Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  2 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: H 1445 / 05
M.  Ijumaa, 10 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Kuchimba Migodi katika Eneo linaloishi Viumbe Hai (Biosphere) ni Dhulma kwa Umma!

(Imetafsiriwa)

Rais Sadyr Japarov alifanyia marekebisho sheria kuhusu “maliasili zilizo chini ya ardhi” na “maeneo yanayoishi viumbe hai (biosphere)” ambapo utafiti wa kijiolojia na utafiti katika maeneo ya yanayoishi viumbe hai (biosphere), uchunguzi wa kijiolojia wa rasilimali za dunia, uchimbaji wa akiba muhimu na kazi ya uchunguzi wa kijiolojia kwa rasilimali za chini ya ardhi zitafanywa kwa msingi wa uamuzi wa serikali.

Wataalamu wanasema kuwa serikali nchini Kyrgyzstan inajaribu kuchimba urani kutoka mgodi wa Kyzyl Ompol kupitia sheria hii, tena. Mnamo 2019, utafiti, uchunguzi na ukuzaji wa akiba za urani na thorium ulipigwa marufuku kwa sababu ya maandamano ya umma. Kulingana na toleo la sasa la sheria, eneo la Issyk-Kul ni eneo la asili linalolindwa mahususi lenye umuhimu wa kitaifa.

Kabla ya hapo, suala la kuendeleza mgodi huo lilikuwa mjadala moto katika jamii, baada ya mkutano wa Japarov na wakaazi wa eneo hilo katika mgodi wa Kyzyl Ompol katika eneo la Issyk-Kul.

Mgodi wa Kyzyl Ompol ulifunguliwa katika eneo la Tonj mwaka wa 1951. Kuna maeneo makuu matano yenye rasilimali za chini ya ardhi katika eneo hilo, ambapo sehemu kubwa iko katika eneo la Tosh Bulak. Wakati wa utafiti uliofanywa wakati wa zama za Muungano wa Kisovieti, iligundulika kuwa ulikuwa na tani elfu 13 za urani. Hapa, tani 3,080 tu za urani ziligunduliwa kutoka kwa takwimu iliyotajwa hapo juu. Mnamo 2019, Shirika la Eurasia lilianza uchunguzi katika eneo hili. Hata hivyo, inageuka kuwa kuna tani 3,519 za hifadhi ya urani katika eneo la Tosh Bulak lenyewe kutokana na matokeo ya utafiti mpya. Urani na misombo yake hutumiwa zaidi kama mafuta ya changamshi katika viwanda vya nyuklia na kama vilipuzi katika silaha za nyuklia na mabomu. Bei ya kilo moja miaka 5-10 iliyopita ilifikia $300, huku bei yake sasa ni karibu $100. Vita vinapozidi kuongezeka nchini Ukraine na maeneo mengine mengi, bei ya urani inaongezeka.

Hifadhi inayokadiriwa ya thoriumu huko Kyzyl Ompol ni tani 29,252. tani 6,880 kati ya hizo kwa sasa ni hifadhi zinazoweza kuchimbwa. Tani 3,390 zake ziko katika eneo la Tosh Bulak. Kulingana na data zingine, Tosh Bulak yenyewe ina akiba ya tani 8,499. Thorium ni nyenzo ya mionzi, mithili ya urani. Inachukuliwa kuwa mustakabali wa nishati ya nyuklia kwa sababu ya uwezo wake wa juu wa nishati. Kwa usahihi zaidi, tani moja ya nyenzo hii hutoa nishati sawa na tani mia mbili za urani au tani milioni tatu za makaa ya mawe. Bei ya kilo moja yake kwa sasa ni kama $100. Mbali na nishati ya nyuklia, hutumiwa katika sekta ya madini, uundaji wa ndege, na uzalishaji wa jenereta. Pia hutumiwa kama nishati kwa vyombo vya anga na nyambizi, pamoja na urani.

Zirconium au zirconium oxide (oksidi) ilikadiriwa kuwa tani 287,636 huko Kyzyl Ompol. 94,000 na tani 441, pamoja na akiba zinazoweza kurejeshwa. Kuna tani elfu 34 zake huko Tosh Bulak. Zirconium pia hutumiwa mara nyingi katika nishati ya nyuklia ili kurutubisha urani na vifaa vingine vya mionzi. Inatumika sana katika ujenzi, dawa na madini. Zirconium pia haina mionzi zaidi kuliko urani na thorium, lakini ni sumu. Bei ya kilo ya zirconium inatoka $ 100 hadi $ 500-600, kulingana na aina yake.

Kuna tani nusu milioni za oksidi ya fosforasi (phosphorus oxide) huko Kyzyl Ompol. Tani 124,645, ikijumuisha hifadhi halisi. Kuna tani 10,000 pekee katika eneo la Tosh Bulak. Fosforasi hutumiwa hasa kwa mbolea ya madini. Fosforasi sio sumu, lakini ikiwa imejazwa urani, inakuwa na mionzi. Bei yake inatofautiana kulingana na nyenzo ambayo imetengenezwa kwayo.

Kiasi cha titanium na magnetite inayopatikana katika eneo hili ni tani milioni 14. Ni tani milioni 2.6 pekee ndio hifadhi zinazoweza kurejeshwa (recoverable). Kuna tani milioni 1.6 zake katika eneo la Tosh Bulak. Titanium hutumiwa katika utengezaji wa magari, meli, ndege, makombora, utengezaji wa kemikali, vifaa vya miundo, alloys, uchimbaji wa rangi, vifaa vya umeme visiunganishwa na waya na nyanja nyenginezo. Bei ya kilo ya titanium ni kati ya dolari 5-6 hadi 20, kulingana na usafi wake.

Kwa kuzingatia asilimia za rasilimali za madini zilizotajwa hapo juu, 95% ya madini hayo ni titanium na magnetite, 3% fosforasi, zirconium 2%, thorium 0.22% na uranium 0.17%.

Kwa hiyo, ni wazi kwamba hifadhi za mgodi katika Kyzyl Ompol ambayo faida halisi ni kidogo. Kwa maana nyengine, madai ya Waziri Mkuu Akilbek Japarov ya rasilimali zilizo chini ya ardhi zenye thamani ya hadi $300 bilioni  yanakinzana na uhalisia. Ni wazi kuwa uchimbaji madini katika baadhi ya migodi mirefu hauhalalishi gharama yake.

Inajulikana kuwa mizozo kuhusu Kyzyl Ompol iliongezeka zaidi mwaka wa 2019. Mwaka huo, ujumbe wa Urusi ukiongozwa na Rais wa Urusi Putin ulifika Kyrgyzstan kwa ziara ya kiserikali, na wakati wa ziara hiyo, mikataba mingi ya umma na ya siri ilitiwa saini. Matokeo yake, rasilimali zote za chini ya ardhi zilitolewa kiuchumi kwa Urusi, na ikiwa kulikuwa na zaidi, wangeweza kupewa wengine. Kwa mfano, ingawa Shirika la Eurasia la Kyrgyzstan, ambalo lilichunguza mgodi wa Kyzyl Ompol, lilisajiliwa nchini Canada, 60% ya hisa zake zilikuwa za Urusi, na 40% za Kyrgyzstan. Kwa hivyo, wanasiasa wa Kimarekani nchini Kyrgyzstan, chini ya jina la "wanaharakati wa kiraia", walikuwa na bidii katika kuamsha kutoridhika kwa watu na mradi wa Eurasia. Kwa sababu hiyo, serikali ya Jeenbekov ilishindwa kutimiza ahadi zake kwa Urusi, na Jeenbekov alilazimika kutangaza kusitisha uchimbaji wa madini ya urani nchini Kyrgyzstan, kutokana na upinzani wa umma.

Sasa, serikali ya Javarov imeanza kuendesha mgodi huu. Faida zake zinazingatiwa, licha ya kuwepo kwa vitu vyenye hatari kwa afya ya wakaazi huko Kyzyl Ompol. Kulingana na Japarov, mgodi huu pia una idadi ya madini ya thamani, kama mgodi wa Kumtor. Kwa kweli, bila kujali chanzo cha utajiri wa madini, haina muundo sawa. Kwa mfano, mgodi wa Kumtor hauna dhahabu pekee, bali pia vitu vingi kama fedha, shaba na sulfur. Hata hivyo, ripoti zilizotolewa kuhusu mgodi wa Kumtor zilijumuisha mahesabu ya faida kutoka kwa dhahabu pekee, kwa muda wa miaka 30.

Kwa bahati mbaya, serikali ya sasa imedhamiria kuendeleza uhalifu wa watangulizi wake, kwa manufaa yake, ingawa uendeshaji wa madini ya urani na thorium una madhara kwa wananchi. Uchimbaji wa madini ya Urani ni tatizo la kweli kwa watu, kwa sababu mgodi huu uliotajwa upo kwenye mwinuko wa mita 1640-3000 juu ya usawa wa bahari. Pindi urani inapotolewa chini ya ardhi, hatari ya mionzi huongezeka, na mabaki hutoka wakati wa mchakato wa kurutubisha urani, na hatari ya mionzi inaendelea kwa miaka elfu kadhaa. Uharibifu wake unaenezwa na maji na upepo. Maji ya mkondo huungana ndani ya mgodi na kujiunga na maji ya Chuy. Kwa kuwa eneo la ziwa lina upepo, upepo huvuma kila wakati kutoka kwa mgodi kuelekea Balıkchi. Pia ni hatari kusafirisha malighafi zilizotolewa kwenye kiwanda cha usindikaji. Makontena yaliyosheheni madini ya urani yakipata ajali, watajaribu kuwahadaa watu kuwa ajali hii haina madhara kwa afya za watu, lakini bado wananchi watapata madhara. Tulishuhudia tukio kama hilo katika ajali ya Barskoon cyanide.

Kwa hakika, urani, kama kila chengine chochote, ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya wanadamu. Tusipoitumia jinsi Mwenyezi Mungu alivyotuamuru, itageuka kuwa maafa kwa wanadamu, na sio baraka. Sasa, katika mfumo wa kibepari, uchimbaji wa mgodi huu wa urani unachukuliwa kuwa ni tatizo la kiuchumi na kupewa makampuni binafsi ya kibeberu, na madhara yake kwa watu hayatiliwi maanani. Madai yao ya kwamba “tunachimba bila madhara” si chochote ila ni uongo, kwa sababu wakiona kitu chenye manufaa kwao hawafikirii kitu chengine. Uislamu hauoni kuwa ni tatizo la kiuchumi, bali ni tatizo la kibinadamu. Kwa hiyo, uchimbaji wa urani unaruhusiwa tu wakati hauna madhara kwa watu. Inategemea imani ya watu na uchamungu (taqwa) kufanya hivi.

Aidha, kwa mujibu wa Sharia, urani inachukuliwa kuwa mali ya umma ambayo manufaa yake yanapaswa kumfikia kila mtu katika dola. Ni Dola ya Kiislamu pekee ndiyo itakayoitumia kwa manufaa ya umma, iwe kwa kuitumia kama nishati ya kiwanda cha nguvu za nyuklia na kutoa nishati inayozalishwa kwa watu bila malipo, au kuzalisha silaha za nyuklia ili kuongeza fahari ya Dola ya Kiislamu, lakini hili halipo kwa sasa. Kuipa urani nchi za kikafiri na makampuni yao ni haramu kwa hali zote.

Kwa kumalizia, mfumo wa leo wa kibepari ni mfumo unaotegemea matumizi, hivyo madhara yanayosababishwa kwa watu wakati wa kuchimba madini hayazingatiwi. Madai yao kwamba wanaweza kuchimba madini kwa njia zisizo na madhara si chochote ila ni uwongo. Hii imeonekana wazi kwa kuyeyuka kwa barafu huko Kumtor na kuvuja kwa cyanide ndani ya maji. Wanasiasa wasitumie tatizo hili kama silaha katika kupigania madaraka. Kuwasaidia katika kazi hii pia ni dhambi. Kwa hiyo, wananchi hawana budi kuiwajibisha serikali kuhusu suala la urani kwa mujibu wa Sharia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu