Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  24 Jumada I 1444 Na: 1444/05
M.  Jumapili, 18 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mikopo Haitarekebisha Kile ambacho Ubepari Umeharibu

Je, Misri inawezaje Kustahamili Uokozi Mfululizo wa Mikopo na Mfumko wa Bei Unaotokana Nayo?

 (Imetafsiriwa)

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulitangaza kuidhinisha mpango wa ushirikiano wa miezi 46 kwa Misri, wa kiasi cha dolari za Marekani bilioni 3, kulingana na taarifa kutoka IMF mnamo Jumamosi 12/17/2022. Kifurushi cha sera zilizojumuishwa katika mpango huo ni pamoja na hatua, ikijumuisha mabadiliko ya kudumu kwa mfumo wa viwango vya ubadilishanaji wa fedha na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kupunguza viwango vya mfumko wa bei.

Migogoro inayoikumba Misri kiasili ilisababishwa na udhibiti wa Magharibi juu ya nchi yetu na utawala wake kwa sheria zake za kibepari zilizotungwa na mwanadamu zinazofanya kuwepo kwake na kupora mali ya nchi ndani ya mfumo wa sheria na jukumu la ulinzi kutoka kwa tawala zilizopo. Na mageuzi yote yanayopendekezwa, ndani ya mfumo wa ubepari, yanazidisha migogoro na kuongeza mateso ya watu, na hivi ndivyo mikopo ya taasisi za kimataifa hufanya ikiambatana na maamuzi ya kuangamiza.

Taratibu au masharti haya yatapelekea kupungua kwa bei ya pauni ya Misri dhidi ya dolari, na hivyo kupanda kwa bei za maduhuli na kupungua kwa bei za mahuruji. Ni kweli kwamba kushuka kwa thamani ya pauni kunaweza kuboresha ushindani wa bei ya bidhaa na huduma za Misri (mradi tu mahitaji yao nje ya nchi yanabadilika, na hali sio ilivyo katika mahuruji ya Misri), lakini hii itaongeza gharama ya maduhuli ya Misri (ambayo hayana mabadiliko kwa mahitaji, ambayo ina maanisha ongezeko kubwa la gharama ya uagizaji). Uchunguzi uliofanywa juu ya kuimarika kwa kiasi cha mahuruji na maduhuli ya Misri unathibitisha kwamba kushuka kwa thamani ya pauni ya Misri hakukuwa na athari nzuri kwenye mizani ya biashara ya Misri. Kadiri thamani ya pauni inavyopungua, ndivyo bili ya maduhuli inavyoongezeka bila kupunguza idadi yake. Misri inaagiza zaidi ya 80% ya kile inachotumia, na kushuka huku kwa pauni hakuathiri kiasi cha mshuruji ya Misri, na hii inaweza kuthibitishwa kupitia data ya mizani ya shughuli za sasa za Misri. Hapo awali, Benki Kuu ya Misri ilitangaza kwamba miamala ya uchumi wa Misri na ulimwengu wa nje kutoka Julai hadi Disemba ya mwaka wa fedha wa 2021-2022 ilisababisha kuongezeka kwa nakisi ya akaunti ya sasa na kurekodi takriban $7.8 bilioni, ikilinganishwa na takriban $7.6 bilioni kwa kipindi kama hicho kutoka mwaka wa fedha uliopita. (Al-Arabiya 4/15/2022). Ikimaanisha kuwa kushuka kwa thamani ya sarafu kutasababisha kuongezeka kwa viwango vya mfumko wa bei, kutokuwa na uwezo wa kununua, na kuongezeka kwa kiwango cha umaskini na masikini. Hivi ndivyo sheria za kibepari zilizotungwa na binadamu zinafanya nchini Misri. Mnamo Mei 2019, Benki ya Dunia ilitangaza kwamba "takriban 60% ya Wamisri ima ni maskini au wanahitaji zaidi" ikimaanisha kuwa wamefuzu umaskini.

Haiwezekani kushughulikia mfumko wa bei na umaskini na kurekebisha uchumi kwa masharti ya mfuko huo na kwa kuzingatia ubepari na masuluhisho yake ya kifisadi na sarafu za karatasi zisizo na thamani halisi. Badala yake, yote yanayotokea ni majaribio ya kupunguza athari za maamuzi hayo mabaya kwa watu ili kuepusha au kuchelewesha mlipuko wowote unaoweza kutokea kwa shinikizo zinazoongezeka ambazo zinazidi uvumilivu wao.

Watu wanapaswa kufahamu kwamba Misri, pamoja na rasilimali zake, haihitaji mikopo au misaada ya kimataifa, hata kama haina masharti. Misri inajitosheleza kwa hili pamoja na rasilimali na utajiri wake, ikiwa tu mseto wa rasilimali utatumiwa ipasavyo na utajiri unatolewa kutoka kwao, na ikiwa serikali itaachana na dolari na kuvunja uhusiano wowote kati yake na uchumi wake. Kwa kutabanniwa kwa sarafu inayoegemezwa na dhahabu na fedha, huondoa mfumko wa bei, ambapo hupelekea ustawi wa bei. Kwa kumalizia, Misri inahitaji ruwaza mpya kutoka kwa mtazamo tofauti na mfumo wa kibepari, na mfumo mbadala wenye uwezo wa kuleta mabadiliko, hivyo je hili linaweza kufanywa vipi? Na ni nani anayeweza kulifanya? Ni nani mwenye kubeba mfumo huu?

Misri ina rasilimali nyingi tofauti tofauti, ikiwemo mafuta, gesi, dhahabu na madini mengine. Hata mchanga wake wa jangwa ni hazina ya thamani, pamoja na vyanzo vya maji vilivyo na utajiri wa viumbe vya baharini na viwanda vinavyotokamana nayo, pamoja na maeneo makubwa ya kilimo ambayo yanatosha kwa Misri kukuza mimea yote ya kimkakati inayohitaji yenye kutosha na kwa wingi, haina haja ya kuagiza chakula kutoka nje. Hata hivyo, ubepari na utiifu huzuia Misri kutumia rasilimali zake na kuiwezesha Magharibi kuzipora. Ili Misri iweze kupata rasilimali hizi na kuregesha vyanzo vyake, makampuni ya kibepari yanayotawala vyanzo vyake lazima yafukuzwe na kugawanya mali kwa msingi wa Uislamu. Kwa hivyo vyanzo vya mafuta na gesi na madini mengine na mali iliyozikwa vinaangukia chini ya mfumo wa milki ya umma, ambayo Serikali hairuhusiwi kuwapa umiliki watu halisi au watu mashuhuri, bali ni lazima izalishe mali kutoka kwayo na kuigawa tena kwa raia kwa usawa mali yenyewe au huduma, hakuna tofauti baina ya tajiri na masikini au baina ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu, kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema: «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ، فِي الْكَلَأِ، وَالْمَاءِ، وَالنَّارِ» Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: malisho, maji na moto.”

Dola pia inawawezesha wananchi wake kumiliki na kuimarisha ardhi kupitia kilimo, viwanda na makaazi, na inawasaidia katika njia hii, kubadilisha nishati kubwa ya binadamu kuwa nishati ya uzalishaji na kuwawezesha kutumia maeneo haya na vyanzo vya maji katika uvuvi na viwanda, kama Mtume (saw) alivyosema: «مَنْ أَحْيَا أَرْضَاً مَيِّتَةً فَهِيَ لَهُ» “Anayehuisha ardhi iliyokufa basi ni yake.” Je, Misri itakuwaje basi wakati huo? Je, italalamikia ongezeko la watu au ukosefu wa ajira?

Ama dolari, ni sarafu ya karatasi isiyo na thamani ya dhati ndani yake, na ni ala mojawapo ya Marekani ya kutawala utajiri wa nchi yetu, na njia ya kuwatia watu utumwani. Sio sahihi kuunganisha uchumi au sarafu yake au karatasi yoyote ambayo haikuegemezwa thamani halisi ya dhahabu na fedha, pesa ya serikali lazima iwe dhahabu na fedha au karatasi zinazoziwakilisha, Misri inaweza kufanya hivi kwa urahisi, kwa sababu kihakika ile dhahabu iliyo nayo ina uwezo wa kutoa kwa wingi, na ukweli kwamba sarafu inaegemezwa juu ya dhahabu huipa thamani inayokinga maafa na migogoro na kushughulikia mfumko wa bei, na Sharia iliwajibisha kwamba pesa ziwe dhahabu na fedha, na hufungamanisha hukmu za Shariah kwake katika suala la zakat, hudud, na kadhalika. Na ilikuwa hivyo hadi hivi majuzi, kama mwanauchumi wa Marekani Nathan Lewis alivyo eleza katika utafiti aliofanya mwaka 2011 kwamba Misri ilibaki kuwa nchi kubwa zaidi yenye kifiniko cha fedha cha dhahabu duniani, hasa kutoka mwaka wa 1926 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1950, licha ya kushuka kwa thamani sarafu yake mwaka 1931 kama sehemu zengine duniani katika kipindi hicho kuzipiku nchi zote duniani kwa nguvu ya sarafu yake yenyewe, ikiwemo Uingereza.

Kushughulika na rasilimali, utajiri, hata fedha, mikopo, na kadhalika, kuna hukmu za Shariah zinazosimamia taratibu zake. Uislamu unadhibiti mambo yote ya maisha yetu kwa hukmu za Shariah zinazotokana na imani ya kisiasa inayowiana na ghariza ya mwanadamu ya kutokuwa na uwezo na haja kwa Muumba. hukmu hizi ni dhamana ya kweli kwa watu kuishi maisha ya heshima ambayo ndani yake roho zao zimehakikishiwa. Zilitekelezwa katika karne zilizopita hadi tulipowaona baadhi ya watawala wa nchi yetu wakisema: “Nyunyiza ngano juu ya vilele vya milima ili isisemwe kwamba ndege ana njaa katika nchi za Kiislamu.” Na anaye hutubia mawingu yapitayo mbinguni kwa kusema: “Nyesha upendavyo, kwani kharaj zenu zitaregea kwangu.” Tunahitaji watu kama hawa katika uchamungu wao (taqwa) na katika kuhukumu kwao kwa hukmu za Uislamu, Shariah yake, na mfumo wake. Tunahitaji dola inayotabikisha Uislamu kikamilifu, kwa upana na usiopungua chini ya Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume.

(وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ)

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi.” [Al-A’raf 7:96]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu