Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  1 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H.T.L 1445 / 19
M.  Ijumaa, 07 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kisimamo cha Hizb ut Tahrir katika Mji wa Sidon
“Ee Jeshi la Kinana, Wakati Umewadia”

(Imetafsiriwa)

Katika msururu wa visimamo vilivyofanywa na Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon, kuinusuru Gaza na ukakamavu wake dhidi ya mashini ya kihalifu ya kijeshi ya umbile la Kiyahudi, na kuyachochea majeshi kuchukua nyadhifa za fahari zinazohitajika kutoka kwao, hasa jeshi la Kinana Misri, jeshi la Jordan, na majeshi ya Waislamu, ambayo yanaorodheshwa kati ya majeshi ya kwanza duniani kwa idadi na vifaa. Leo, Ijumaa, tarehe 6/7/2024, Hizb ilifanya kisimamo katika mji wa Sidon, mji mkuu wa kusini, ambao ulipambana na kumshinda mvamizi katika historia yake angavu. Kilitanguliwa na vituo viwili jijini Tripoli, ash-Sham na Bekaa mnamo Ijumaa 5/31/2024.

Kulikuwa na hotuba za wazungumzaji mashuhuri, zilizoanzishwa na Dkt. Bassam Hammoud, Makamu wa Mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Chama cha Kiislamu nchini Lebanon, ambapo aliweka wazi kwamba dori muhimu zaidi inapewa majeshi katika eneo hilo, ambayo hadi sasa bado wangali wanaiangusha Gaza na Palestina na kwamba Waislamu lazima wachukue kila dori inayowezekana kwa maneno, utetezi, silaha, na pesa, wakikumbuka kwamba tawi la kijeshi la Chama cha Kiislamu, linalowakilishwa na Vikosi vya Al-Fajr, linafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuwanusuru watu wetu nchini Palestina na Gaza na bado kinaendelea kutoa mashahidi kwenye njia hii, akibainisha umuhimu wa misimamo hiyo na kuendelea kwake. Kisha ikaja hotuba ya afisa wa uhusiano wa Kiislamu katika harakati ya Jihad nchini Lebanon, Ndugu Shakib Al-Aynat, ambaye alivisifu vita hivyo na kuendelea kwake kuwa ni kati ya haki kamili na batili kamili, na kwamba watu wa Palestina wanakabiliana na Mayahudi na Magharibi nyuma yao, hasa Marekani, na aliisifu misimamo ya kuwanusru watu wa Palestina kwa jumla na hasa Gaza.

Kisha maneno ya kufunga yalikuwa ni hotuba ya mwanachama wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Abu Hamza Misriya, ambapo alibainisha kwamba sura ya kusikitisha ya Gaza inadhihirisha uhalisia wa Ummah wetu, uliochanika vipande vipande, ukikandamizwa na kibaraka dhalimu mlaji njama hapa na pale anayewazuia kunusuriana. Bendera za Sykes-Picot zinapepea juu ya mbingu zetu badala ya bendera: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Alielekeza hotuba yake katika kuhamasisha azma ya majeshi, hivyo akasema, akiwahutubia: Enyi watu wenye nguvu katika majeshi ya Waislamu, je mandhari za damu inayotiririka katika ardhi ya Gaza na Palestina, kibla cha kwanza cha Waislamu, mahali pa Masrah (safari ya Mtume wenu), hazikuathirini?! Je, hamusikii sauti za wale wanaokulilieni wakiwemo wanawake, watoto na wazee wasioweza kupata msaada wala njia?! Enyi Askari Waislamu katika Majeshi: Je, hamuoni kwamba nyinyi ni walinzi wa kundi la vibaraka linalokula njama za kumwaga damu za ndugu zenu mbele ya macho ya kila mtu?! Enyi askari katika Majeshi ya Waislamu: Je, hivi mnadhani Mayahudi ni watu wa vita? Hapana, Wallahi wao ni waoga zaidi kuliko mnavyotarajia. Tuna somo katika matukio matukufu ya tarehe 7 Oktoba 2023; Idadi ndogo ya vijana waumini waliondoka baada ya kutawadha na kuswali huku wakimtegemea Mwenye nguvu, Mwenye nguvu, Mwenye kunusuru na Msaidizi. Walifanya vyema kwa silaha zao hafifu, mbele ya majeshi ya uovu yenye nguvu zaidi, wakiwaua baadhi, wakiwajeruhi, na kuwateka wengine.

Kisha kisimamo hicho kilihitimishwa kwa dua ya Haj Hassan Al-Nahhas, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon.

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye fadhila zake ni njema.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu