Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  13 Shawwal 1444 Na: 1444/15
M.  Jumatano, 03 Mei 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watu wa Sudan Hawana na Hawatakuwa Mgogoro kwa Watu wa Misri, Badala yake, Watu wa Misri na Jeshi Lake Lazima Wawakumbatie na Kuwanusuru
(Imetafsiriwa)

Rais wa Misri Abdel-Fattah El-Sisi alisema kuwa nchi yake "itakabiliwa na athari za kiuchumi na matatizo" endapo itapokea raia wengi wa Sudan, katikati ya mgogoro unaoendelea kati ya pande zinazozozana nchini mwao. Haya yalijiri katika mahojiano aliyoyatoa kwa gazeti la Japan la "The Asahi Shimbun", ambalo lilichapisha makala hayo, jana, Jumanne, 2/5/2023, kwenye tovuti yake, siku 3 baada ya kufanywa katika mji mkuu wa Misri, Cairo, mnamo Jumamosi, 29/4/2023. El-Sisi aliongeza kuwa "Wasudan wengi wanakimbilia Misri na tunakabiliwa na matatizo." Hii ni katika muktadha wa mjadala juu ya migogoro ya kiuchumi iliyoikumba dunia dhidi ya hali ya vita vya Urusi nchini Ukraine, hususan bei za bidhaa na vyakula, aliendelea kusema: “Ikiwa tutawakubali Wasudan wengi zaidi, bila shaka Misri itahisi athari zake.” Aliongeza: "Tayari kuna mamilioni ya Wasudan nchini Misri, lakini hatuwaiti kama wakimbizi bali wageni… Huku kukiwa na matatizo ya kiuchumi yanayotokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Wasudan wengi wamekimbia hivyo Misri pia inakabiliwa na matatizo.” Alisema, "Tayari tunakabiliwa na mfumko wa bei na bei za mahitaji ya kila siku zinapanda." (GBC News 2/5/2023)

Mipaka iliyochorwa na wakoloni wanaotenganisha nchi za Kiislamu haitenganishi watu. Uwepo wao unahusishwa na kuwepo kwa tawala za vibaraka zinazotawala nchi zetu. Misri na Sudan zina takhsisi katika suala hili; Sudan, ambayo ni upanuzi wa asili wa Misri na ilikuwa hadi hivi karibuni chini ya utawala wa Misri. Wengi wa watu wake wanaishi Misri kwa kiasili. Hawakuwa na hawatawakilisha tatizo la kiuchumi kwa watu wa Misri. Badala yake, tatizo halisi ni mfumo wa kibepari unaotabikishwa na utiifu wa utawala kwa Marekani. Wananchi wa Sudan hawakuufanya utawala wa Misri kuomba mikopo kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), wala hawakuilazimisha ishushe thamani ya pauni, wala hawakuiomba iuze mali ya dola hiyo ambayo haina tena uamuzi, kwani uamuzi wake unategemea ishara ya makabaila katika Ikulu ya White House!

Sababu ya kile ambacho Misri inateseka nacho sio kuhama kwa watu wa Sudan, wala vita kati ya Urusi na Ukraine. Ni nani anayeilazimisha serikali kuagiza ngano kutoka Urusi na Ukraine badala ya kulima na kuuza nje?! Na ni nani aliyeilazimisha kukabidhi ya Mto Nile na kuiruhusu Ethiopia kujenga Bwawa Kuu la Ufufuo la Ethiopia?! Na ni nani aliyewalazimisha wakulima kupunguza maeneo ya kulima mpunga?! Na ni nani aliyetumia mabilioni ya pesa kwenye miradi feki, miji hewa, makasri, barabara na madaraja ambayo hayahitajiki?!

Shina la maradhi ni ubepari ambao serikali inautawalisha na utiifu wake kwa Marekani, ambao uliiwezesha kudhibiti uchumi wa nchi, rasilimali, utajiri na hata watu wake ambao wamekuwa chini ya mstari wa umaskini na kuishi maisha ya watumwa katika nchi, au labda baya zaidi.

Serikali ilipata katika kuhama kwa watu wa Sudan kuwa ndio sababu ya kufeli na utasa wake kukabiliana na matatizo ya sasa ya kiuchumi. Ingekuwa bora kwake kunyoosha mkono wa kweli wa msaada kwa watu wa Sudan kwa kukata vichwa vya vibaraka wa Kimarekani wanaopigana na kuiunganisha ardhi yote ya Sudan kwa Misri ili iregee jinsi ilivyokuwa chini ya utawala wake. Lakini hatua hii ya kijasiri haiwezi kuchukuliwa na vibaraka waliotiishwa wa Magharibi, ambao maamuzi yao yamewekwa rehani kwake. Kazi hii inahitaji watu wenye ikhlasi walio na hamu tu na radhi za Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kwa manufaa ya Dini na Umma wao, na hawa ndio tunaowasihi nchini Misri na Sudan, waweke mikono yao mikononi mwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha dola ambayo itauokoa Ummah kwa jumla na sio Misri na Sudan pekee, na kuwanusuru wanaodhulumiwa na kuwapa haki wanyonge chini ya utawala wa uadilifu, dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi Wenye Ikhlasi katika Jeshi la Kinana: Mwenyezi Mungu (swt) amewajibisha juu yenu kuwanusuru kikamilifu watu wenu wa Sudan na kuhifadhi haki na damu zao kutokana na wale wote waliowashambulia. Hakuna salama kwenu kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na hisabu endapo mtamsaliti na itakuwa ni hasara iliyoje kwenu basi, naapa kwa Mola wa Ka’ba. Wajibu wenu sasa ni kuwadhibiti watu wenu kutoka Sudan iwe wale walioikimbia na wakatafuta hifadhi kwenu au wale waliobaki humo chini ya moto wa mapigano yanayoendelea kwa ajili ya Marekani, na hili linahitaji kutoka kwenu kusimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kuwang'oa viongozi wa wapiganaji wa Sudan na kukabidhi, uongozi wake na utawala wake kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu akufungulieni na akupeni ushindi kwa mikono yenu na akukusanyeni katika usuhuba na Manabii, wakweli, mashahidi, wema, na hao ndio marafiki bora zaidi.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَـئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal: 74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu