Alhamisi, 14 Sha'aban 1446 | 2025/02/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  9 Sha'aban 1446 Na: H.T.L 1446 / 11
M.  Jumamosi, 08 Februari 2025

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23].
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir in Wilayah Lebanon inaomboleza mmoja wa watu wake miongoni mwa wabebaji dawah:

Hajj Ali Ezz Eldien Al-Duhaibi

Ambaye alifariki katika mji wa Miniyeh jioni ya Jumamosi, tarehe 9 Shaaban 1446 H sawia na 8/02/2025 M.

Hajj Ali Al-Duhaibi, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliishi miaka sabiini na tatu, ambayo mingi yake aliitumia kubeba Dawah ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah, akilingania haki kwa uwazi, bila kuogopa lawama ya mtu yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mfano na kiigizo chema katika kusimama dhidi ya batili, kuamrisha yaliyo mema na kukataza yaliyo mabaya, na licha ya maradhi na uzee, hakurudi nyuma wa kusitasita katika kubeba Dawah.

Shujaa huyu alishuka na akwenda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sifa zimwendee kwa vijana waliojiunga na Dawah, hao ni matunda ya juhudi zake.

Sisi ndugu zake katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Amjaalie yale yaliyompata kuwa kafara na utakaso, akubali kutoka kwake yale aliyoyatoa na kuyafanyia kazi katika njia ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na amkusanye yeye, kwa rehma zake, pamoja na Manabii, wakweli, Mashahidi, na watu wema. Wao ndio masahaba wazuri!

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [AlBaqara:156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu