt) asema jukumu la Muislamu kuhusiana na kaka na dada zake wanaokandamizwa,

 [وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72].

Mtume (saw) alisema:

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لَا يُسْلِمُهُ وَلَا يَظْلِمُهُ وَلَا يَخْذُلُهُ»

“Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamsalimishi, hamkandamizi, hamuangushi.”

Miito hii mitukufu haizingatiwi na watawala wa Waislamu, ambao hatutarajii lolote zuri kutoka kwa Ummah huu. Wamewauza watu na nchi na kuwaangusha wanawake na watoto. Inawezekana vipi miito hii isifikie masikio yenu ilhali nyinyi ndio watu wenye nguvu na ulinzi?! Je mayowe ya watoto wa Syria, ambao wamepangiwa njama dhidi yao na kila ambaye anawachukia na anayeuchukia Uislamu na Waislamu, hayajawafikia nanyi pia?

Hivyo basi, tunawalingania mutoe Nusra (msaada) kwa Hizb ut Tahrir kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ndio ngao ya ulinzi na ngome yake. Na ndio ambayo itayahami majeshi pasi na kuchelewa, ili kutimiza majukumu yenu ya kuwakomboa Waislamu na kuwalinda wale wote wanaokandamizwa duniani, na mutakuwa walinzi wa Dini!

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرا]

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako?” [An-Nisa’: 75]

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu