Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  28 Jumada I 1446 Na: HTM 1446 / 14
M.  Jumamosi, 30 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miaka Miwili ya Utawala bila Uislamu: Kupuuza Amana ya Mwenyezi Mungu

(Imetafsiriwa)

Katika hafla ya kuadhimisha mwaka wake wa pili afisini, Waziri Mkuu wa Malaysia, Datuk Seri Anwar Ibrahim, aliandaa Mpango wa Miaka Miwili wa Serikali ya Madani (2TM) na Kongamano la Kitaifa la 2024 la Marekebisho ya Utumishi wa Umma mnamo Novemba 23-24, 2024 katika Jumba la Mikutano la Kuala Lumpur (KLCC). Hafla hilo ilionyesha huduma mbalimbali za serikali chini ya paa moja, na zaidi ya vibanda 30 vinavyotoa huduma na bidhaa kwa umma. Ripoti zilisifu hafla hiyo kuwa ya mafanikio, ikiwa na zaidi ya wageni 200,000. Zaidi ya hayo, Anwar aliendesha kikao cha ukumbi wa jiji kuangazia mafanikio na mipango yake chini ya serikali ya Madani huku akishughulikia ukosoaji, haswa kuhusu mahojiano yake ya CNN yenye utata kuhusu uwepo wa umbile la Kiyahudi na ufadhili wa makampuni ya kibinafsi wa safari zake na ujumbe wake nje ya nchi.

Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia! Haijalishi ni kwa upana kiasi gani unasimulia mafanikio yako, watu wanafahamu kikamilifu uhalisia wao, baada ya kuyapitia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Baada ya miongo kadhaa ya mapambano kufikia nafasi yako ya sasa, uliahidi mwezi na nyota kwa watu, na ilikuwa juu ya ahadi hizi kwamba waliweka imani yao kwako. Hata hivyo, miaka miwili ya utawala wako, watu wamekua wakifahamu zaidi utawala wako na uhalisia wa ahadi zako.

Hivyo, katika hatua hii muhimu ya utawala wako, tunakukumbusha kwamba nafasi yako ni dhamana ya kimungu iliyotolewa na Mwenyezi Mungu (swt). Yeye Ndiye Aliyekuweka hapo, na Amefanya hivyo kwa lengo kubwa: kwa ajili yako kutekeleza sheria Zake kwa ukamilifu na kueneza Dini Yake duniani kote. Ni wajibu wako kuung'oa mfumo wa kikoloni-demokrasia na kuuweka mfumo wa Khilafah kama ulivyoasisiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Amana hii ni jukumu kubwa ambalo Mwenyezi Mungu (swt) amekupa wewe kama kiongozi wa Malaysia. Kwa kukubali cheo cha Waziri Mkuu, umekubali mzigo wa amana hii— ambayo ni nzito sana hivi kwamba mbingu, dunia, na milima zilikataa kuibeba. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَنْ يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنْسَانُ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا]

“Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga.” [Al-Ahzab (33) :72].

Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia! Inaumiza moyo kwamba unaonekana kupuuza au kushindwa kutafakari sababu ya Mwenyezi Mungu (swt) kukuweka katika nafasi hiyo. Yeye (swt) anakupa fursa ya kufikia aidha heshima au fedheha. Ukiitimiza amana hii kwa kutekeleza sheria zake, utapata heshima duniani na Akhera. Kinyume chake, ikiwa utasaliti amana hii, utakabiliwa na fedheha na mateso katika maisha yote mawili. Chaguo ni lako. Pamoja na amana hii, Mwenyezi Mungu (swt) ametoa onyo kali; Kushindwa kuisimamia kutakuweka miongoni mwa waovu, madhalimu na makafiri, endapo usaliti utaambatana na imani.

Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia! Unapoketi kwenye kiti chako cha madaraka, ukipumua hewa ambayo Mwenyezi Mungu (swt) anakupa, tunakusihi utafakari kama umeitimiza amana hii au umeisaliti katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Jibu, tuna uhakika, ni wazi kwako na sisi. Ingawa unaweza kujivunia kuboresha mtazamo wa umma wa utawala wako, hili lina umuhimu mchahce au halina kabisa. Swali muhimu zaidi ni kiasi gani umefanya kuboresha msimamo wako mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Kumbuka, nguvu zako ni za kupita. Hazipaswi kupotezwa kwa kupuuza amana ya mungu juu ya mabega yako. Historia imejaa mifano ya jinsi Mwenyezi Mungu (swt) alivyowavua upesi hata yule mwenye uwezo mkubwa zaidi wa mamlaka yake. Baadhi wamekwisha kutana na Mola wao wakiwa wamebeba mzigo wa khiyana, na wengine wanangojea zamu yao.

Ama wasaidizi wako wanapokusifu, sifa kama hizo zisikupeleke kwenye kuridhika, kwani hazikuongezei cheo chako mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Badala yake, sikiliza ukumbusho wetu: wokovu wa mwisho upo katika kutimiza amana hii—wajibu ambao tumeshuhudia ukiupuuza katika kipindi cha miaka miwili iliyopita—simamisha sheria za Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu! Mawaidha yetu yanalenga kuwa ushahidi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama, ili usije ukaishi maisha ya mwisho kwa majuto. Kama Mtume Muhammad (saw) alivyoonya, uongozi unaoshindwa kutimiza amana yake huwa chanzo cha fedheha na majuto.

Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia! Mawaziri Wakuu wengi wamekutangulia, na vyama vingi vya kisiasa vimeshika madaraka, lakini hakuna hata kimoja kilichotimiza amana ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliwapa. Kwa hakika, katika ulimwengu wa Kiislamu leo, watawala sio tu kwamba wanasaliti amana yao ya Mwenyezi Mungu, bali pia, katika baadhi ya matukio, wanawakandamiza watu wao wenyewe, hasa wale wanaotaka kusimamishwa kwa Dini ya Mwenyezi Mungu.

Enyi Waislamu! Mnawajua watawala wenu vizuri na munajua kabisa ikiwa wanatimiza imani yao au wanasaliti. Msiwe miongoni mwa wale wanaounga mkono watawala wasaliti. Badala yake, jilinganisheni na wale wanaojitahidi kurudisha amana hii kwa mbebaji wake halali—Khalifa ambaye atatekeleza sheria za Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu, kuunganisha Ummah chini ya mwavuli mmoja, kuwashinda maadui wa Uislamu, kukomboa ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu, kufungua ardhi mpya, na kuiangaza dunia kwa nuru ya Mwenyezi Mungu (swt). Matarajio haya wakati fulani yalitimizwa chini ya Khilafah, na Insha Allah, yatatimizwa tena hivi karibuni, kwa kurudi kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume— ruwaza ya Hizb ut Tahrir inaendelea kufanya kazi kwa kiwango cha kimataifa.

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu